Hasira za watu ziko hapa:-
1. Chama chenu kimetawala kutoka uhuru. Hivi mnaposema mmefanya maendeleo mnalinganisha na nani au chama kipi? Ninyi ni mapimbi lazima uwe na variable utonyeshe ni kwa ulinganifu upi utaonyesha kuwa kuna juhudi. Kinachowasaidia ni ajira za waliofeli kuingia idara ya polisi na hivyo amri yoyote inakuwa halali maana hawawezi kutafsiri.
2 Miaka mitano hakuna ajira wala kupanda mishahara. Lakini mnahitaji huduma bora, mnajisifu kwa kujenga hospitali nyingi na vituo vya afya. Ni ujinga kuweka miundombinu bila kuangalia wataalamu wa kufanya hiyo mapango yes ni mapango sababu ni makazi ya popo bila kuwa na wataalamu wa kundesha shughuli stahiki kwenye majengo hayo na mengi yao maana yamejengwa kifisadi yanahitaji ukarabati kabla hata ya kuanza kazi.
3. CCM hakuna demokrasia. Wajumbe walikuwa 164 (Tanganyika ni 129 na Zanzibar 35), kura zimepigwa matokeo ni kama ifuatavyo Hussein 129 (Tanganyika), Nahodha 16 na Khalid 19 = 35 hizo za Zanzibar. Kifupi Mwinyi amechaguliwa na Watanganyika sio Zanzibar. Atakataliwa mtatumia polisi kuleta vurugu kwa wazanzibar kama kawaida yenu miaka yote.
4. Unafiki mkubwa ni upigaji wa kura jana. Mnajua mwenyekiti wenu hakubaliki maana anawaburuza wanachama, akawamrisha mpige kura za wazi watu wakajengewa hofu ya kumkataa.
5. Wana CCM og hawana nafasi mbele ya wahamiaji. Hii ni hatari na ni nzuri kwa vyama mbadala hasa CHADEMA ambao wataona hakuna chaguo lingine zaidi ya kuungana na wananchi wazalendo wenye moyo safi kuikataa ccm na matendo yake yote hatimae tupate ukombozi.
Nitaungana na wazalendo wowote ambao by any means wapo tayari kwa hari na mali kuiondoa ccm madarakani.