Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

We don't need world bank to finance projects we need mafisadi CCM kutufadhili watanzania. CCM pesa ndefu ya ufisadi usiseme mwanangu.
 
Mbona unaonekana una hasira sana mkuu kwa Mwandishi Msomi Hon Pascal Mayalla? Samahani lakini, wewe ni mwandishi wa gazeti la chama??
Ukweli utabaki kuwa ukweli tu..swali la Mayalla liligonga mfupa na ndio maana hata majibu yalikuwa blah blah yani kwa kifupi swali halikujibiwa..

Kwa mtu asiyeelewa chochote kuhusiana na doctrine of separation of powers ndio anaweza kutumia zile blah blah eti kuitwa kuhutubia bunge kutoa muelekeo, kuombwa hela na mahakama kama majibu ya swali la Mayalla!
 
Kati Ya Pascal Mayala na Bwana yulee wa awamu iliyopita nani alistahili kupewa Udaktari wa heshima?
 
Ngoja tumalize kuweka data vizuri!! Watanzania watamjua Paskali ni nani. Huyu ni Mr. NJAA Kama maana ya Jina lake ktk lugha ya kisukuma. Na NJAA NI LAAANAAA!!

Queen Esther
Queen, nina mashaka kama unamjua Pascal kiasi hicho unachotaka kutuaminisha. Kwa vile tu kasema kile usichokipenda wewe basi amekuwa Mr. NJAA. Si kweli, Pascal tangu akiwa DTV na kipindi chake maarufu cha KITI MOTO ndipo nilipoanza kumjua ni mtu wa namna gani. Hakuna mgeni/kiongozi yeyote aliyekuwa anaalikwa kwenye hicho kipindi asipate wakati mgumu wa kujibu maswali ya Pascal. Sio mtu wa kuuliza maswali ya kumpamba mtu. Na sauti yake ni hiyohiyo na kama wewe uliona sauti aliyotumia kumuuliza swali JPM ni ya ukali ni dhahiri humjui huyu Pascal.

Unapokuwa na ujasiri na kujiamini na kuamini pia unachasema, unaweza kumuuliza mtu swali lolote bila uoga ili mradi tu uvunji sheria wala kumdhalilisha. Swali la Pascal lilikuwa very clear wala hakuzunguka kama wengine walivyokuwa wanazunguka. Lilikuwa ni swali la kikatiba na majibu yake yalitakiwa yawe ya kikatiba. Sijaona mahali ktk katiba inamwelezea rais kama General Pay Master( GPM) kama unavyodai wewe. Nakubaliana na wewe jambo moja tu, ni kweli katiba iliyopo sasa hivi issue ya separation of power haipo. Inazungumzwa lakini uhalisia siyo hivyo. Na ni kweli ndio maana majaji badala ya kufanyiwa vetting wanateuliwa na rais, wabunge wanakuwa mawaziri na mengine mengi siwezi kueleza yote. Lakini katiba hiyo hiyo haimpi mamalaka rais kuwafuta kazi majaji. Ni maajabu mengine hayo mtu uliyemteua huwezi kumfuta kazi. Kama ilivyo kwa wabunge, wananchi waliomchagua mbunge hawawezi kumwondoa mbunge waliyemchagua hata kama hatimizi wajibu wake.

Kwa kumalizia, sijaona kosa la Pascal, sijaona njaa ya Pascal. Ninachokiona kwake ni kujiamini, kutokuwa mwoga na kuwa na msimamo na ujasiri wa kusema kile anachokiamini hata kama wengine hawaamini hivyo. Na haiwezekani pia kila unachosema Pascal kikubalike na kila mtu, lakini ukweli haujifichi utaonekana tu, kama ulivyo uongo na unafiki.

Mwisho kabisa, eleza hicho unachosema unakijua juu ya Pascal acha kuzunguka, kama kina ukweli kuwa jasiri na eleza. Usilete habari ya Pascal ni Mr. NJAA, na NJAA NI LAANA. Hapo hujaeleza bado. Unaogopa nini kama kuna ukweli?
 
KITENDO CHA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII, MABAA NA TV KUWA YEYE TU NDIO AMEULIZA SWALI ZURI KULIKO WAHARIRI WOTE WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI NI KASHFA KUBWA KWA TASNIA YA HABARI NA JAMII YOTE!!

Queen Esther
Hivi ni kweli amefanya hivyo? Nilidhani ni wana mtandao wenyewe waliompa sifa hiyo?
 
Kama kuna mtu anafagilia maswali ya mayala...yafaa naye apimwe akili!mayala amedhihirisha jinsi alivyomweupe kichwani japo alijambulisha kama mwanasheria....mwanasheria gani hajui katiba ya nchi yetu!unamuuliza Rais...nani amekupa mamlaka/kwa mamlaka gani unafanya haya......kichwani yuko vizuri huyu?hujui mamlaka ya Rais?hujui Rais anapewa mamlaka na nani?ni dhahiri taaluma hii imevamiwa!
Unadhani aliuliza kwa sababu hajui,au alikuwa ana mwambia rais afuate katiba,yale maswali yalikuwa yanaujumbe mzito sana.

Na kwanin Mayala amekuwa maarufu ghafla juu ya swali lake,kwa sabb wananchi wanaona ombwe ka rais kwenda tofauti na katiba alioapa mwenyewe kuilinda.

Sema ukiwa unaegemea upande fulan wa shilingi lazima uone mayala ana njaa!!
 
Kama kuna mtu anafagilia maswali ya mayala...yafaa naye apimwe akili!mayala amedhihirisha jinsi alivyomweupe kichwani japo alijambulisha kama mwanasheria....mwanasheria gani hajui katiba ya nchi yetu!unamuuliza Rais...nani amekupa mamlaka/kwa mamlaka gani unafanya haya......kichwani yuko vizuri huyu?hujui mamlaka ya Rais?hujui Rais anapewa mamlaka na nani?ni dhahiri taaluma hii imevamiwa!
Povu la Lumumba hili...Wewe ndo mweupe kabisa hata hiyo katiba huijui kaz kula buku 7 za Lumumba tuu....Kila mhimili umetatwa kwwnye katiba na mipaka yake imetajwa kabisaa...sasa siku nyingine kma hujui kitu tulia uambiwe..Acha kusoma makabrasha ya Lumumba chukua katiba usome.nymbaf
 
Kwa mtazamo wangu,kama kweli jina MAYALA maana yake ni njaa
Ndugu Pascal alistahili kupewa jina hili.
kwa nini nasema hivyo,kwa sababu njaa huwa haichagui mtu
wa kumkabili.Haiogopi cheo wala mamlaka.Ukikosea utaratibu
wa kutokula kwa muda muafaka inakukumba tu.

Sasa huyu Bwana Mayala alidhihirisha ujasiri kama wa njaa,
hakuangalia cheo wala madaraka,alisimamia na kuuliza
swali ambalo wengi wangepata nafasi waliyopewa wahariri
wangeuliza maswali yale.

Nampongeza tena Bwana njaa,na tabia ya njaa
huwa haina unafiki,ukipita maeneo yake inakukumba tu.
hivyo wahariri wengi waige mfano wa Bwana huyu
kwa kusimamia mambo ya msingi pindi wapatapo nafasi adimu.
 
Back
Top Bottom