Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Maana ya Mayala ni "njaa" kwa kisukuma,amesema Magufuli
Swali ZURI Majibu mepesi MNOOO. Eti Mayalla ni Njaa. Eti Mayalla Oyee! Hebu tuwe WAKWELI: Hili ndo jibu kwa swali lililoulizwa. Msingi wa jibu ni kuwa Mhimili mmoja UNATAFUTA hela na kuzigawa. Je, hii ndo sababu wa kuiingilia? Kwa maoni YANGU: Swali HALIKUJIBIWA!
 
Swala la kufuta mikutano ya vyama vya siasa limepotezewa, ila kama utafwatilia majibu ya mkuu utagundua kuwa since yeye ndiyo mtoa hela atataka kuona mihimili mingine inayojitegemea inafwata muhili anaousimamia yeye unachotaka
Tido Mhando na Ayoub Rioba walikaa kimya bila follow up

Nadhani walikusudia kumuokoa Rais maana hakuwa na jibu

Ayoub Rioba namwelewa maana mkate wake upo kwa Magufuli. Tido Mhando, nguli wa habari! simwelewi hata kidogo
 
Inavyooneka [HASHTAG]#Pasco[/HASHTAG] wa JF sio [HASHTAG]#Pascal[/HASHTAG] Mayalla wa JF, inaonyesha kabisa hawa ni member wawili tofauti...

Anyway, napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa kaka Pascal Mayalla, shikamoo kaka Pascal!

Ila jibu alilolipata sasa!! hiiiiii!!!
Kaaaazi kweli kweli!
Kwa hiyo kwasababu serikali ndio inatoa pesa basi rais anauwezo wa kwenda kinyume na katiba na kufanya analolitaka na maamuzi yoyote anayoyataka juu ya hiyo mihimili mingine?
Tuna kiongozi wa ajabu sana!!!!!!!!
 
Hawa ndiyo waandishi mahiri tunaowahitaji ktk taifa letu sio wale wa vibahasha.
 
Inawezekana kabisa kusifia bila kuponda upande mwingine...........hongera pascal nimefurahi kukuona live
 
Separation of powers haina ukuu

Hapa tukubaliane tu kuwa dhana nzima hakuielewa, hilo halina mjadala

Kwamba mhimili unaotoa pesa ndio superior! serious!
Ndio maana nasema anahitaji semina elekezi ajue mamlaka yake, mipaka na ukomo wake pamoja na anapaswa kufanya nini kama Rais na kusema nini. Ukweli hajui kabisa, ila kutokujua sio kosa kama atataka kujifunza
 
hivi Ruge nae alikuwemo? nimeskia anasifiwa tu na imoo yake.... nilitamani aulize swali la kiboyaboya
Hakwepo alitajaaa imooo na tarehe plus venue wakati akijibu swali la mwandish WA star tv aliuliza maadili na uvaaji fyyuuuuu huyu boya vitu vipo kibao anauliza uvaaji
 
Mkwepa maswali yetu kinehe. Akiulizwa hivi anajibu vile mi naona kama anatuchanganya tu.
 
Majibu ya Magufuli kwa Pasco yanadhihirisha kuwa TANZANIA haiendeshwi kwa katiba tena, Bali kwa mapenzi ya Bw. MAGUFULI, in the long run, this is very dangerous....! Maslahi ya taifa bila katiba ya Tanzania, sio maslahi ya taifa.
 
Kwa mara ya kwanza nampa hongera mayalla kwa kuitumia vizuri nafasi aliyo ipata leo.angalau ameonyesha ukomavu wa kiuandishi.
Potelea mbali majibu ya mwendokasi yaliyotolewa.

Eti kwa sababu tuu yeye ndo anaetoa mishahara basi yuko huru kufanya anachotaka.
 
Hata akiuliza hayana msaada wowote... Lazima mjue hivyo... Kwanza masilahi ya taifa mamlaka yakatiba baadae....
 
Huwezi akaanza kudai ulisi kutoka kwa baba yako wakati Hanna Mali... Pata Mali kwanza ulisi baadae...
 
Rais kasema hivi ''Katika mihimili mitatu upo mmoja uliozama zaidi'' Ukielewa hilo hoja zako zote hapo juu zinakosa mashiko
Ni kweli amesema hivyo yeye lakini ndivyo ilivyo kikatiba? Mbona katiba inaipa bunge nguvu ya kumwajibisha rais endapo atakiuka maadili au kuvunja katiba? Ndio maana Mzee Butiku alisema hatuhitaji rais TEMBO!
 
Ukawa Leo chali ndembe ndembe kifo cha mende!
 
ile press conference cjaona maana yake yani waandishi asilimia 99% wameuliza maswal mepesi na maswal magum yaliyoulizwa kama yale ya jamaa wa BBC na Pasco yamejibiwa kiujanjaujanja tu, mtu anatoa majibu ambayo yako out of the question, that conference was meaningless and a wastage of time.
 
Back
Top Bottom