Hongereni JWTZ na Watanzania kwa kuwa na 'Ndege Vita' nzuri zilizokuwa 'zinazurula' tu Anga la Tanzania leo Mchana

Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.
 
Safi sana Mkuu...sasa unadhani ( mnadhani ) GENTAMYCINE nisingeanzisha Uzi wangu huu huku nikitumia Mbinu ya 'Kukandia' ili mkasirike ( mhamanike ) na mje na hizi Intellectual Facts zenu na 'Madini' sisi tungejuaje Umuhimu na Uimara wa hizo ( hizi ) Ndege na kuwa nazo pia?
 
Watu wameona chopa za Airbus 225 lakini wanajifanya wanataka kuona vipya zaidi.mnataka maadui watupime kirahisi tu.mfumo wetu ni kulinda na sio kutoka kwenda kushanbulia ,sisi ni kama urusi.tunangoja adui afike mipakani .
Mbowe mnayemsingizia Gaidi nae alifika huko Mipakani?
 
Hii mada kama una akili utaelewa kama jinga utaelewa na ujinga wako,

Nchi ya mama wapiga dili kibao
Huwa napenda sana kukutana na Watu 'very smart' kama Wewe hapa JamiiForums na ambao huwa mnanielewa upesi GENTAMYCINE na yale ambayo huwa nayalenga kama siyo kuyakusudia.
 
Most of them are out of service!
Tundege twa 1960s lazima tulete shida kwenye service. Kampuni mtengenezaji unakuta ashaachana na hizo outdated types bali wamebaki wamiliki wanaojiweza kidogo kiteknolojia ndio wanaweza toa spare parts na maintenance. Ni kama North Korea na India
 
Matumizi mabaya ya Kodi zetu,ukiimarisha demokrasia na ujirani mwema uhitaji kupoteza kodi kugharamia jeshi.
Yafaa nini mtu hadi anastaafu ajawahipiga hata risasi
Seriously?
 
Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.
Nimelazimika kumtaja mkuu. Serikali yake ndio iliagiza zile jets kutoka China
 
Jeshi ni lazima liwepo,Ili mtawala aking'ang'ania madaraka limfurushe,bila mabeo bashiru angekuwa raisi.
Kazi ya jeshi sio kufukuza viongozi. Ukiona nchi bado inategemea jeshi ndio lifukuze kiongozi ujue hiyo bado ni ya ovyo. Katiba inaelekeza serikali zote za duniani ziondolewe na bunge au mahakama. Sijawahi sikia katiba inayoelekeza jeshi liondoe serikali
 
Sera zao za nje ni kulinda maslai yao nje ya mipaka.
Sisi masikini unalinda nn.
Maslahi ni nini?
Sisi maslahi yetu ni kulinda rasilimali za majini kama bahari ya Hindi hivyo lazima tuwe na Navy yenye silaha kama boats na warships. Hizo zitasaidia kuzuia maharamia, wavuvi haramu na kulinda miundombinu ya mafuta na gesi kwenye vitaru.

Maslahi ya ardhini ni kulinda mipaka isivamiwe na waasi wa nchi nyingine kumbuka eneo la maziwa makuu halijatulia. Endapo wakipata safe heaven kwetu maana yake silaha zitazagaa mitaani na majambazi yataongezeka. Tunajilinda dhidi ya kina Amboni na kina Kibiti, jumlisha na wale wa Kusini kutoka Cabo Delgado. Tuna migodi ya madini, hujui pale DRC kuna wahuni wanabeba madini bure na sio Wakongo. Tunalazimika kuwa na vifaru, APCs, IFVs, etc.

Angani tunatakiwa kuhakikisha usalama wa vyombo vyetu vya usafiri na kuzuia mashambulizi endapo adui akiamua. Tunalazimika kununua radar, air defence system, anti aircraft missiles, etc. Utaletaje watalii sehemu hakuna usalama? Hebu ngoja niishie hapa....

Lengo kuu la jeshi la nchi yoyote ile ni kuzuia vita, sio kuanzisha vita. Marekani ina doomsday submarines za Ohio Class a.k.a Boomers. Makamanda wake huwa wanaziogopa wanasema MAFANIKIO YAO NI KUTOZITUMIA HIZO BOOMERS. Yani US ilitumia gharama kubwa kutengeneza hizo Ohio subs ili mtu akitaka kuishambulia US kwa makombora ya nyuklia basi aache maana kuna retaliation strike atapata. US ina silaha ambayo kazi yake ni kutotumika. Strange!

Sasa basically jeshi linatakiwa kuogopesha adui, sio kumshawishi. Ukifuta JWTZ utashangaa Burundi inasema Kigoma ni yao. Ukikosa jeshi adui anajilazimisha, ukiwa nalo unaogopwa kiunafiki
 
Genta kichwa wa SAUT banaaa kuna mtu ameniambia unashindaga sana pale makumbusho bar ya "Simba kapakatwa" na huachi kuvaa jezi yako ya Simba SC.....
 
Upo sahihi kabisa sikatai ila nje na ndege vita huwa na machaguo ya kujikita ipasavyo kulingana na mazingira yanayokuzunguka inawezekana ukawekeza zaidi katika Air defense systems ambazo ni za kileo zaidi kwasababu ndege vita nyingi operational cost yake ni kubwa hasa kwa ndege vita zinazotoka ulaya na amerika tofauti na za kichina au Urusi nje tu na kununua.

Sitakwenda deep Sana ila naimani umenielewa vizuri kuna muda kinachozingatiwa hasa ni nani anakuzunguka na ana nini Cha zaidi na unaweza kumkabili vipi.
 
Ni wazi hatujafika level ya juu ya sophistication kuendana na mahitaji ya vita za leo, lakini juhudi zenye muendelezo zinafanyika kila uchwao.

Benchmark ya utayari wa kivita na zana za kijeshi wa Jwtz huwezi kuuweka kwenye mizania moja na US Army. Kuendana na mazingira yetu, tupo better off kuliko majirani zetu. Ingawa mengi inabidi yafanyike.

Nakubaliana na wewe kwenye Navy, kulingana na ukubwa wa pwani yetu, more is to be done.
 
Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.

Kikwete kwenye muhula wake wa mwisho alimteua afande Shimbo kama balozi kule CHINA na ndio wakati huo alipopiga dili la ndege hizi za kivita toka China!! Shimbo na Kikwete wana historia ya muda mrefur tangu Kikwete alivyofukuzwa Monduli na Afande Sayore kwa kuleta fitina jeshini!!
 
Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.
Nyerere hakukosea kusema bwana yule ni mtoto hafai kuwa rais. Nyerere aliongelea utoto wa fikra, maono, upeo, uwezo, uthubutu na sifa nyingine nyingi ambazo Mkwere hakuwa nazo.

Jamaa aliharibu sana nchi. Yeye na kundi la marafiki zake wachache wakajihodhisha uchumi wote wa Taifa.
 
Kama kiongozi haishemu katiba na jeshi la police kaliweka kwapani, huku akimaliza wananchi, inatakiwa aondolewe kwa mtutu,Ili kuepuka machafuko jeshi huwa linaingia kumfurusha mbwa kichaa asimalize kuku.
Jeshi ni mali ya wananchi sababu linamfumo huru unaojitegemea, police na vyombo vingine ni mali binafsi ya mtawala uvitumia atakavyo,tuliona bashite aliambiwa utoto wake akafanyie vyombo vingine thus ukumuona akidrive jeshi kama alivyodrive police, kwenye ishu ya vyeti baba yake aliambiwa jeshi sio vyeti thus ishu ya vyeti jeshini hakuthubutu kuonea.
Jeshi ulinda watawaliwa dhidi ya mtawala,, police ulinda chama na mtawala dhidi ya watawaliwa.
 
Kuna Mtu umemtaja hapa inasemekana kwa tabia yake ya 'Madili' baada ya kuona kashtukiwa akaamua atengeneze yale Mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto ili kupoteza Ushahidi na kweli alifanikiwa.
 
Hapo endeleeni tu mkuu. Huko mko nje ya ufahamu wangu.
 
kwa bongo issue sio hizo ndege uzionazo, issue iko kwenye mikataba iliyotumika kuzinunua na hao wazabuni....dah na CAG ndio hafikagi kule...
Hii nchi kaka imeshaharibika. Ata marehemu sikuona kama alikuwa na uzalendo kama anavyosifiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…