Tumpe maua mengi sana Eng Hersi kwa kuinyoosha simba kwa kuipiga wiki na kuwafunga midomo, kutupa raha wanayanga na kubeba ubingwa zote. Hakika kwasasa Africa nzima hakuna Rais bora wa timu kama Hersi. Rais bora anaekaa jukwaani hata mechi ikachezwe Malinyi huko. Hii huwapa moyo sana wachezaji, mashabiki na benchi la ufundi.
Tuseme kwa sauti ndogo sana tunapomkosoa Hersi ili asivunjike moyo kwa kazi kubwa mno ya kuipambania Yanga ambayo kwa nguvu na akili za Eng Hersi sasa hivi Yanga iko level za kina Real Madrid, Bayern na Al Nasr ambao tutaomba nao mechi tuone kama Mbappe au Ronaldo atafunga mbele ya Baka huku tukiwapa makolo baraka zote za kwenda kucheza ndondo cup aina ya shirikisho mwakani na nina uhakika my wetu au Yanga B hatoboi hata makundi.
Kitu kidogo nili note pale Amaan , Eng Hersi alizungumza sana na kuwashukuru wadhamini, wachezaji na benchi la ufundi, ila alipitiwa kabisa kuwapa maua mashabiki waliofunga safari toka kila mahali kwenda Zenji kuishabikia Yanga yao.
Pale Eng Hersi alichemka kibinadamu kutokana na kuzidiwa na furaha ya kombe tulilopata kwa jasho na damu maana mechi ilikuwa tough sana. Tukumbuke yule kocha mshamba alisema mashabiki wa uto tunashangilia kama manyani akidhani katutukana kumbe alitupa sifa kubwa maana ushangiliaji huo huo ndio unajaza makombe kabatini na kuwapa mzuka wachezaji wanaothibitisha kwa kuandika wenyewe kama Aziz Ki, usajili bora kabisa wa Eng Hersi.