Hongera Sana TCU kwa Kuanzisha mfumo wa Paper writing

Hongera Sana TCU kwa Kuanzisha mfumo wa Paper writing

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Huyu Prof aliyegundua mfumo wa Paper writing kwa hawa post graduate alifanya Jambo moja zuri na msaada sana kwenye kuwajengea uwezo wasomi wetu wa kulinganisha hoja (speech with references)

Huwa naumia sana ninapoona Hawa wasomi wa miaka ya nyuma kidogo wanapoita press harafu wanakuwa hawana hoja linganifu ili kutetea kile wanacho kizungumza Kwasababu kuwa msomi tu ww tayari ni public figure kila mtu anataka kupata Elimu kupitia ww. Mtu anafarijika anaposkia kwa mfano huu ugonjwa ulio nao alishauguaga mtu fulani alipona mpaka Sasa ni mzima, nk.

NB; wasomi nyie ni nguzo muhimu kwa Taifa letu mkiamua kuita press Basi muwe mmejipanga mmeshafanya mini research syo mnakuja na hoja za upande mmoja. HESHIMA KWENU WASOMI.
 
Saivi huwezi kugraduate postgraduate degree kama huja-publish papers.
Sidhani kama wametafakari vya kutosha, vyuo vina option ya ku-award postgraduate degree based on dissertation/thesis submitted, kuna baadhi ya vyuo ambavyo vinataka uambatanishe publications zako ndani ya thesis, lakini bado vinakubali unpublished thesis.

Swala la publication ni motivation ya mtu husika, huwezi kulazimisha kila mtu a publish maana wakati mwingine kuna gharama zinatakiwa na ni swala linalohitaji muda.

Ni uonevu kumkwamisha mtu kuwa awarded wakati ameshakamilisha thesis.......awe awarded publication libaki kuwa swala lake binafsi kuamua ndani ya ratiba zake mwenyewe.​
 
Kuna Masters za aina mbili ndugu mtoa mada.

Masters by Thesis na Masters by dissertation.

Kwa ninavyojua Masters yenye ulazima wa ku publish ni masters by thesis kwasababu mtu haingii darasani kwahiyo ndo mana ameongezewa challenge ya ku publish paper ili a graduate pamoja na ku submit dissertation.

Masters by dissertation haina ulazima wa ku publish paper kwa sababu mtu anakaa darasani karibu mwaka mzima kwahiyo mda wa kuandika paper hautokuwepo
 
Sidhani kama wametafakari vya kutosha, vyuo vina option ya ku-award postgraduate degree based on dissertation/thesis submitted, kuna baadhi ya vyuo ambavyo vinataka uambatanishe publications zako ndani ya thesis, lakini bado vinakubali unpublished thesis.

Swala la publication ni motivation ya mtu husika, huwezi kulazimisha kila mtu a publish maana wakati mwingine kuna gharama zinatakiwa na ni swala linalohitaji muda.

Ni uonevu kumkwamisha mtu kuwa awarded wakati ameshakamilisha thesis.......awe awarded publication libaki kuwa swala lake binafsi kuamua ndani ya ratiba zake mwenyewe.​
Kupublish huwa inachukua muda mrefu kidogo kwahyo vyuo huwa wanahitaji mwanafunz atume paper yake kwenye journal husika then wale watampa acceptence letter ya kuipokea hyo paper, then atatakiwa kuiunganisha kwenye dissertation yake pamoja na paper yake. Ndpo atagraduate Sasa...gharama Ni kuanzia usd 55 - 150 hv
Zote hizo lazima upublish paper
 
Kuna dili litaibuka la journals uchwara ili papers uchwara ziwe published. Mi nafkiri wangewaacha wale wale wa PhD tu. Kuishusha hiyo publication ba level ya masters ni Tena by dissertation ni kujaza mambo mengi yatakayoleta longolongo nyingi ingawa yatamfanya mtu kuwa fit professionally na academically.
Pia, hili liendane na uboreshaji wa vitu kadhaa ili liendane na muda. Publication takes time.
 
Shaka ondoa kuna matumizi ya AI siku izi. Unachotakiwa kuwa nacho ni bando tu 😂😂😂
 
Back
Top Bottom