Hongereni 'Mortuary Attendant' wa Tanzania, ila usiombe Nduguyo afie India halafu uje uipokee Maiti yake waliyoiandaa Wao huko

Hongereni 'Mortuary Attendant' wa Tanzania, ila usiombe Nduguyo afie India halafu uje uipokee Maiti yake waliyoiandaa Wao huko

[emoji1787] mtani bana.

Niliwahi sikia miaka mingi iliyopita kuwa mtu akifia India huo mwili unateswa sana yaani unakunjwa and sometimes mifupa wanaivunja ili uingia kwenye kibox cha mizigo.

Niliwahi pokea mwili wa mtu mmoja maarufu miaka hiyo mkoa fulani alifia India. Walipoupokea mwili airport moja kwa moja kuelekea mkoani,

Niliogopa nilipoona kile kisanduku, kuuliza nikaambiwa its economic.

Kweli mwenye mgonjwa ukiona hali inazidi kuwa mbaya ni vema umrejeshe tu nyumbani.
Thamani yako kwao ni ukiwa hai, maana unawapa hela.. Ukishakufa huna faida wala thamani tena kwao
 
vipi kutibiwa huko treatment inakuaje au ndio kukatana vidole na kuingiziana vidole matakoni
 
miezi ilyopita nilifiwa na bibi kwa kuwa mtoto wa kiume nilipeka mpaka mwochwari mda ulikuwa usiku.
Aisee nyie acheni kule .hawa watu wanavumilia mengi yani nilivoingiza kwenye friji,maiti zilizopo pembeni za kila aina na harufu fulani ambayo naikuta sana mabuchani mpaka nilishindwa kula nyama.
 
[emoji2][emoji2][emoji2] Kumbe mnachagua uzi wa kuomba picha,, mwambieni mwamba atume tu picha maana kuna wadau watasem bila picha uzi ni batili
Tunaogopa maiti zenu!,[emoji1787][emoji1787]
 
Hili la Kumpunguza Viungo vyake vya ndani kwa Maiti yoyote ile inayosafirishwa kutoka nchi za mbali ni la Kawaida kwani vikiachwa Maiti itanuka vibaya kwakuwa hivyo Viungo huoza kwa haraka sana.

Concern yangu ni Mwili kuandaliwa kwa Kulipua lipua, Kutokuujali na kuupa tu treatment ya kutimiza wajibu kiasi kwamba inaibua Hisia kuwa huenda Wahindi wanatudharau sana Sisi Waafrika.

Nimesikitika mno.
Mimi nimekuelelwa bwana Mino
 
Maelezo marefu kiini cha ulalamishi hakuna wejamaa vipi? Dish liko upande upi? Ili turekebishe.
 
Kuna Maiti nimetoka kuipokea na kwenda Kuihifadhi Hospitali fulani Jijini Dar es Salaam ila baada ya Kuifungua ili ianze kuwa treated ikitokea nchini India alikofia kiukweli nimeamini Waafrika tunadharaulika mno na hawa Wahindi siyo Watu japo hapa Tanzania tunawapenda na hata Kuwanyenyekea vile vile.

Huko nyuma pia niliwahi kubahatika katika Kushughulikiwa Mwili ( Maiti ) iliyokuwa ikiandaliwa ( treated ) tayari kusafirishwa kwenda nchi fulani na kiukweli Mortuary Attendant wa Tanzania ( katika Hospitali husika ) waliuandaa Mwili vizuri kabisa, Kiutaalam, Kiupendo na Kiutu kabisa na naamini hata Walioupokea huko ulikoenda walishukuru na kuridhika nao.

Mwili ( Maiti ) niliyoipokea leo kutoka nchini India ( nilikoamini kuwa kuna Watu makini na Weledi ) baada ya kufika na kuikagua tayari kwa Kuiandaa kwa Kuagwa Kesho imenifanya niamini kuwa kumbe Waafrika ( hasa Watanzania ) ambao ni Mortuary Attendant wana Utu, Hekima na Ustaarabu sana katika Kuandaa Miili ya Marehemu Wetu lakini imenifanya nianze Kuwachukia Wahindi na kuamini kuwa kumbe ni Watu wenye Roho Mbaya na hawana Ubinadamu.

Ushauri wangu ( na silazimishi ) kama utakuwa na Ndugu yako nje ya nchi hasa nchini India kama mkiona dalili za Kupona hazipo tafadhali upesi sana mrudisheni tu Tanzania aje afie huku ili apate treatment nzuti ya Mortuary Attendant wa Kitanzania ila mkiacha wafie nje ( hasa huko India ) wakija huku katika Jeneza ( ambalo hugeuka kuwa Cargo ) tegemeeni kukutana na Makwazo na Uchungu mkubwa pale mkiupokea.

R.I.P Marehemu wote nchini Tanzania.
Pole sana popoma
 
Umeandika nini sijui unajua wewe mwenyewe.
 
Mkuu niko hapa kwa andishi hilo
 
Back
Top Bottom