Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Nimefurahi kumuona Pasco, nimekuwa nikisoma sana makala zake hapa jamii forum
 
Umenena vyama. Waanzilishi wa hii dhana na separation of powers amina Jeremy Bentham walitamani iwe hivyo yaani kila muhimili uwe kivyake bila kuingiiliana lakini wakagundua kwamba hakuna separation of powers isiyo na kuingiliana ndio wakaja na kitu inaitwa checks and balances. Rais anaweza kusamehe na anaweza kubadili hukumu. Mkuu wa Dola anakuwa na upper hand dhidi ya wakuu wengine wa mihimili. Hutaki basi sikulazimishi ila unaona mwenyewe nani ni namba 1 wa nchi.

..hakuna mhimili wenye upper hand, uess mhimili mmojawapo umeamua kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba.

..huwezi kusema Raisi ni nambari 1 wakati anaweza kushtakiwa bungeni na kuondolewa madarakani.

..ningekuelewa, tena kwa kujilazimisha, kama ungesema bunge ni nambari 1. Kwasababu bunge likigoma kupitisha bajeti basi linaweza kupelekea kuitishwa kwa uchaguzi mkuu.

NB.

..Raisi anateua majaji lakini hana mamlaka ya kuwafuta kazi. Jaji anafutwa kazi baada ya kuchunguzwa na tume maalum.
 
Rais haapi utii kwa jaji bali anaapa utii kwa katiba.
Sasa sii angekaa nayo ofisini na kuiapia? Kwa hiyo hata wale wanaoapa mbele yake wanaapia utii kwa katiba hiyo hiyo ila tuu wanasimama mbele yake kama anavyo simama mbele ya Jaji mkuu?
Anyway, endelea kuamini kuwa Rais ndio mwisho wa mambo yote na hakuna kinacho mzuia kufanya chochote
 
Pasco katuwakilisha jf hapo ikulu vilivyo

OVA
 
Rais atakuwa kawaona v.i.l.a.za sana hawa waandishi wa habari yaaani maswali kama wanafanya kikao cha maandalizi ya harusi kweli safari kama taifa kila sekta bado sana, hawa CCM wana haki ya kututawala maana kama hawa ndio angalau tunaamini wanauelewa shangazi zetu, bibi, babu na vijana huko vijijini watakuwa na uelewa kweli wa kinachoendelea.
 
Rais atakuwa kawaona v.i.l.a.za sana hawa waandishi wa habari yaaani maswali kama wanafanya kikao cha maandalizi ya harusi kweli safari kama taifa kila sekta bado sana, hawa CCM wana haki ya kututawala maana kama hawa ndio angalau tunaamini wanauelewa shangazi zetu, bibi, babu na vijana huko vijijini watakuwa na uelewa kweli wa kinachoendelea.
 
Mayala alianza hotuba,kujifagilia na kutangaza kampuni yake na kujipigia debe la kutafuta fursa ikulu .Sehemu kubwa ya aliyonngea yalikuwa hasa ya kujinadi mnadani yeye binafsi.Kwangu naona kama aligeuza Ikulu na ile press conference kama gulio la kujinadi zaidi kuliko kuuliza swali.
So Far Maswali ya Pasco ndio yanabamba na kushika kila kona ya nchi kwa watu wenye kujielewa kuliko hata Tukio zima.
Maana nyingine Pasco ameonesha kuwa ana akili kuwazidi Wanahabari wote waliokuwa leo pale
 
Hongera Pasco kwa swali lako lililoibua rangi za rais wetu.
Kwamba kwa sababu serikali ndio inatafuta pesa basi yeye ndio yuko juu ya wote. Kama ni kwa dhana hii mkuu wa Tra ndio bosi japo hata hivyo hizo pesa hazitoki kwenye shamba lake bali kwa wananchi
 
Hata mi hapo nampa big up sana Pasco katendea haki uhuru wa kujieleza,safi sana!![emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Rais pia ni sehemu ya bunge...kwa katiba yetu Rais is top of everything isipokuwa katiba yenyewe ambayo ndiyo wananchi
 
.naomba nipatiwe mfano wa hata nchi moja inayoongozwa na mahakama au bunge
Nchi zote zenye demokrasia halisi, Bunge ndilo kila kitu. Bunge ndilo chombo halisi cha wananchi! Nafikiri umeona jinsi mabunge ya Marekani yanavyomwendesha Obama, pamoja na kwamba anaweza kutumia executive powers kuamua mambo mengine. Nchi kama Uswisi, bunge nalo ndiyo kila kitu, na ukizingatia nchi hiyo haina Rais kama Rais.
 
Mayala alianza hotuba,kujifagilia na kutangaza kampuni yake na kujipigia debe la kutafuta fursa ikulu .Sehemu kubwa ya aliyonngea yalikuwa hasa ya kujinadi mnadani yeye binafsi.Kwangu naona kama aligeuza Ikulu na ile press conference kama gulio la kujinadi zaidi kuliko kuuliza swali.
Mkuu Hebu zungumzia kidogo kuhusu maswali aliyouliza? Hayo ya kujinadi tumwachie Ngosha,maana amejinadi kuwa yeye ndiye super power! Katiba si kitu kwake! Kisa alipata nafasi ya kulihutubia bunge! Hogwash!
 
Ndio maana Mh Rais kamrejesha kwenda kuisoma katiba upya....mhimili iko sawa kwa juulakini kuna ambao umechimbiwa zaidi
Jibu swali ni wapi katika katiba ya JMT kuna zuio la kufanya mikutano. Acha bla bla. Sema ni wapi. Swali la separation of power limejibiwa tayati japo lina utata.
 
Kwa Mujib wa katiba au utashi wa akili ambayo ukishavuta bangi akili inakuwa si yako tena
duuh bangi tena?! hivi wakuu mambo mengine mnayotaka yafanyike mngekua viongozi mngeruhusu yafanyike bila mpangilio? katiba inaelekeza njia tuu,, maamuzi ya tunapitaje ni yetu
 
Hii ni kwa mjibu aa vigezo vyangu;
Wafuatao ndo wametumia vizuri nafasi ya kumwuliza rais maswali
1. Mayalla
2. Mwandishi wa BBC
3. Katibu wa MOAT
4. Tiddo Muhando
5. Muhariri wa Mwananchi (aliuliza swala za Zanzibar)
yule mzee wa MOAT kajibiwa mbovu sana.......mzee wa watu mpaka akawa anatetemeka
 
Back
Top Bottom