GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #61
Rwanda tuna zaidi yenu na hatushoboki.Ndege vita za tanzania we nyarwanda zinakutesea nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rwanda tuna zaidi yenu na hatushoboki.Ndege vita za tanzania we nyarwanda zinakutesea nini?
Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.Kuna ndege mpya JWTZ imepatiwa? Sitaki kuamini kama uchumi wetu unaruhusu. Namlaumu Kikwete kuagiza Chengdu J-7G miaka ya kuanzia 2012 wakati ni ndege very outdated kwa sasa. Hizo Mig 21 tulitumia kipindi cha vita ya Iddi Amin hadi leo zipo sijui hata status yake kama ni functional na serviceability status
Safi sana Mkuu...sasa unadhani ( mnadhani ) GENTAMYCINE nisingeanzisha Uzi wangu huu huku nikitumia Mbinu ya 'Kukandia' ili mkasirike ( mhamanike ) na mje na hizi Intellectual Facts zenu na 'Madini' sisi tungejuaje Umuhimu na Uimara wa hizo ( hizi ) Ndege na kuwa nazo pia?Watanzania muache upumbavu saa nyingine. Jeshi linajengwa wakati wa amani, huwezi vamiwa leo eti ndio ukanunue ndege muda huo. Hizo ndege ukitoa order leo unaanza kupokea mara nyingi baada ya miaka miwili. Ukilazimisha upewe mapema wanakuuzia kwa bei kubwa sana, ukilazimisha upewe muda huo huo vita ikiwa imeanza itabidi ukodishe au upewe kutoka kwenye jeshi la nchi nyingine. Natoa mfano, Saddam Hussein miaka ya 1980s alipotaka kushambulia meli za mafuta za Iran kwenye Tanker War alikuwa hana ndege mahususi kwa ajili ya mashambulizi ya baharini wakati Iran alikuwa nazo. Ilibidi Saddam akodishe kwa gharama kubwa ndege za jeshi la Ufaransa wakati akisubiria order ya ndege alizonunua kwa kampuni ya Dassault.
South Korea miaka ya zamani ilikuwa inaamini kwenye kujenga uchumi sijui viwanda kama mnavyobwabwaja hapa na wakati huo North Korea iko inalamba umasikini. N. Korea ikajenga jeshi kubwa, mazoezi na silaha za kutosha kisha ghafla ikavamia South Korea. Hao na uchumi wao mkubwa walipigwa ndani ya wiki mbili wakasogezwa karibu na mji mkuu, Marekani ikatoa wanajeshi wote Japan ikasaidie ila nao hawakutosha. Ikabidi Marekani iagize wengine zaidi ya 1,700,000 na mpaka vita inaisha wanajeshi zaidi ya 36,000 wa USA walifariki. Kuanzia muda huo ungerudia kuwaambia South Korea wasikazane na jeshi wangekuzaba vibao. Leo hii kila mwanaume lazima aishiriki 'JKT' yao.
Hata Switzerland na historia yake ndefu haijawahi ingia vitani ila ina silaha pamoja na kuwa imezungukwa na allies. DRC hii hapa inapigwa na ka Rwanda. CAR hiyo hapo eti waasi wa Anti Baraka na wa Sereka walilishinda jeshi la serikali. Mi nilikuwa nashangaa inakuaje waasi waliovaa kandambili na jezi za Arsenal wanalishinda jeshi na wakati hawapambani na serikali, kuja kugundua maskini jeshi la serikali halina silaha hata buti na wanavaa sare tofauti yani ukienda Kariakoo ukakutana na bakabaka lolote ukalangua unavaa unaenda gwaride.
Muamar Gaddafi hakuanza kiherehere cha kupigana ovyo kwetu alipomsaidia Iddi Amin. Alishaanza mapigano na Misri na Chad. Chad ilikuwa maskini na hata leo ila ilikuwa na jeshi la kujitetea kama sisi. Gaddafi aliivamia ila Chad wakapambana na silaha zao hafifu kwenye kile kinachoitwa TOYOTA WARS, ndio chimbuko lake huko.
Yani historia zote na uzoefu wote unaonesha ni muhimu kuwa na jeshi imara, jeshi kufanya mazoezi, kuwa na silaha. Hivi vitatu vitategemeana na situation tofauti na geopolitics hivyo ulinzi usiharibu sekta nyingine. Misri inalazimika iwe imara kuliko Tanzania. Mnataka msiwe na silaha nyie mmekuwa Vatican?
Mbowe mnayemsingizia Gaidi nae alifika huko Mipakani?Watu wameona chopa za Airbus 225 lakini wanajifanya wanataka kuona vipya zaidi.mnataka maadui watupime kirahisi tu.mfumo wetu ni kulinda na sio kutoka kwenda kushanbulia ,sisi ni kama urusi.tunangoja adui afike mipakani .
Huwa napenda sana kukutana na Watu 'very smart' kama Wewe hapa JamiiForums na ambao huwa mnanielewa upesi GENTAMYCINE na yale ambayo huwa nayalenga kama siyo kuyakusudia.Hii mada kama una akili utaelewa kama jinga utaelewa na ujinga wako,
Nchi ya mama wapiga dili kibao
Tundege twa 1960s lazima tulete shida kwenye service. Kampuni mtengenezaji unakuta ashaachana na hizo outdated types bali wamebaki wamiliki wanaojiweza kidogo kiteknolojia ndio wanaweza toa spare parts na maintenance. Ni kama North Korea na IndiaMost of them are out of service!
Seriously?Matumizi mabaya ya Kodi zetu,ukiimarisha demokrasia na ujirani mwema uhitaji kupoteza kodi kugharamia jeshi.
Yafaa nini mtu hadi anastaafu ajawahipiga hata risasi
Nimelazimika kumtaja mkuu. Serikali yake ndio iliagiza zile jets kutoka ChinaUkimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.
Kazi ya jeshi sio kufukuza viongozi. Ukiona nchi bado inategemea jeshi ndio lifukuze kiongozi ujue hiyo bado ni ya ovyo. Katiba inaelekeza serikali zote za duniani ziondolewe na bunge au mahakama. Sijawahi sikia katiba inayoelekeza jeshi liondoe serikaliJeshi ni lazima liwepo,Ili mtawala aking'ang'ania madaraka limfurushe,bila mabeo bashiru angekuwa raisi.
Maslahi ni nini?Sera zao za nje ni kulinda maslai yao nje ya mipaka.
Sisi masikini unalinda nn.
Nyie hamna kitu tunauwezo wa kuwapiga ndani ya masaa 2.nyie hamna kitu.Rwanda tuna zaidi yenu na hatushoboki.
Upo sahihi kabisa sikatai ila nje na ndege vita huwa na machaguo ya kujikita ipasavyo kulingana na mazingira yanayokuzunguka inawezekana ukawekeza zaidi katika Air defense systems ambazo ni za kileo zaidi kwasababu ndege vita nyingi operational cost yake ni kubwa hasa kwa ndege vita zinazotoka ulaya na amerika tofauti na za kichina au Urusi nje tu na kununua.Jpm alijitahidi sana kulifanya jeshi kuwa la kisasa, amenunua "vitu" vingi vya kisasa!
Shenyang F-7 ( J -7) zimekuwa old fashioned kulingana na ujuzi wa kisasa, Mikoyan (MiG old model) pia zinahitaji replacement n
Kwa kufanya new acquisition of different variants.
Hongera wanajeshi wetu, mnawajibika ipasavyo!
Ni wazi hatujafika level ya juu ya sophistication kuendana na mahitaji ya vita za leo, lakini juhudi zenye muendelezo zinafanyika kila uchwao.Maslahi ni nini?
Sisi maslahi yetu ni kulinda rasilimali za majini kama bahari ya Hindi hivyo lazima tuwe na Navy yenye silaha kama boats na warships. Hizo zitasaidia kuzuia maharamia, wavuvi haramu na kulinda miundombinu ya mafuta na gesi kwenye vitaru.
Maslahi ya ardhini ni kulinda mipaka isivamiwe na waasi wa nchi nyingine kumbuka eneo la maziwa makuu halijatulia. Endapo wakipata safe heaven kwetu maana yake silaha zitazagaa mitaani na majambazi yataongezeka. Tunajilinda dhidi ya kina Amboni na kina Kibiti, jumlisha na wale wa Kusini kutoka Cabo Delgado. Tuna migodi ya madini, hujui pale DRC kuna wahuni wanabeba madini bure na sio Wakongo. Tunalazimika kuwa na vifafu, APCs, IFVs, etc.
Angani tunatakiwa kuhakikisha usalama wa vyombo vyetu vya usafiri na kuzuia mashambulizi endapo adui akiamua. Tunalazimika kununua radar, air defence system, anti aircraft missiles, etc. Utaletaje watalii sehemu hakuna usalama? Hebu ngoja niishie hapa....
Lengo kuu la jeshi la nchi yoyote ile ni kuzuia vita, sio kuanzisha vita. Marekani ina doomsday submarines za Ohio Class a.k.a Boomers. Makamanda wake huwa wanaziogopa wanasema MAFANIKIO YAO NI KUTOZITUMIA HIZO BOOMERS. Yani US ilitumia gharama kubwa kutengeneza hizo Ohio subs ili mtu akitaka kuishambulia US kwa makombora ya nyuklia basi aache maana kuna retaliation strike atapata. US ina silaha ambayo kazi yake ni kutotumika. Strange!
Sasa basically jeshi linatakiwa kuogopesha adui, sio kumshawishi. Ukifuta JWTZ utashangaa Burundi inasema Kigoma ni yao. Ukikosa jeshi adui anajilazimisha, ukiwa nalo unaogopwa kiunafiki
Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.
Nyerere hakukosea kusema bwana yule ni mtoto hafai kuwa rais. Nyerere aliongelea utoto wa fikra, maono, upeo, uwezo, uthubutu na sifa nyingine nyingi ambazo Mkwere hakuwa nazo.Ukimtaja Kikwete huna nachukia mno Mkuu kwani hakuna Rais ambaye Tanzania imekuwa na bahati mbaya kuwa nae kama Yeye na huwa nawashangaa sana Watanzania wengi ( siyo Wote ) wakiwa wanamsifu na wanampenda.
Kama kiongozi haishemu katiba na jeshi la police kaliweka kwapani, huku akimaliza wananchi, inatakiwa aondolewe kwa mtutu,Ili kuepuka machafuko jeshi huwa linaingia kumfurusha mbwa kichaa asimalize kuku.Kazi ya jeshi sio kufukuza viongozi. Ukiona nchi bado inategemea jeshi ndio lifukuze kiongozi ujue hiyo bado ni ya ovyo. Katiba inaelekeza serikali zote za duniani ziondolewe na bunge au mahakama. Sijawahi sikia katiba inayoelekeza jeshi liondoe serikali
Kuna Mtu umemtaja hapa inasemekana kwa tabia yake ya 'Madili' baada ya kuona kashtukiwa akaamua atengeneze yale Mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto ili kupoteza Ushahidi na kweli alifanikiwa.Kikwete kwenye muhula wake wa mwisho alimteua afande Shimbo kama balozi kule CHINA na ndio wakati huo alipopiga dili la ndege hizi za kivita toka China!! Shimbo na Kikwete wana historia ya muda mrefur tangu Kikwete alivyofukuzwa Monduli na Afande Sayore kwa kuleta fitina jeshini!!
Hapo endeleeni tu mkuu. Huko mko nje ya ufahamu wangu.Kwahiyo kuweka wazi hapa JamiiForums kuwa nimemaliza SAUT mwaka 2009 na Kuishi Hostels za Darfur ndiyo unajifanya unanijua sana Pimbi Wewe? Aliyekuambia au Kukudanganya kuwa nawe sikujui au sijakujua nani? Nakujua kuwa upo JWTZ na ulipigiwa pande na Baba yako ambaye sasa ana Ushawishi mkubwa ndani ya Chama baada ya Kustaafu Jeshini.
Sasa kama unajifanya kunijua mno mbona husemi kuwa mwaka huo huo ( 2009 ) tukiwa Darasa la M9 tunafanya Mtihani wa Somo la Uchumi la Mwalimu ( Mhadhiri ) Luzangi.
Ambapo GENTAMYCINE niliweka Rekodi ya Kuufanya na Kuumaliza ndani ya dakika 50 tu wakati ulikuwa ni wa Masaa ( Saa ) Tatu na matokeo yalupotoka nikapata ( nikaufalu ) kwa kupata A ya distinction kabisa?
Cc: Amari
Hii nchi kaka imeshaharibika. Ata marehemu sikuona kama alikuwa na uzalendo kama anavyosifiwa.kwa bongo issue sio hizo ndege uzionazo, issue iko kwenye mikataba iliyotumika kuzinunua na hao wazabuni....dah na CAG ndio hafikagi kule...