Ngoja tumalize kuweka data vizuri!! Watanzania watamjua Paskali ni nani. Huyu ni Mr. NJAA Kama maana ya Jina lake ktk lugha ya kisukuma. Na NJAA NI LAAANAAA!!
Queen Esther
Queen, nina mashaka kama unamjua Pascal kiasi hicho unachotaka kutuaminisha. Kwa vile tu kasema kile usichokipenda wewe basi amekuwa Mr. NJAA. Si kweli, Pascal tangu akiwa DTV na kipindi chake maarufu cha KITI MOTO ndipo nilipoanza kumjua ni mtu wa namna gani. Hakuna mgeni/kiongozi yeyote aliyekuwa anaalikwa kwenye hicho kipindi asipate wakati mgumu wa kujibu maswali ya Pascal. Sio mtu wa kuuliza maswali ya kumpamba mtu. Na sauti yake ni hiyohiyo na kama wewe uliona sauti aliyotumia kumuuliza swali JPM ni ya ukali ni dhahiri humjui huyu Pascal.
Unapokuwa na ujasiri na kujiamini na kuamini pia unachasema, unaweza kumuuliza mtu swali lolote bila uoga ili mradi tu uvunji sheria wala kumdhalilisha. Swali la Pascal lilikuwa very clear wala hakuzunguka kama wengine walivyokuwa wanazunguka. Lilikuwa ni swali la kikatiba na majibu yake yalitakiwa yawe ya kikatiba. Sijaona mahali ktk katiba inamwelezea rais kama General Pay Master( GPM) kama unavyodai wewe. Nakubaliana na wewe jambo moja tu, ni kweli katiba iliyopo sasa hivi issue ya separation of power haipo. Inazungumzwa lakini uhalisia siyo hivyo. Na ni kweli ndio maana majaji badala ya kufanyiwa vetting wanateuliwa na rais, wabunge wanakuwa mawaziri na mengine mengi siwezi kueleza yote. Lakini katiba hiyo hiyo haimpi mamalaka rais kuwafuta kazi majaji. Ni maajabu mengine hayo mtu uliyemteua huwezi kumfuta kazi. Kama ilivyo kwa wabunge, wananchi waliomchagua mbunge hawawezi kumwondoa mbunge waliyemchagua hata kama hatimizi wajibu wake.
Kwa kumalizia, sijaona kosa la Pascal, sijaona njaa ya Pascal. Ninachokiona kwake ni kujiamini, kutokuwa mwoga na kuwa na msimamo na ujasiri wa kusema kile anachokiamini hata kama wengine hawaamini hivyo. Na haiwezekani pia kila unachosema Pascal kikubalike na kila mtu, lakini ukweli haujifichi utaonekana tu, kama ulivyo uongo na unafiki.
Mwisho kabisa, eleza hicho unachosema unakijua juu ya Pascal acha kuzunguka, kama kina ukweli kuwa jasiri na eleza. Usilete habari ya Pascal ni Mr. NJAA, na NJAA NI LAANA. Hapo hujaeleza bado. Unaogopa nini kama kuna ukweli?