Nimefuatilia sana mdahalo wa wagombea wa Urais wa Tanganyika Law Society (TLS). Kati ya wagombea wa kiti hicho ninachukua nafasi hii kumpongeza Wakili msomi Mwabukusi kutokana na maswali aliyoulizwa kwa kujibu maswali yote kwa ufasaha. Naona upepo umebadilika licha ya kupigwa vita Wakili Mwabukusi. Wanachama wa TLS huu ndiyo wakati wa kutoa uamuzi wa kumchagua mtu ambaye ana msimamo na haogopi.