Kumekuwa na dhana kuwa mtu pekee aliyeuliza swali la msingi kwa Mh. Rais ni Mayalla pekee. Ni kweli anastahili pongezi kwa swali lake bora kabisa.
Lakini pia kuna mtu mmoja aliuliza swali ambalo ukikaa na kufikiri zaidi ni suala ambalo ndilo lililo hot kwa sasa, na wapinzani pamoja na wanaharakati wamekuwa wakilipigia kelele. Swali liliulizwa na mwandishi wa BBC "SAMI AWAMI" Lilikuwa liki dai "INAONEKANA RAIS ANATUMIA KUKANDAMIZA DEMORASIA KWA EXCUSE YA MAENDELEO, HASA BAADA YA KUZUIA MIKUTANO YA WAZI YA VYAMA VYA SIASA"
Leo hii tumesahau na huku tulikolalamika kila kukicha kuwa rais anakandamiza uhuru na haki ya kufanya siasa, uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kutoa maoni.
Mimi kwa upande wangu nilimuelewa sana huyu mtu. Nadhani Pasco amekuwa popular kwa kuwa tu alijinasabisha kuwa ni member wa JF, ndio maana leo tumesahau watu wengine makini kama hawa kuwapa credit na kutoa airtime zaidi kujadili hoja zao.
Nawasilisha.