Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Nchi tunaipenda ni ya wote na kumbuka Rais ni binadamu siyo Mungu anamazuri yake na mapungufu pia.
 

Habar wajamen!!.

Nimetoka hapa Kigamboni nikiwa kwenye daladala,nikakuta watu wanajadili na kubishana kidogo kama mrejesho wa mkutano wa jana kati ya rais na wanahabari;lakini pamoja na maswali mengine watu wengi nimeona wanamtaja sana huyu Mayala,kuwa aliuliza swali zuri japo Rais hakumjibu badala yake akaishia kutafsri jina la Mayala kulingana na kilugha chake.

Mim binafsi huyo Mayala ndio nimeanza kumjua jana ,yaani mkutano wa jana ndio umenifanya nimjue kwani hata kama niliwahi kumskia basi sikuwahi kuchukua muda mwingi kukaa nikafikiria chochote kumhusu.

Swali alilouliza Mayala,basi hapa kwenye daladala(UDA tupo takribani abiria45-56) wote wanaonesha kuunga mkono swali la huyu Mayala,na zaidi kuonesha kuwa hawakurdhika na majibu aliyotoa Rais.

Naskia swali lilimtaka Rais ase me au ajibu kuwa kwakuwa Taifa,linamihimili mitatu,yaani Bunge,Mahakama na Serkali yenyewe kama cjakosea,akaulizwa yeye kama Rais ni mhimili mmoja tu kati ya hizo tatu,na kikatiba mihimili hio inajitegemea,

Rais aliapa kuilinda katiba,je anatumia mamlaka gani kutoa matamko yanayopenya hadi kwenye hio mihimili mingine?..

Lakin pia Rais aliulizwa kuhusu Kutoa matamko ya kuzuia mikutano ya kisiasa.

Rais alioneshwa kuchukizwa na swali hili,na kuthibitisha hili alimshambulia muuliza swali kwa kutafsiri jina lake kuwa lina maana 'njaa' kulingana na kisukuma,na aliendelea kwa kumwambia swali alilotegemea amuulize.


Hii ilitakiwa kuwa ati angemuuliza kwanini alihutubia kwa mara ya kwanza bungeni? Sasa sijui kuhutubia bungeni ndio kulimaanisha amepewa mamlaka ya kuingilia mihimili mengine? Bila shaka hapana..

Jibu lake lilikuwa rahisi kuwa ati "anafanya yote kwa sababu anabana matumizi",
hivi anabana matumizi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani?.....how does this work?
 
Out of order
 
...kwanza ni kupomgeze Pascal Mayalla kwa kuuliza maswali mazuri aka ya msingi...pili,nashindwa kumtofautisha mjibu maswali ya Pascal na yule kijana aliyechora mazombi kwenye karatasi la kujibia maswali ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne...
 
Kama katika marking kungekuwa na negative rating ningekupa (-100%) kwa huu UP ulioenda. Chukua 0% yako inakutosha kwa hilo jibu lako
 
mengine alipoulizwa akiambiwa eti ya kichokozi.

lakini mayala nampa bigup sanaaa.

tungekuwa nao kama kumi na yule aliyeuliza wa bbc namwingine kahusisha zanzibar
 
....sidhani kama ataalikwa tena ikitokea mkutano mwingine, na hata akialikwa nahisi atapewa muongozo bhahahhaaaaa....
 
Kuna maswali ukiuliza tuu utajulikana kama umetumwa alafu yanashusha cv yako muda mwingine bora unyamaze ili watu wajue huna swali kauliza upuuzi tuu
 
1.Kuwa head of state maana yake ni kuingilia mihimili mingine? 2. Unakubaliana na kinachofanyika kwa kuwa kinafanywa na head of state?
Kuingilia kwa maana gani? Kwamba wakitaka kusafiri inabidi wapate state house clearance ni kuingilia muhimili mwingine? Hufahamu kwamba utaratibu huo upo siku nyingi?
 
Kuingilia kwa maana gani? Kwamba wakitaka kusafiri inabidi wapate state house clearance ni kuingilia muhimili mwingine? Hufahamu kwamba utaratibu huo upo siku nyingi?
Rejea swali la Mayala!
 
Hahahaha mkuu mi mwenyewe nilikua napata shida nilikua nikidhani ni huyu wa jf, kumbe huyu wa jf ni mropokaji wa humu tu hana lolote, shame on him
Yeye mwenyewe kabla ya maswali yake kwa rais alijitambulisha ni member mwandamizi wa Jamiiforums
 
Ni wawili mkuu, Sami Awami wa BBC naye kamchapa swali la Demokrasia ameshindwa kujibu kifasaha. Maswali magumu anapanic.
Ogopa sana kuujua ukweli na undani wako.Mapungufu yako,kama anayekueleza anaeleza taratibu kama Mayalla.Unaweza anguka ghafla.Mayalla ameuliza baadhi ya mapungufu ambayo kila mtu anayo.Binafsi ningeunga unga tu majibu.Ila ukweli utabaki kama hivi,Baba atimize majukumu ya familia kama ilivyo siku zote.Mama na atkmize wajibu wake kama mama.Na watoto pia wathamini majukumu yao.Hapo ndipo familia huwa bora.Nchii yetu ni mfano wa familia flani hivi.Baba kuwa mkali sana haimaanishi utaogopwa.Hapana wote tutakaa pembeni huku tukiiga ukali wako.Na kusema ngoja tuoone mzee atafikia wapi.Kuongoza watu hasa kizazi hiki cha nyoka.Huhitaji nguvu kubwa ya kuongea na vitisho.Ndio maana kila kukicha mitaa inazidi kubadilika na matatizo hayaishi.Wajifunze kuepuka ushabiki na kuja ghafla na matamko ambayo yana athari kubwa kwa raia.Hasa wasio kuhitaji.
Muda unaenda na hali inazidi kuwa ngumu.Waangalie na hayo pia si kila kitu ni kupinga.Hakuna Mungu hapa Duniani wala asiyekosea.Mkuu wa nchi unafanya mazuri tunayaona.Ila pia pokea mapungufu yako sio dhambi.Sikiliza pande zote na tazama kwa sasa jamii yako inavyoishi.
Tukiendelea na kauli za kuudhi na tukaonekana wachache ndio tunaiongoza nchi.Hata wanaotuzunguka watatuangusha haraka sana,hasa kimaendeleo.Watakuongelea kuwa upo vyema kumbe wanatumia huu muda wa sisi kutokueleweka.Nini tunahitaji.
ANGALIA KUPOLOMOKA KWETU NI FAIDA KWA NCHI JIRANI.NA WATAZIDI KUKUSIFIA ILI MUDA UENDE.TUREKEBISHE TUNAPOKOSEA HARAKA.HII NCHI SI YA MTU MMOJA.
 

Kwa nini mnaunganisha matukio juu juu?

Mpaka Humphrey anapewa ukuu wa wilaya alikuwa tayari alishawapiga chini UKAWA, na kwenye kampeni aliongea pumba sana na zile ndo zimempa ukuu wa wilaya.

Alishabadilika zamani sana na kuongea ongea pumba ndo baadae kalipwa.
 
mkuu,
vp mahakamani,hoja kama hii inaweza kukubarika?
 
Hakuna njia rahisi ya kummaliza mtanzania kama kumpa cheo/ulaji/uheshimiwa..

Misimamo yake yote inasambaratika na kutokomea kusikojulikana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…