BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Hakujibu swali huyu. Ni wapi alipata hii dhana kwamba kwa kuwa Serikali inatoa pesa kwa Bunge na mahakama basi Serikali inastahili kuminya uhuru wa mihimili hii muhimu miwili? Na hizi pesa si zake wala za Serikali bali ni za walipa kodi nchini ambao tunataka kuona mihimili hii miwili inakuwa huru bila kuingiliwa kwa namna yoyote ile na Serikali. Majibu yake yote ni majibu uchwara. Hongera sana Pasco ila nimeshangaa sana maswali mengi muhimu hayakuulizwa labda maswali hayo yalikataliwa yasiulizwe. Hapa Majanga tu hana jipya hata chembe.
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.
Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.