Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Watu wanapolilia katiba mpya mnawaambia katiba haina maana yoyote
 
Rais kajibu vizuri sana,naMayala hakuwa amesoma katiba na kuielewa...yawezekana ametumia uzoefu wa kijiweni kwake,au magazeti ya udaku...
Kifungu kipi cha katiba kinampa mamlaka rais kuingilia muhimili wa mahakama na bunge?
 
"Mayalla oye" Magufuli
 
Head of state ni katiba inayomwongoza katika kuongoza siyo yeye ndiyo maana hakuna aliye juu ya sheria usituchanganye maswali ya Pasco kajibu moja tu mengine kayakwepa
 
Kwani hii mihimili mitatu tunaposema 'Inajitegemea' ina maana gani?...

Mwenye kujua anieleweshe tafadhali..
 
Mkuu Pasco hongera sana kwa kuuliza swali lenye Mashiko na utashi wa hali ya juu.Kwa imani yangu muulizwa swali kamwe haji kukusahau.Kila akiwaza mambo ya Bunge,Mahakama na serikali atakukumbuka tu.Pia wewe Muungwana sana Kwani ukuitupa mbali JAMIIFORUMS ulijieleza kuwa Mwanachama wa JF.Mungu atakulipa mkuu
 
mfano leo ungebahatika kuwepo kwenye kikao cha waandishi na mh:rais ungemuuliza swali gani lenye tija kwa taifa.karibuni
 
Ni mwandishi pekee aliyeuliza swali bila hofu! Nampongza Tido kwa kusisitiza dhana ya Udikteta
 
Kwanza kusema kweli katika kumuunga mkono Pascal Mayalla pamoja na kumpiga kijembe asli ya jina lake lakini maswali yake yalielekea kama yamemkera kwa nilivyofuatilia hotuba yake na majibu yake ya jumla jumla katika kujibu nimegundua kitu ambacho watu wengi hawajakigundua kwa hulka ya Rais wetu kuna kitu kinamkera lakini inaonekana hana jinsi afanyeje katika nchi hii anataka yeye ndiyo apewe heshima kusifiwa na kuabudiwa anapoonekana kuwa siyo peke yake anayetetemekewa kuna mtu mwingine akionekana naye anapewa heshima kama kiongozi wa nchi kinamkera sana nadhani ndicho kinachopelekea apige marufuku mikutano ya hadhara kwa sababu umaarufu wake utaporomoka hicho ndicho nilichokigundua kwa mwendo huu itabidi wakubali yaishe maana hata kwenye mkutano huu karudia tena kutamka ni kipindi cha kuendeleza nchi siyo mikutano
 
kwajinsi ulivyomtwanga muheshimiwa yale maswali nilijua tu majibuyake yatakuwa mepesi big up pasco waandishi wote wanapaswa kuiga mfano uliouonyesha Leo unajiamini sana nimekupenda bure
 
Pasco kuwa Muungwana Mkuu kwa kuja na ku Acknowledge na kutoa Shukran kwetu wana JF
Ona sasa Mjadala Mzima kule wa Mkutano wa JPM ume Cease watu tuko Busy kwenye huu uzi kuona Jinsi ulivyoleta Faraja leo
 
Kifungu kipi cha katiba kinampa mamlaka rais kuingilia muhimili wa mahakama na bunge?
Kifungu kinachompa mamlaka rais ni kuanishwa kwa majukumu yake, kuwa Serikali ndiyo mkusanyaji mapato na msimamizi wa matumizi ya pesa, kwa maana hiyo muajiri mkuu ndiye anayebuni vyanzo na ndiye anayesimamia matumizi ya mapato hayo. Udhibiti wa Safari za nje lengo lake ni udhibiti wa Matumizi ya pesa ya umma ambapo mihimili mingine yote inaomba pesa toka kwa muidhinishaji mkuu ambaye ni rais. Makosa yetu ni kudhani mihimili mingine imeingiliwa kwa kuzuiwa kusafiri tu hatuendi mbali na kujua udhibiti huo wa safari lengo ni kudhibiti matumizi ya fedha za umma ambazo zingeweza kutumiwa kwa shughuli nyingine za muhimu zaidi. Hii NDIYO MAANA YA MAJIBU YA RAIS kwa Pascal Mayalla
 
Magu kashindwa kujibu maswalo anaipigia promo Clouds.
 
Pasco kuwa Muungwana Mkuu kwa kuja na ku Acknowledge na kutoa Shukran kwetu wana JF
Ona sasa Mjadala Mzima kule wa Mkutano wa JPM ume Cease watu tuko Busy kwenye huu uzi kuona Jinsi ulivyoleta Faraja leo
Una uhakika yuko salama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…