Nilishawahi kusema,haiwezekani mahakama iitwe muhimili huru
wakati mkuu wake ambaye ni jaji mkuu ni mteule wa muhimili
mwingine(rais). Na kama jaji mkuu ni mteule wa rais,huenda akikorofisha anaweza
kutolewa jipu na aliyemteua,hapa uhuru wa huu mhimili uko wapi?
Chukulia kama unaitwa baba,alafu kuna mtu anaweza kuja kukuchapa viboko
mbele ya wanao na mkeo na maisha yakaendelea hapo kuna uhuru!au wewe ni mtumwa
wa huyo aliyekuchapa?
Majaji wote ni wateule wa rais,kama kweli mhimili huu ni huru
ni kwa nini jaji mkuu usiteue/kupitisha wanasheria wenye viwango wawe majaji
badala yake rais ambaye si mtaalam wa mambo ya sheria na ni mkuu wa serikali
ndo hutangaza wanasheria kupanda na kuwa majaji?