Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Ile dhana kuwa nchi inaendeshwa Na mihimili mitatu isiyoingiliana ni uongo tu.

Ukweli ni kwamba Bunge Na Mahakama ni taasisi kama zilivyotaasisi Zingine za Serikali.
 
paskali kauliza swali safi sana,na hii ndio umuhimu wa uandishi with specialisation/special knowledge,Pascal Mayalla . ni mwandishi mwanasheria,ndio maana hata jinsi alivyoliweka swali alikuwa anacheza nalo kama.anavyotaka.

waandishi wengi ni jack of all trades master of none

mmoja bwana manyerere yeye aliishia kuulizia whisky na matangazo ya magazeti

Hivi hivi ukipata mwandishi anamuhoji waziri wa fedha au gavana,awe na taaluma ya uchumi/fedha

mwandishi akimuhoji waziri.wa afya,awe na ABC za afya
 
Pasco kanifuraisha kwa swali lake la msingi na muhimu kwa siku ya Leo. Waandishi wengine wameuliza maswali mepesi mepesi tu, pia kuipasha JF wengi hupita JF na kuitokui acknowledge.
Mmoja sijui wa amelilia tunzo.....yaani tuna safari ndefu mno!
 
Hata fc Lumumba wanataka mikutano sema boss kabana kumbe
 
Ni kweli kauliza swali zuri lakini rais kamjibu kiutu uzima.rais anayo mamlaka yote dhamira ikiwa ni nzuri hata kama sheria haimpi mamlaka hayo tuache ushabiki wa kimachinga eti sheria na vitu vingine
Umejibu vizuri. Inafahamika kuwa kweli ni kwa nia njema, lakini swali lilkua ni "Where in the Constitution", na Siyo Why!
 
Simpendi!! Ila namkubali kama great thinker.
Big up Mayala a.k.a njaa kwa tafsiri ya aliyeshindwa kujibu swali lako"....mamlaka anayapa wapi,?"
 
Big up ndugu Pasco Mayalla kwa maswli mazuri pamoja Na Yule mwandishi wa BBC
 
Hakika mayalla alinifanya niwe na shauku ya kusubir majibu y kina toka kwa rais lkn daa majibu yale yalinifanya nizime na radio kabisa!!
 
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?

Unachokisema si kweli....rais hawezi kubugudhi mihimili mingine namna hiyo unayotaka kutuaminisha.

Kukitokea migongano rais hataweza tawala....mihimili mingine ikiamua ku-exercise their power against executive kwa pamoja nchi haitatawalika.

Executive kupeleka hela kwenye hii mihimili mingine sio eti ndio wana mamlaka zaidi ya hiyo mihimili,hii ni myopic view.

Kupeleka hela ni wajibu wa executive kwa hii mihimili,hakuna mambo ya kuomba...nani kakwambia ni hisani ya executive kupeleka hela judiciary na parliament?

Mnajua nyie mna matatizo...huwezi kuhemea mihimili mingine namna hii as if hii mihimili ni wake wako unaweza fanya utakacho...

Unaweza jenga ego na hasira kwenye hii mihimili mingine na hiyo ikulu ukaicha ukaenda Chato kulima...tatizo mnajifanya nyie executive ndio mna ego kubwa sana,mtasababisha friction na nyie ndio mtafeli..

Kwanini masiendeshe nchi kwa inclusion na power brokerage kila mtu akajiona anatakiwa kichangia na yupo included na anaheshimika?Nchi huwezi ijenga peke yako,huwezi,nguvu hizo hamnazo.Nchi ni watu kama wewe na wana uwezo kama wako au zaidi,treat people with respect and honest.Acheni kulewa madaraka mapema hivi.
 
Back
Top Bottom