Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hakujibu swali huyu. Ni wapi alipata hii dhana kwamba kwa kuwa Serikali inatoa pesa kwa Bunge na mahakama basi Serikali inastahili kuminya uhuru wa mihimili hii muhimu miwili? Na hizi pesa si zake wala za Serikali bali ni za walipa kodi nchini ambao tunataka kuona mihimili hii miwili inakuwa huru bila kuingiliwa kwa namna yoyote ile na Serikali. Majibu yake yote ni majibu uchwara. Hongera sana Pasco ila nimeshangaa sana maswali mengi muhimu hayakuulizwa labda maswali hayo yalikataliwa yasiulizwe. Hapa Majanga tu hana jipya hata chembe.

 
Binafsi katika maswali yote hilo la Paschal Mayalla nililipenda sana. It was a critical question.
Akanikumbusha pia enzi zile anaeendesha kipindi cha KITIMOTO.

Hongera Pascal Mayalla
 
mkuu alifaulu vipi mitihani mpaka kuwa dokta? ameulizwa katoa wapi mamlaka ye anajibu kutoa maelezo ni kwanini aliingilia mihimili mingine. swali ni where ...... ye anajibu why .....
 
Naomba nimpe pongezi zangu pia nimependa the way alivo uliza na swali lake pia,yangekuwa ya dizaini ile press ingevutia zaidi
 
Tuache wivu
 
Binafsi swali la Sammy Awamu alilomuuliza rais magufuli limekuwa chachu na nimeliona la maana zaidi.

Ni mwandishi gani ameuliza swali lililokukonga moyo wako na lenye maslahi mapana kwa nchi yetu?
SAMMI anafanyakazi BBC havizii uTEUZI hawa wapuuzi wanaogopa kuuliza maswali ya maana wakiamini watakumbukwa
 
Humu mulisema kuwa watakaouliza maswali wote wameandaliw hii n maana kuwa hata pasco ameandaliwa pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…