Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Habari,
Wakuu kama tunafatilia habari na mitandao tunatambua wiki hii nchini wetu imetawaliwa na matukio mengi. Miongoni mwa tukio lililogusa vituo vya habari ni pamoja na Mgombo wa wafanya biashara wa Kariakoo.
Imekuwa sio kawaida kwa viongozi wetu kujitokeza kusikiliza migogoro ya Wananchi na kero za Wananchi. Nampongeza Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa kujitokeza mbele na kusikiliza madukuduku ya Wananchi kiuwazi.
Pamoja na kumpongeza kujitokeza kusikiliza bado nahimiza kwamba asibaki kusikiliza kero tu ili kutuliza upepo bali iwe ni sehemu ya mchakato wa kutafuta suluhu ya kero hizi.
Zaidi ya hayo pia zipo kero nyingi na sehemu tofauti tofauti zinawakabili Watanzania ni vyema viongozi wetu wasiishie Kariakoo peke yake na pia wasisubiri mgomo na maandamano.
Tanzania bora ya kesho inawezekana.