Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Kamuuliza kuwa kapata wapi mamlaka ya kuzuia safari za watumishi nje wakati kuna mihimili mitatu na yote inajiongoza yenyewe? Pia kwa nini mikusanyiko ya kisiasa inatambulika na katiba lakini yeye kaizuia wakati aliapa kutumikia nchi kwa mujibu wa katiba?
Kama wangekuwepo hata watano tuu wenye mwelekeo wa Pasco hakika angependa hayo masaa mawili ya ishe aondoke, lakini kwa vile waliopo wengi ni makanjanja basi kawaambia waulize mpaka wachoke wenyewe.
Lizbon hajauliza kuwa kuna watu wana Imani na ukwa??? Je rais unalisemeaje
 
Kijana ameuliza swali ambalo pamoja na kwamba lilikuwa swali zuri la mwandishi wa kweli, lilijikita kwenye katiba, utendaji na madaraka halisi ya Raisi, utengano wa utawala kati ya bunge,mahakama na Ikulu.

Ukweli ni kwamba Pascal alimfanya rais kuhamaki na kupandisha jazba , hasa kutokana na majibu ya vijembe aliyokuwa anatoa na kukimbia kujibu swali la msingi.

Kama mle ndani tungepata wanahabari walau kumi tu kama Mayalla taifa lingekuwa limetendewa haki.

Asante Sana Pascal Mayalla
 
Kweli Mayalla ameuliza maswali ya msingi sana na bahati mbaya rais amekwepa kujibu swali kuhusu kuzuia shughuli za kisiasa na Tido kachangia kwa kulipotezea swali hilo na kukimbilia kwenye swali jingine

Tido ni mzoefu alishaona kuwa JPM angepata shida sana kulijibu hilo swali la pili la Pasco na ndio maana akaingilia kati na kulipotezea!!
 
Wakuu JF Amani iwe Nanyi.

Sina mengi ya Kuongea, ila Hongera sana Mwana JF kwa Pascal kwa Maswali yako Mujarabu Kabisa
Wangepatikana watu kumi kama wewe Leo Pale Pangechimbika, Ki Msingi swali lako halikuwa na Majawabu.
JF Mubashara leo ilikuwa Bora kuzidi Vituo vyote vya Habari including kile kinachoendeshwa kwa PAYE zetu.
Nimefuatilia Live Coverage through JF Bila Chenga, kwingine ilikuwa ni Full Chenga.
JF is everywhere, imetisha Mpaka ndani ya Jumba Jeupe

Muwe na Siku Njema

Note

Mods Naomba huu uzi usimame kama ulivyo, Huu ni Uzi wa Pongezi
naunga mkojo
 
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.



Hata mimi nilipenda sana alivyouliza na courage aliyokuwa nayo ya kuuliza kama alivyouliza. Hongera sana Mayalla, ubarikiwe sana. Ingawa hukupata jibu kwa swali lako, uliuliza swali ambalo ni la msingi sana.
 
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.



Tatizo tuna katiba ya chama kimoja tunayoitumia kwenye vyama vingi. CCM kwa ujumla hawajawahi kutaka vyama vingi walichoogopa ni kuwa sidelined na westerners kwaa jili ya misaada. Kwa viongozi wa kiafrika hulka za absolute power huwa ni za kawaida hivyo ni vigumu sana kwa an African sitting president kubadili katiba ya chama kimoja akiwa term yake ya kwanza kikwete alifanya alichofanya kwa kuwa alijua anondoka for good. Ila kwa jibu la Mh. Kwa Mayalla ni uvunjaji wa katiba wa moja kwa moja. Kinachonishangaza hili swali lilikuwa linatabirika kuwepo na alipaswa aande jibu diplomatic kidogo.
 
Back
Top Bottom