Unachokisema si kweli....rais hawezi kubugudhi mihimili mingine namna hiyo unayotaka kutuaminisha.
Kukitokea migongano rais hataweza tawala....mihimili mingine ikiamua ku-exercise their power against executive kwa pamoja nchi haitatawalika.
Executive kupeleka hela kwenye hii mihimili mingine sio eti ndio wana mamlaka zaidi ya hiyo mihimili,hii ni myopic view.
Kupeleka hela ni wajibu wa executive kwa hii mihimili,hakuna mambo ya kuomba...nani kakwambia ni hisani ya executive kupeleka hela judiciary na parliament?
Mnajua nyie mna matatizo...huwezi kuhemea mihimili mingine namna hii as if hii mihimili ni wake wako unaweza fanya utakacho...
Unaweza jenga ego na hasira kwenye hii mihimili mingine na hiyo ikulu ukaicha ukaenda Chato kulima...tatizo mnajifanya nyie executive ndio mna ego kubwa sana,mtasababisha friction na nyie ndio mtafeli..
Kwanini masiendeshe nchi kwa inclusion na power brokerage kila mtu akajiona anatakiwa kichangia na yupo included na anaheshimika?Nchi huwezi ijenga peke yako,huwezi,nguvu hizo hamnazo.Nchi ni watu kama wewe na wana uwezo kama wako au zaidi,treat people with respect and honest.Acheni kulewa madaraka mapema hivi.
Hodi hodi mwana wane naingia kupitia mlango wa nyuma..
Jamani kwanza mfahamu ya kwamba Katiba yetu imeandikwa kwa muundo gani kisha ndio tujenge hoja zetu kwa sababu NENO KUTOINGILIA halina maana kuweka USAWA wa KIMAMLAKA. Nachoelewa mimi ina maana kwamba mhimili mmoja hauwezi kuingilia shughuli za mhimili mwingine hivyo rais kama kiongozi wa Serikali ataifanya kazi yake ya shughuli za serikali pasipo kuingiliwa na Bunge ama Mahakama.
Mfano:- Bunge linalokaa na kujadili sheria ama kupitisha Muswada, rais na Mahakama hawana mamlaka ya kuingilia shughuli hiyo. Pia Mahakama inapofanya shughuli zake za kimahakama Rais na Bunge hawaruhusiwi kuingilia maamuzi ya Mahakama. Tofauti na Katiba ya Marekani ambayo Bunge na Mahakama zimeundwa ili kupunguza nguvu za kimamlaka (Power) ya rais na hivyo kwa kila shughuli za Serikali kuu vyombo hivyo vinahusika kwa njia moja ama nyingine (President Executive order or Proclamation)
Kwa wenzetu huwezi kuona mikataba ikiwekwa na nchi za nje pasipo Bunge au Mahakama kupitia, sisi majuzi tu Magufuli katangaza kughairisha sikuu za Uhuru na Muungano na ikawa. Tumeingia mikataba 21 na Morocco, ni mhimili gani umehusishwa? ama ni kifungu gani cha sheria kinachomkataza ama kusema Bunge linaweza kuingilia? Bila shaka sheria inasema wasiingilie sio waingilie. Sijui kaa nakosea lakini ndivyo nachoelewa mimi. Toka mikataba ya Buzwagi, Bulyanhulu hadi Richmond walihusishwa?
Leo hii ndio tumegundua kumbe hata mkataba wa India kuna mazao ambayo tunatakiwa kuzalisha nchini soko limeshapatikana India na fedha zipo mikononi mwetu, nani alijua hayo?. Labda nirudi nyuma kidogo, Magufuli alipopitisha Elimu bure hadi Sekondari lilijadiliwa lini bungeni? Kwa hiyo, kwetu sisi ilani yachama ikisha pita na wananchi kumchagua rais, kinachojadiliwa ni FEDHA TU. Wizara gani imepata kiasi gani na sio mambo gani yatafanyika.
Leo hii tumetangaziwa nchi ya Viwanda! Nini lengo la kuanzisha viwanda nchini ikiwa hatuna masoko nje? Je ni kukimu mahitaji yetu kwa nini wawekezaji watoke nje ama kuuza nje na kama nje tutauza vipi? tumejiandaa vipi kwa masoko nje ya EAC.inaonyesha wazi kwamba wananchi wengi walikuwa hawajui kinachoendelea, hata hao waandishi wa Habari. Kwa maana pana zaidi Bunge lipo pale kupitisha Bajeti tu ya serikali, nimeshangaa hata incentives zinazotolewa waandishi wa habari hawazijui wakaulize wapi vile!.