Hongera Waziri Ummy Mwalimu kwa mkakati mpya wa kupambana na COVID19


Kuna mikakati ya mazishi lakini hakuna ya kuzuia maambukizi?

Tunataka mikakati ya kuzuia maambukizi haya mengine ni kelele tu.
 
Wakuu naona wengi tuna criticize badala ya kutoa maoni nini kifanyike. Imefika hatua tunashutumiana, kukashifiana na kutoka nje ya mada.

Nilitegemea tusisitize upatikanaji wa vifaa kinga na tiba (tunaambiwa hakuna tiba lakini watu wanapona). Mfano, kupata vipimo sahihi ni muhimu sana kwa sasa. Hivyo kila hospitali ya mkoa iwe na huduma hiyo.

Kuwa na mashine za kusaidia kupumua za kutosha ingawa hata wenzetu walioendelea hiyo ni changamoto, kujenga wodi za dharura hata kwenye viwanja vya michezo, tumeona vilabu Fulani huko Uingereza wamejitolea viwanja vyao vitumike ktk kutoa huduma. Tunao wataalam wa majengo ya dharura au hata jeshi linaweza kutumika. Tuache siasa.
 
Nchi hii imejaa wajinga watupu kuanzia juu mpaka chini .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afya kama sekta kuna madaktari, manesi na wengine. Mna vyama vikiwamo vya madaktari (MAT), manesi nk.

Hivi kweli mmesalimisha utaalamu wenu kwa wanasiasa. Mkafumbwa midomo mkafumbika na kuwa watazamaji tu wa ugonjwa huu hadi kufikia hali ilivyo sasa?

Sekta hii imekumbwa na nini?

Kwanini mmeshindwa kuwa wazi cha nini kifanyike hali utaalamu mnao?

Ndugu zetu mnatuangusha.
 
Jitihada nzuri hadi hapo, naomba tusiwe watu wakupinga na kubeza kila kitu. Hii ni hatua muhimu sana na kipekee nimpongeze Waziri wa afya kwa kushirikisha wataalam na kuomba ushauri wa nini kifanyike kwa wakati huu.

Hapo kwenye namba sita inahitaji elimu ya kutosha, kuna watu wenye dalili ndogondogo wananchi waelimishwe namna ya kuishi na hawa watu majumbani bila kueneza maambukizi zaidi ikiwa mazingira yanaruhusu.

Tuonyeshe u great thinker wetu kwenye kutoa mapendekezo na ushauri ya nini kifanyike.
 
Habari za chini nilizopata 3dys ago kuwa wahudumu kama 80 wameugua rona...! Na serikali haitak kukiri!...hatarious..
 
Ubarikiwe mkuu kwa ushauri, wewe ni muungwana sana. Ni muhimu kushirikiana kipindi hiki, umetoa maoni mazuri sana
 
Kwenye UKIMWI mliambiwa muavoid unsafe sex, blood transmission nk..

Covid 19 tumeambiwa tukae ndani kama hakuna ulazima wa kukutoa nje ukishindwa mkuu kasema tujifukize
 
Ni kweli maana ukiangalia hosp kwenyewe hapatoshi, nadhani jamii inaweza kuelemishwa
 
Good!
 
Tupunguze kulalamika..Hii ni vita ya Mtu moja moja..
Hata tuandike magazeti Hapa JF haibadilishi kiti,
cha msingi nunua satinaiza(Sanitaizer), Barakoa wagawie wasio Nazo,
usichoke kutoa elimu ya kujikinga.
 
Loud and clear
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Uko sahihi mkuu, huu ni wakati wa kuweka mbali siasa kwa sasa.

Kwa hali ilivyo sasa hivi, hospitali zote kama sio nyingi kwa sasa wahudumu wote kuanzia mapokezi wapatiwe vifaa vya kujikinga kwa sababu, mgonjwa atakuja kutaka huduma na hajui hali yake ya maambukizi ya Corona na akishaingia hospital hadi kujua ikiwa anaweza kuwa na maambukizi/ dalili tayari wahudumu wa awali tayari watakua wameshaambukizwa.

Kuna haja ya kuanzisha kituo chenye wataalam wakawa wanatoa ushauri iwe kwa simu au mitandao kwa wenye kujisikia dalili za maambukizi. Wakapatiwa ushauri na nini cha kufanya au wapi pa kwenda kupata huduma stahiki.
 
Hivi mtu kama huna cha kuandika si unakaa kimya tu kwani lazima wote tuanzishe siredi

Sent using Jamii Forums mobile app
Khantwe omba msamaha haraka sana kabla sijaweka mambo yako wazi
Niombe msamaha kwa kosa gani? Weka hayo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨
πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
 
Mkuu mass testing linaweza kuwa suluhisho ili mgonjwa akienda hosp ajulikane status yake. Otherwise wauguzi na ma dakitari wakiathirika wote ina maana wataeneza ugonjwa kwa kila anayetembelea hosp na aliyeko hosp.

Serikali ianze mkakati wa kununua vifaa toka kwa wajasiriamali USA, maana kuna zaidi ya 200 approved test kit.
 
Kaja inbox kuomba msamaha
 


Uwezo huo tunao? Na Je, tumeshatengeneza mazingira ya namna ya kukabiliana na hao watakaokua wanagundulika wana maambukizi?
Kwa sasa tu karanteen na self isolation zinatushinda kwa kuwa watu ni wengi.

Mimi sio mtaalam wa afya ila naamini mass testing ikifanyika watakaokua hawana huo ugonjwa ni wachache sana ni vile sio kila mtu daliki ziko wazi na wengine haiwapi homa wala mafua ila wanaambukiza wengine.

Mbaya zaidi uchukuaji wa sample nao hauko rafiki sana, mtu kujitolea inahitaji moyo.

Lakini penye nia pana njia, wataalam wanaweza kuja na njia mbadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…