Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

View attachment 429403
Kwanza kaanza kwa kuitaja JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.

Mkuu Chakaza, kwanza asante kwa kuniona hivyo, ila kiukweli, sii mimi pekee niliyeuliza maswali ya maana, kuna maswali mengi na ya maana zaidi hata ya swali langu kama lile la Zanzibar, lile la Katiba na lile la udikiteta, ila mimi nimepaishwa zaidi kwa sababu tuu niliitaja JF.

Kuna wengi wanasifu swali langu kwa sababu ni new generation hawakuwahi kukiona kipindi changu cha Kiti Moto, hivyo wala hawamjui Pasco Mayalla ni nani, ila wale wa zamani waliotazama Kiti Moto, maswali yale ni maswali ya kawaida kabisa kwenye Kiti Moto, tofauti ya Press Conference ya Rais na kipindi cha Kiti Moto, kwenye Press Conference, rais amepewa an easy ride na moderators, hivyo amejipatia mteremko, kwenye Kiti Moto rais angepewa hard time, hakuna mteremko, ni mlima tuu. Kuna watu walikuwa wakisikia wamealikwa Kiti Moto, walikuwa wanakimbia na wengine wanaomba Po! .

Kufuatia majibu ya juzi ya rais Magufuli yasiyokidhi, kiukweli kabisa kuna haja ya kuanzishwa kipindi kama Kiti Moto ili kuwafunza viongozi wetu namna ya kujibu maswali ya waandishi makini, sio kiongozi anaulizwa hivi, anajibu vile au hajibu kabisa lakini anaachwa.

Kwenye Kiti Moto, no stone is left unturned! .

Paskali.
 
Watu wangefahamu kwa nini baada ya kutoa hotuba bungeni hotuba ya Rais hujadiliwa halafu pia wangefahamu hakuna nchi yeyote duniani ambako mihimili mitatu inafanya kazi kwa nguvu sawa, hizo ni siasa za kitoto sana! Spika anapigiwa kampeni ya siku mbili, jaji mkuu anateuliwa na rais, kampeni ya urais miezi kadhaa, kinachoamuliwa na bunge mpaka kipitishwe na rais halafu eti unasema separation of power! Kama kusoma hujui hata kuangalia picha nako hujui?

Kwa wanaojua Paskali ameambiwa ki utu uzima kuwa wewe hujui, hizo theory ulizo nazo hazifanyi kazi katika dunia halisi. Hizo ni theory za ideal world, theory za darasani za kujibia mtihani tena katika level ya chini kabisa ya kumbukumbu wala haijafikia hata level ya application. Naungana na Chakaza kusema pamoja na class situation aliyoitumia Paskali angalau yeye aliuliza swali kwani anafahamu hata swali ni kitu gani. Wengine kweli wanastahili wafanyiwe ithibati
 
Kwaiyo Katiba yetu niyamaigizo tu maana inasema ivyo
 
Kwaiyo Katiba yetu niyamaigizo tu maana inasema ivyo

Kwenye Katiba humo humo ndiko kumpako Rais nguvu. Watu watulie wasome waone. Karibu vipengele vyote vinasema bila kuathiri sharia zilizopo, wanachokifanya ni kutunga sheria tu. Ukitoka katika katia inabidi urudi kujua sheria inasemaje kuhusu suala husika
 
The Government of the United Republic and its authority Act No.15 of 1984
34.-(1) There shall be a Government of the United Republic which shall have authority over all Union Matters in the United Republic and over all other matters concerning Mainland Tanzania. (2) The authority of the Government of the United Republic shall relate to the implementation and upholding of this Constitution and also to all other matters over which Parliament has power to legislate. Art.9 (3) All the authority of the Government of the United Republic over all Union Matters in the United Republic and also over all other matters concerning Mainland Tanzania shall vest in the President of the United Republic. (4) Subject to the other provisions of this Constitution, the authority of the Government of the United Republic shall be exercised by either the President himself or by delegation of such authority to other persons holding office in the service of the United Republic. (5) It is hereby declared that the provisions of this Article shall not be construed as - (a) transferring to the President any powers which by the law have been conferred to another person or authority other than the President; or (b) preventing Parliament from conferring power upon any person or authority other than the President.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na mamlaka yake Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara. (2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
28
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. (5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayatahesabiwa kwamba- (a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au mamlaka yoyote ambayo si Rais; au (b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka yoyote ambayo si Rais.
Utekelezaji
 
SURA YA TATU BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO SEHEMU YA KWANZA BUNGE
Bunge Sheria ya 1984 Na.15 ib.12
62.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. (2) Bunge litakuwa na wajumbe wa aina zote zilizotajwa katika ibara ya 66 ya Katiba hii ambao wote wataitwa Wabunge. (3) Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na sehemu zote mbili za Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katika hii au masharti ya sheria nyingine yoyote, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vile vile na Rais, kwa mujibu wa madaraka yao kuhusu jambo hilo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
49
Madaraka ya Bunge Sheria ya 1984 Na.15 ib.12
Sheria ya 1992 Na.4 ib.17 Sheria ya 1992 Na.20 ib.11
63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo. (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
 
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO
108.-(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu") ambayo mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote. (2) Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazi kwamba shauri la aina iliyotajwa mahususi litasikilizwa kwanza katika Mahakama ya ngazi iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basi Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri la aina hiyo. Hali kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kutekeleza shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila za kisheria zinazotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwa kawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu. Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila ya kuathiri mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.
Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao Sheria ya 1979 Na.14 ib.6 1985 Sheria ya 1985 Na.15 ib.22 Sheria ya 1990 Na.14 ib.5
109.-(1) Kutakuwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu (ambaye katika ibara zifuatzo kwenye Katiba Hii atatajwa tu kwa kifupi kama "Jaji Kiongozi") na Majaji wengine wa Mahakama Kuu wasiopungua kumi na watano. (2) Jaji Kiongozi na Majaji wengineo wa Mahakama Kuu watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama.
 
Mipaka kwa haki na uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ib.6
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma. (2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya-
(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi; (b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
24
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya umma; (c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai au la jinai; (d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama; (e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji, uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya watu binafsi nchini; au (f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla. (3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu. (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka sheria kwa ajili ya- (a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii; (b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;
(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
25
(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika, kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.
 
Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine Sheria ya 1984 Na.14 ib.6

20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-

(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano;

(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:

(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;

(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano;

(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.

(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.

(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
 
Watu waache kukubali kudanganywa kwa sababu ya uvivu wao wa kusoma hivyo kungoja kuambiwa na watu utadhani hao wengine wameumbwa ili waje wasome kisha wafikiri kwa niaba yao
 
Mkuu Chakaza, kwanza asante kwa kuniona hivyo, ila kiukweli, sii mimi pekee niliyeuliza maswali ya maana, kuna maswali mengi na ya maana zaidi hata ya swali langu kama lile la Zanzibar, lile la Katiba na lile la udikiteta, ila mimi nimepaishwa zaidi kwa sababu tuu niliitaja JF.

Kuna wengi wanasifu swali langu kwa sababu ni new generation hawakuwahi kukiona kipindi changu cha Kiti Moto, hivyo wala hawamjui Pasco Mayalla ni nani, ila wale wa zamani waliotazama Kiti Moto, maswali yale ni maswali ya kawaida kabisa kwenye Kiti Moto, tofauti ya Press Conference ya Rais na kipindi cha Kiti Moto, kwenye Press Conference, rais amepewa an easy ride na moderators, hivyo amejipatia mteremko, kwenye Kiti Moto rais angepewa hard time, hakuna mteremko, ni mlima tuu. Kuna watu walikuwa wakisikia wamealikwa Kiti Moto, walikuwa wanakimbia na wengine wanaomba Po! .

Kufuatia majibu ya juzi ya rais Magufuli yasiyokidhi, kiukweli kabisa kuna haja ya kuanzishwa kipindi kama Kiti Moto ili kuwafunza viongozi wetu namna ya kujibu maswali ya waandishi makini, sio kiongozi anaulizwa hivi, anajibu vile au hajibu kabisa lakini anaachwa.

Kwenye Kiti Moto, no stone is left unturned! .

Paskali.
Paskali, nikiri kuwa nilikuwa mfuatiliaji mkubwa wa kipindi chako cha Kiti moto na kweli kilikuwa kitimoto kweli. Na ni kweli kuwa pamoja na baadhi ya wengine waliuliza maswali yenye maana siku ile.
Ila usidhani kuwa kwa kuitaja JF ndio ulipopata credit, la hasha bali ni style ya uulizaji swali ambayo ilikupa authority kubwa mpaka ukawa uko juu ya muulizwaji ambaye ni Rais. Uliuliza kwa mamlaka makubwa kama Mwajiri wake Rais na hilo ndilo lililonipa hamasa ya kuanzisha uzi huu ulioungwa mkono na wengi.
Ile ndiyo namna ya kumhoji Rais ambaye ni Amiri jeshi mkuu huku ukimuonyesha kuwa wewe Raia wa kawaida unayo haki ya kutaka majibu sahihi toka kwake kwani wewe ndiye uliyemuweka kazini. "Umepata wapi mamlaka ya kufanya hivi na vile nje ya Katiba uliyo apa hadharani?" Hilo ni bonge la swali na authoritative kabisa. Maswali yale ya wengine hata kama yalikuwa ya maana lakini yalikuwa kama yakubembeleza hisani yake kujibu.
Nakubaliana na wazo lako la kufufua kipindi kama kile cha Kitimoto hasa kwa wakati huu tulionao, tengeneza waandishi jasiri wa kukusaidia na media huru ya kutangazia kipindi chako na utaona kitakavyo pata umaarufu sio TZ tuu bali East Africa nzima.
Note;
Nilifurahishwa sana na kauli ile ya kutaka kuwepo katika ziara za nje na kuwa sio lazima kulipiwa na serikali uwezo wa kujilipia upo. Ni kauli makini sana ya kuonyesha hakuna njaa (hata kama alisema una njaa) na kuwa haujikombi kwa kufuata maslahi ya serikali bali unahitaji furusa ya kufanya kazi.
 
Mipaka kwa haki na uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ib.6
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii
25
(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika, kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.
Mkuu Domokaya, kwanza asante kutuletea vifungu vya katiba. Tanzania ni nchi ya kidekrasia inayofuata katiba na sheria. Katiba ndio sheria mama, hakuna mtu yoyote aliye Juu ya katiba, hata rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania yuko chini ya katiba, kila kitu rais anachokifanya, anafanya kwa majibu wa katiba ambayo kuna vifungu maalum vinavyompa rais mamlaka ya kufanya maamuzi yoyote. Kwa vile Katiba ndio imetoa haki ya kufanya mikutano, rais ametumia mamlaka gani kutoa amri inayokwenda kinyume cha Katiba? .

Hapa ndipo dhana ya udikiteta ilipoibukia. Chadema walipotaka kuandamana kwenye maandamano ya UKUTA, niliwabeza kuwa udikiteta wa rais Magufuli ni jambo la kisheria na sio jambo la kisiasa, hivyo uvunjifu wa katiba, hauwezi kupingwa kwa maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima bali hupingwa kwa kufile petition Mahakama Kuu .

Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA: Nimehamasika, Nitashiriki, Tujitokeze kwa Wingi! Ila...!

Paskali.
 
Maana ya Mayala ni "njaa" kwa kisukuma,amesema Magufuli
Mkuu Yohana Mbatizaji, ni kweli Mayalla kwa Kisukuma ni Njaa ila sio njaa ya tumbo ya kukosa chakula ambayo tiba yake ni shibe, bali ni baa la njaa lilosababishwa na ukame, yaani Mayalla is not hunger caused by lack of food, but famine caused by climate change.

Rais aliposema njaa, watu wanafsiri mimi ni mtu wa njaa njaa, hivyo naendekeza njaa, nikishibishwa, natulia. Kiukweli Wasukuma sio miongoni mwa makabila ya njaa njaa, Wasukuma ni mutu ya shibe, hawaendekezi njaa njaa, Wasukuma ni matajiri sana wa roho japo ni masikini wa moyo, yaani ni masikini jeuri, sio watu wa kujipendekeza au kujikombakomba kwa yoyote kwa sababu yoyote.

Nimethirika sana kisailolojia kwa kauli ile ya rais hivyo nafanya mawasiliano na wanasheria nguli kuangalia uwezekano wa kumfungulia kesi ya madai, kwa sababu ile kinga ya rais kutoshitakiwa mahakamani inahusu utekelezaji wa majukumu yake Kitaifa, kukosea tafsiri ya ukame na njaa kumepelekea kina ninapo pita mitaani nataniwa Pasco Njaa!, japo wengine hunikaribisha chakula.

Paskali
 
Kwanza hakujibu swali na pia sikupenda alipoamua kukukejeli kuhusu jina lako na kicheko chake kilichofuata cha kinafiki.

Nilipenda body language yako baada ya mkuu kukuita NJAA...inaakisi hiki ulichoandika.
 
Back
Top Bottom