Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyongeza ni kuhusu upatikana wa vifaa vya kupimia, senegal ni Waafrika wenzetu kama hicho kifaa chao kweli kinafanyakazi MSD wanunue kwa wingi na viuzwe Pharmacy pamoja na maelekezo ya namna ya kujipima. Sharti liwe kujipima hapo hapo Pharmacy na kuanzishiwa dawa kama una maambukizi badala ya kusubiri mpaka mtu aanze kukohoa ndio aanze kupimwaKipengele namba 6 ushauri wangu self isolation ikiambatana na "prescribed medicine" ni nzuri zaidi kuliko kuwaweka watu ambao hawako serious wodini na kutowapa huduma yoyote. Ni vizuri sasa wataalamu wa afya ambay hawajaajiriwa wakapewa mafunzo ili wawe washauri wa watu wanajitibia nyumbani hasa kuhusu dawa za kutumia na unywaji wa maji na vitamins
Mimi nimepata kitu, kumbe kuna watumishi wa afya wameambukizwa siye tulifichwa tukaambiwa hali ni shwari.Hivi mtu kama huna cha kuandika si unakaa kimya tu kwani lazima wote tuanzishe siredi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mudawote hivi kwa nini huwa mnamhusisha yeyote ambaye hawaungi mkono au mpinzani wa CCM kuwa ni CDM? I have said it time and again, kuwa sina unasaba na CDM. Naunga mkono juhudi zao za kuondoa uonevu wa awamu ya tano, basi! Kupotea watu, kuuawa, kupigwa risasi, kubambikiwa kesi etc! Labda kwa faida yako, nilianza maisha na Tanu Youth League...... and have traversed all the way through Nyerere to this regime!Mkuu independent outlook ya kumkopesha Mh Mbowe 800milion? Pole sana
Kisha wewe jamaa ni muondo na mshenz.Great Thinkers, ujumbe unaofuata unaonesha jinsi wizara ya afya ilivyojipanga kukabiliana na COVID19, kikao alichofanya na chama cha Madakitari (chini ya rais wao Dr Osati) kinatoa matumaini mapya kwa watanzania.
Mrejesho wa kikao cha wanataaluma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Habari za leo
Jana tarehe 27 Aprili, 2020; vyama vya kitaaluma vya afya nchini kikiwemo MAT tulikutana na timu ya Wizara ya Afya kujadiliana kuhusu mwenendo wa wa COVID-19 nchini. Kikao hiki ni matokeo ya mkutano wa vyama vyote wa tarehe 26 Aprili, 2020 kilichofanyika kupitia "zoom ". Tulijadili yafuatayo.
1. Upatikanaji wa PPEs Wizara
Mheshimiwa. Waziri Ummy Ally Mwalimu alisema tayari wameagiza mzigo wa PPEs unaotosheleza matumizi ya mwezi mzima; mzigo huo unategemewa kufika wakati wowote wiki hii. Pia wizara imepata fedha kiasi cha shilingi za kitanzania 9.6Billioni walioielekeza MSD kwa ajili ya kuagiza mzigo mwingine wa PPEs.
2. Wagonjwa kukataliwa kwenye hospitali mbalimbali
CMO na RMOs wameagizwa kushughulikia swala hili mara moja. Hii itaambatana na kuangalia upya mwongozo wa utumiaji wa PPEs bila wafanyakazi kuambukizwa. Sambamba na hilo watumishi wamehimizwa kufuata mwongozo wa IPC ili kuepuka maambukizi na hivyo wasiwakatae wagonjwa wanaopewa rufaa au kuja kwenye vituo vyao.
Kikao pia kiliridhia kwamba mafunzo ya IPC lazima yaendelee kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya. Pamoja na hayo tulikubaliana kuwa isolation centers ziongezeke hata kwenye hospitali za binafsi (private hospitals); kwa kuanzia hospitali hizi kupitia kwa Association of Private Health Facilities in Tanzania (APHFTA) wamekubaliana kutenga isolation za level 3 (level1, 2 and 3) katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam na baadae mikoani, kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa.
3. Ucheleweshwaji wa majibu ya COVID-19
Wizara imekubali kuongeza vituo vitatu kati ya tisa zenye uwezo wa kupima COVID-19. Kuanzia Jumanne ya wiki ijayo ya tarehe tarehe 5 May, 2020; maabara ya NIMR Dodoma itaanza kutoa majibu, ikifuatiwa na Mwanza na Mbeya. Changamoto imekuwa ni uwepo wa wataalam wanane tu wa maabara wanaoweza kuchakata majibu ya COVID-19. Kwa hiyo Mafunzo kwa wataalam wengine yameanza na watasambazwa kwenye vituo husika.
4. Mazishi ya waliofariki
Ikitokea mgonjwa amefariki kwenye hospitali, ndugu inabidi wahusishwe iwezekanavyo chini ya uangalizi wa wataalam wa afya kutoka manispaa husika kuhusu mazishi na eneo la kuzikia. Mganga mkuu wa wilaya (DMO) husika ataarifiwe kwa msaada zaidi ikiwa ni pamoja na magari na utaratibu wa mazishi bila kupoteza muda zaidi.
5. Contact tracing
Kwa upande wa Dar es Salaam ambapo tayari kuna maambukizi mengi kwenye jamii ni changamoto kuendelea na kuwatafuata "contacts" na pia ni vigumu kuwa weka wote ‘’isolation’’. Wizara walishauri kwa hatua tuliyo nayo sasa kwa mkoa wa Dar es Salaam kama mtu anahisi kuwa na dalili za COVID-19 aende kwenye kituo husika kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo, na kurudi nyumbani huku wakiendelea kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa Barakoa na kujitenga na wengine. Mikoa mwingine ambayo ugonjwa haujasambaa sana waendelee na utaratibu wa "contact tracing".
6. Kuweka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolations
Kuhusu hili tulijadiliana na hatukufikia muafaka. Mheshimiwa Waziri akaomba wanataaluma tujadiliane halafu tumshauri kwenye hili. Maswali yakiwa; Je ni sahihi kuwa weka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolation ambazo tayari zimejaa au tuwape ushauri halafu wajitenge nyumbani mpaka Ikitokea wana dalili za hatari?. Hii itabidi tuitolee maoni sisi kama wanataaluma
7. Upungufu wa Damu salama kipindi hiki
kumeonekana kuna upungufu mkubwa sana wa damu salama katika benki za damu hasa kwa Dar es Salaam. Wito umetolewa kwa hospitali zote kupunguza kufanya/kutoa huduma ya upasuaji usio wa dharura ili kupunguza matumizi ya damu.
8. Utafiti kwenye eneo la COVID-19
Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) tayari inaendelea na tafiti tatu juu ya COVID-19 na pia imetoa mwongozo wa utafiti kwa wakati huu wa COVID-19. Utafiti pia unahusisha dawa za miti Shamba (tiba mbadala) ikiwa ni pamoja na kujifukiza.
9. Ufafanuzi ya juu ya kauli ya waziri kuwa hakuna watumishi walioambukizwa
Mheshimiwa Waziri alisema alichomaanisha ni kuwa hakuna mtumishi anayehudumia wagonjwa kwenye isolations aliyeambukizwa. Kwa sababu labda walipewa Mafunzo zaidi ya namna ya kujikinga. Alisema anajua kuwa kuna watumishi wameambukizwa wakiwa EMD/Mapokezi na OPDs (idara ya magonjwa ya nje). Kwahiyo ameomba Mafunzo zaidi yaelekezwa kwa watumishi wote.
NB: Tunaomba maoni yenu juu ya kipengela Namba 6 hapo juu.
Nawasilisha
Dr Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Ukionywa onyeka mkuu wangu Retired , usishupaze shingo. Hata Snowden yupo uhamishoni Russia, China wao wananyonga ukiwa msaliti wa maendeleo ya nchi.Mudawote hivi kwa nini huwa mnamhusisha yeyote ambaye hawaungi mkono au mpinzani wa CCM kuwa ni CDM? I have said it time and again, kuwa sina unasaba na CDM. Naunga mkono juhudi zao za kuondoa uonevu wa awamu ya tano, basi! Kupotea watu, kuuawa, kupigwa risasi, kubambikiwa kesi etc! Labda kwa faida yako, nilianza maisha na Tanu Youth League...... and have traversed all the way through Nyerere to this regime!
Sasa unaanza vitisho! Unanionya kwa kosa lipi? Sana sana ni kufa tu, basi! Hilo sina hofu nalo kama alivyosema Lwaitama kuwa mnanisogeza kaburini!Ukionywa onyeka mkuu wangu Retired , usishupaze shingo. Hata Snowden yupo uhamishoni Russia, China wao wananyonga ukiwa msaliti wa maendeleo ya nchi.
China si wauaji na wanaongoza kwa kukiuka haki za binadamu! duniani! Nimesaliti wapi?wananyonga ukiwa msaliti wa maendeleo ya nchi.
Wangapi akina nani?Ndugu zako au family yako wamepimwa?Unataka kujua takwimu kutoka kwa akina nani?Tunataka kujua watu wangapi wamepimwa wangapi wanaugua, wangapi wako karantini na wangapi wamepoteza maisha.
Hii ndio akili ya watu tuliowapa madaraka watuongeze!. ShameWangapi akina nani?Ndugu zako au family yako wamepimwa?Unataka kujua takwimu kutoka kwa akina nani?
Senti bai yuzingi tecno T301
Wangapi akina nani?Ndugu zako au family yako wamepimwa?Unataka kujua takwimu kutoka kwa akina nani?
Senti bai yuzingi tecno T301
Mbona flyovers mnacopy, ni kitu gani Tz hatucopy mpaka ukomunisti tumekopi.Ndukidi hayo mambo ya kupanikishana tuachane nayo, tuweke mikakati ya mass testing ila hakuna mambo ya kutoa taarifa, kwa sababu hatuna briefing ya HIV au Kisukari so why iwe COVID19???? Kwanini tukopy kila kitu?
Je kuna umuhimu wa kutaja maambukizi ya malaria? Cancer??? Au kuna umuhimu wa kutaja vifo vya malaria??? Nadhani mikakati ya kujikinga ni bora zaidi. Tuungane kumpongeza Waziri Ummy kwa hatua aliyochukua
Kuhusu nini kifanyike tulisema zamani sana tukapuuzwa, au hukuwa umejiunga JF?Wakuu naona wengi tuna criticize badala ya kutoa maoni nini kifanyike. Imefika hatua tunashutumiana, kukashifiana na kutoka nje ya mada.
Nilitegemea tusisitize upatikanaji wa vifaa kinga na tiba (tunaambiwa hakuna tiba lakini watu wanapona). Mfano, kupata vipimo sahihi ni muhimu sana kwa sasa. Hivyo kila hospitali ya mkoa iwe na huduma hiyo.
Kuwa na mashine za kusaidia kupumua za kutosha ingawa hata wenzetu walioendelea hiyo ni changamoto, kujenga wodi za dharura hata kwenye viwanja vya michezo, tumeona vilabu Fulani huko Uingereza wamejitolea viwanja vyao vitumike ktk kutoa huduma. Tunao wataalam wa majengo ya dharura au hata jeshi linaweza kutumika. Tuache siasa.
Ushauri ulishatolewa ila haukufuatwa, sasa unataka ushauri gani tenaJitihada nzuri hadi hapo, naomba tusiwe watu wakupinga na kubeza kila kitu. Hii ni hatua muhimu sana na kipekee nimpongeze Waziri wa afya kwa kushirikisha wataalam na kuomba ushauri wa nini kifanyike kwa wakati huu.
Hapo kwenye namba sita inahitaji elimu ya kutosha, kuna watu wenye dalili ndogondogo wananchi waelimishwe namna ya kuishi na hawa watu majumbani bila kueneza maambukizi zaidi ikiwa mazingira yanaruhusu.
Tuonyeshe u great thinker wetu kwenye kutoa mapendekezo na ushauri ya nini kifanyike.
Data mtazitoa tu, subiri donors wawakalie kooni, au umesahau ya watoto wa kike na ujauzito shuleniData si mnazo na mnazitoa kila mara mitandaoni ?,au mnataka kulingania ?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo ishatokea hata tukilaumu haitusaidii kitu.Bado mpo kwenye mikakati. Kumbe uwezo wetu wa kukabiliana na huu ugonjwa ni mdogo. Kwanini hamukuchukua hatua kali za kuudhibiti tangu mwanzo?.
Ushauri ulishatolewa ila haukufuatwa, sasa unataka ushauri gani tena
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhusu nini kifanyike tulisema zamani sana tukapuuzwa, au hukuwa umejiunga JF?
Sent using Jamii Forums mobile app