Habari za jioni wana JF wenzangu!
Naomba nichukue fursa hii adimu kujadili upande wa pili wa swali linaloonekana na baadhi ya watu kuwa NI swali bora kuliko maswali yote ya wahariri walipokutana na Mhe. Rais wa JMT Dr. Magufuli.
Kwanza naomba kusema kuwa halikuwa swali bora hata kidogo bali lilijaa mihemuko na wanaolishabikia wamejaa mihemuko. Sio analytical question hata kidogo kwa sababu zifuatazo:-
1. Halikuwa na background information ya nini kimefanyika ili uweze kukipinga vizuri
2. Halikuwa na any kind ya data kulipa backup ya mtu aliyeenda shule
3. Halikutoa madhara yoyote ya hatua za kubana safari za nje! Hivyo kukosa uhalali wa kuzitetea
4. Pascal Mayall ni kati ya watu waliomtukana Rais Kikwete kuwa ni VASCO DAGAMA kwa masafari lukuku
5. Ameshindwa kuelewa nafasi ya Mhe. Rais ktk mihimili mitatu
6. Ameonesha kuwa ni "MSEMAJI WA WAPIGA DILI"
Kwa muktadha huu, naomba sasa nije kwenye majibu ya Mhe. Rais
Rais ni kiongozi katika mihimili yote mitatu (BUNGE, MAHAKAMA, SERIKALI) kwasababu zifuatazo:-
- Kitendo cha kwenda kuhutubia Bunge na kutoa direction ya nchi
- Kitendo cha Mahakama kuomba pesa za kuendeshea kesi kinaonesha wanamtegemea kama kiongozi wao
- Yeye ni Pay Master General (PMG)
- Yeye ndie anayeteua majaji nk
Hivyo basi kitendo cha Paskali Mayalla kujinasifu kuwa ndie aliyeuliza swali bora kuliko wahariri wote ni dharau kubwa kwa waandishi wenzie wa habari.
Unafiki mkubwa wa huyu bwana unajitokeza anapowaambia wenzake hawakutakiwa kumuona kama Rais. Hivi huyu Paskali anapokaa na baba yake mzazi kuna saa anamuona kama house boy au shamba boy??????
Hivi angeuliza lile swali kwa tone ya kawaida angepungukiwa nini?? Kweni ukiongea kwa kufoka ndio vyombo vya habari vya nje vitakuona na kukupa kazi?? Huko nje wenzake wanaheshimu Ma Rais wao!!!
Huyu Ndugu ni wakupuuzaaaa!!! Jina lake ni Njaa na Njaa imepanda kichwani!! APUUZWEE NA KUSAMEHEWA!!!
Jioni Njema.
Mimi Ndugu yenu.
Queen Esther