Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Magufuli amejitahidi kujibu maswali vizuri lkn maswali ya Pasco, JPM hakuweza hata kujaribu kujibu swali la pili.

Vv
 
PASKAL MAYALA!! MAN OF THE YEAR! SO PROUD OF YOU BROTHER....!!
 
Wahariri wa Tanzania bana vichekesho kama kina sunche na kapeto hamna jipya bora hata Nape anavotaka kuwafanya ninyi! Yani nyinyi ni vihiyo kabisa!
 
Pasco kuwa Muungwana Mkuu kwa kuja na ku Acknowledge na kutoa Shukran kwetu wana JF
Ona sasa Mjadala Mzima kule wa Mkutano wa JPM ume Cease watu tuko Busy kwenye huu uzi kuona Jinsi ulivyoleta Faraja leo
Kuna swali lakujiuliza nitoke vipi? paskal Mayala au Pasco wa JF
( aah natania tuu)
 
Kauliza vizuri lakini sasa mjibu swali kaingiza matani na kuliondolea maana
So he is
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?
Just because he is the head of Governmet and the State, is he entitled to break the law?
 
Wakuu kama mnakumbuka mdau mbishi wa Katiba ya Warioba Bwn.Humphrey Polepole alipewa ukuu wa Wilaya.Hii ilitafsriwa kuwa ni kumziba mdogo bwana huyu kwa kutumia kipande cha keki.Bwana yule hakuna na uwezo wa kutema kile kipande utamu ukamzidia Leo hii ni DC wa Ubungo cheo ambacho alikipinga sana akiwa timu ya Warioba.

Sasa from Nowhere amekuja Mwana JF mwenzangu Pasco,amevuma sana Leo mitandaoni.Paskali amehoji mambo magumu sana na hayakupata majibu,si kwa bahati mbaya,bali hakukuwa na majibu.

Je,mbinu iliyotumika kumrambisha udambwi-dambwi H.Polepole au Dr. Ryoba utatumika kwa Msukuma Paskali?

Ombi:Kwa kuwa Paskali amewahi kutuambia humu kuwa yeye hana shida na cheo kwa kuwa ana kipato kinachomtosha,Je uyaendelea na msimamo wako. Je,unamshauri nini Polepole kwa yale majibu ya Rais Hakuna katiba mpya?
 
Swali kutoka kwa Mr. Mayala.
Mh. Rais uliapa kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TZ, Je ulipata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya siasa wakat katiba haikupi nafas ya kufanya hivyo?
Jibu....
Mayala kwa kisukuma ni njaa! Yawezekana ww Mayala ulizaliwa kipindi cha njaa! Wote wakacheka[emoji16], akaendelea....
Mh. Mayala uliwahi kujiuliza kwa nn hotuba yangu ya kwanza ya kubana matumizi niliitolea Bungeni Mbele ya Spika? Ukijua mpikaji wa chakula ni nan na mgawaji wa chakula ni nan bas utanielewa.

Hilo jibu la swali lililoulizwa , cjui kama ni vinaendana.
[emoji81][emoji81][emoji81][emoji81][emoji81][emoji81][emoji81][emoji81] yaaan issue n kwamba anajaribu kucomplicate ........anatumia ka falsafa fulan HIV kwamba if they don't want to understand yhu complicate them[emoji81]
 
Kauliza maswali mazuri yaliyojibiwa kirahisi mno.
Kasema maslahi ya nchi kwanza mengine baadae, inamaana hata kama tunavunja Katiba tuendelee tu?
Mh. Rais kajibu vizuri sana swali la Pasco ile asijue sheria hawezi kufahamu kwamba swali limejibiwa. Mh Rais alianza kujibu swali kwa kuuliza swali, mfumo amvao hutumiwa na wanafalsa kuwafanya waliouliza maswali kupata majibu yao kwa kujibu swali walilouliza.
Mh Rais alimuuliza mbona hukuuliza kwa nini nilikwenda kuhutubia bungeni??
Kama yuko smarti bila shaka atapata jibu kupitia ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tz ambapo inasomeka hivi[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]

Ibara ya 62.

Ibara ndogo ya (1),
Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.

Ibara ndogo ya (2),
Bunge litakuwa na wajumbe wa aina zote zilizotajwa katika ibara ya 66 ya Katiba hii ambao wote wataitwa Wabunge.

Ibara ndogo ya (3),
Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na sehemu zote mbili za Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katika hii au masharti ya sheria nyingine yoyote, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vile vile na Rais, kwa mujibu wa madaraka yao kuhusu jambo hilo.

Katiba ya Tanzania - Android Apps on Google Play
 
Ya Slow Slow na katiba Mpya kupinga Nafasi za u DC na yeye kupewa u DC inanikumbusha ule usemi "Mchawi/ Mwanga Mpe Mwanao akubebee"
Hatokaa amroge asilani
 
Sina hata hamu na hizi habari baada ya kusikia "ajira zilifunguliwa miezi miwili baada ya kufungwa" nimechoka kabisa yani.....
 
ningeuliza chooni ni wapi nikanye niweke historia nishawahi kunya ikulu

maana maswali hayajibiwi
 
Mihimili inatakiwa kufanya kazi kwa kuheshimiana kwa kutumia system of checks and balances.
Bunge likiamua kumuondoa Rais madarakani inawezekana, tena kwa kufuata katiba.
Hata hivyo, ugoigoi wa mhimili mmoja husababisha kuonekana mwingine uko juu zaidi.
Yawezekana, Rais Magufuli kama alivyo Magufuli John Joseph Pombe, angekuwa ndiye kiongozi wa Bunge au Mahakama, mhimili wake ungeonekana kuwa juu kuliko serikali (Rais).
 
Ukiiangalia Nchi ilivyo haiitaji hata maswali labda labda ingekua kwa Rais mgeni alietoka Nje huyu tunae hapa kila siku Vumbi analiona angetoa maelezo tuu maana hata hayo maswali hajajibu wa TBC kaishia kuuliza unapendelea nini mkuu..
 
Huyu huyu Pasco ninaemchukia kumbe wakati mwingine anaakili....Hongera Pasco ila ninaswali bado utapewa udc kweli au uded maana umempiga Mkuu Wa kaya chini ya belt
 
Back
Top Bottom