Hongera TRA kwa kuita watu interview,ila zipo changamoto za kutatua

Hongera TRA kwa kuita watu interview,ila zipo changamoto za kutatua

KUNGUNIMSOMI

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Posts
203
Reaction score
235
Tukiwa wahanga wa mda mrefu wa sahili za TRA ,na wengi kufanikiwa kupata nyakati za utumishi ila kwa kipindi ambacho wanasimamia TRA wenyewe, changamoto zilikuwa nyingi sana,nadhani kwa kipindi iki wanaenda kutatua ,tunaimani nao sana.

Baadhi ya changamoto zinazopaswa kutatuliwa ni:

1.Vimemo:
Swala la vimemo ni ugonjwa mkubwa,kwa sasa TRA wakitaka kuwa wasafi waachane na vimemo.

2.Kuzingatia muda: Ni vyema TRA Kuzingatia muda wa kuanza usahili mfano, mwaka jana mtihani wa asubuhi umekuja kufanyika jioni.

3.Wasimamizi wenye weledi: Kuna baadhi ya wasimamizi wa usahili wanakuwa na ndugu na marafiki,kipindi mitihani inaanza wanajadiliana na watu hao.

4.Kuepuka kuvujisha mitihani:Ushauri TRA watumie njia zote kuhakikisha mitiani haivuji.

5.Watu wasio na sifa ila wameitwa kwenye interview ni vyema wataarifiwe mapema sio mtu anafika kwenye interview ndio anazuiliwa kuingia mfano,kuna mwaka watu wa banking and finance walizuiliwa kuingia kwenye usahili wa taxation.

6.Ulinzi uimalishwe: Kuna wasailiwa wengine wanaenda kuiba mikoba ya watu Mfano kuna mwaka TRA waliweka askari unaulizwa utaje kitu kilichopo kwenye mkoba wako ndio unachukua(iyo ilikuwa safi)

7.Matokeo yatumwe kwenye website kwa uwazi :kama walivyo tuma majina ya usahili,na sio kutuma majina kwenye email,kutuma majina ya waliofaulu kwenye email hii inaleta ukakasi.

Nawatakia maandalizi mema

Updates
Usahili uliofanyika leo ,kwa upande wa mikoani kulikuwa na usimamizi mzuri.

Ila kwa Dar ni mvurugano,kwenye kuchukua mabegi na vyeti wakati wa kutoka watu wamekanyagana , na pia wasimamizi nguvu ni chache walichoka mapema ata kukagua.

Mitihani ya kesho ongezeni usimamizi mzuri kama wa utumishi.Na nilishatoa ushauri mapema.
 
Samahani ndugu hivi ukiwa na photocopy ya cheti original kimepotea hauruhusiwi kufanya usahili
Sidhani kama watakubali, kama huna barua kutoka necta na loss ripoti.

Ila jaribu kuwapigia simu TRA mapema kabla ya mtihani wao watakupa jibu kamili .

Ila kwa sasa kuna utaribu wa kupata vyeti necta .

Vya secondary nenda NECTA watakupa utaratibu au tembelea kwanza website yao kuna masharti wameainisha ili kupata cheti mbadala ,Kama umemaliza chini ya 2008 hawatoi vyeti mbadala.

Ila lazima uwe na loss report
 
Asante kwa maoni.

Nakuhakikishia kwamba yote tutayafanyia kazi kika
Msisahau kuwapa Kipaumbele waliosota mtaani miaka 10 baada ya kuhitimu chuo. Hapa ni ikiwa watafanya Vizuri Usaili. Wamesota hadi kuuza chips na mahindi ya kuchoma mtaani.
 
Msisahau kuwapa Kipaumbele waliosota mtaani miaka 10 baada ya kuhitimu chuo. Hapa ni ikiwa watafanya Vizuri Usaili. Wamesota hadi kuuza chips na mahindi ya kuchoma mtaani.
Wakifanya vizuri hao wanaenda peponi moja kwa moja
 
Amesema cheti chake kimepotea. Akija na Affidavit, Loss report na Copy ya cheti hawezi kusaidika kijana amesota sana mtaan aisee.
Msaidieni huyu kijana, anauliza mtu mwenye majina yafuatayo
1. Kasukali Mtani Jembe
Na
2. Kasukali M Jembe

Ana haja ya kuwa na affidavit ili kuonesha ni mtu mmoja?
 
Back
Top Bottom