Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini

US au Marekani lazima mwanafunzi aliyehitimu degree ya sheria, akitaka kuwa wakili lazima atafute leseni.

Na hiyo hupatikana baada ya kufaulu mitihani ya shule ya sheria na huko pamoja ya kufaulu lazima kuonesha kuwa unaaminika yaani hauna mkandokando na uoneshe uelewa wa mambo mengi ambayo hayakufundishwa chuoni ambayo unaweza kukumbana nayo unapokuwa wakili.

Kukariri na kufaulu mitihani huku ukipuuzia general knowledge kunakufanya usitoshe kuwa wakili maana utakuwa na mapungufu mengi utapokutana na wajanja mtaani ambao uelewa wao wa dunia ni mpana sana ingawa siyo mawakili au waliohitimu degree ya sheria. Uwakili ni kushawishi na ushawishi lazima uwe mahiri katiika elimu ya ziada ya mtaani.
Foreign Attorney Applicant Strategy for tackling the CA Bar Exam source: Ca Bar Style how I got rejected by all the law firms I applied ... source : Gordon Chung
Mfano unaulizwa masuala ya kawaida juu ya ufahamu na umahiri lugha kiSwahili na Kiingereza ili uweze kuwasiliana / kushawishi, culture/ tamaduni, historia, umesoma novel ngapi, za aina gani, biashara halali na haramu cartels n.k, umewahi kumsikia mwandishi Mario Puzo, War and Peace mwandishi Leo Tolstoy, je umewahi kutazama series dizaini ya Better Call Saul n.k Hayo yote huyajui sasa ulikuwa unaishi dunia gani ? Hivyo mitihani ya shule ya sheria Tanzania wanatakiwa kuongeza viwango zaidi.



Admission to the bar means the permission given to a lawyer to practice law under a particular court system.

The permission is given by a court that functions under the court system in which a lawyer intents to practice.

To get admission to the bar a lawyer will have to pass a state administered bar exam after attaining a Juris Doctor degree from a law school of the state in which s/he intents to practice.

Apart from the bar exam there will be a character and fitness evaluation. Each state in the U.S sets out its own rule for admission to the bar.

A lawyer, admitted to practice in one state will not be admitted to practice in another state unless s/he passes the bar exam of that state. Attorneys of states who have entered into a reciprocal agreement can practice law in other states without full bar exam of other states. Admission to the bar is also termed as admission to practice law.


CAN A FOREIGN LAWYER PRACTICE LAW IN AMERICA

Source : Jackie Murphy
 
Naunga mkono hoja!. Kufuatia LL.B kufanywa ni biashara, vyuo vikuu vinawadahili hata vilaza na kuwapa LL.B za michongo, LST ndio chekecheke ya nchi kupata mawakili wazuri.
P
 

THE LAW SCHOOL OF TANZANIA : Taasisi ya Uanasheria kwa Vitendo


Kuandikishwa ktk daftari kama mawakili binafsi walioonesha umahiri kupitia mitihani yao hivyo wanaweza kuwawakilishi wateja katika mahakama za wilaya, mahakama kuu na mahakama ya rufaa....



KUKIMBILIA MUHURI WA UWAKILI

Wakili mwandamizi / senior legal counsel Rwechungura : Mbivu na Mbichi za Biashara ya Law Firm kwa Mawakili
Jinsi firm inavyowakuza vijana katika fani ya uwakili, senior counsel Charles Rwechungura anatufungua macho taaluma hii inayoheshimika na kuaminika inavyopikwa ikapikika ... kutambua skills alizonazo na kuzielezea .... kuna kuandika FB attorneys hutoa maandiko ... vijana tengenezeni website ili kuonessha umahiri upate kujulikana ... msuguano wa mawazo .... baadhi ya vijana hawana uvumilivu wa kujituma wanataka mambo ya haraka tofauti na senior counsels walivyokuwa wanajifua kuwa mahiri ....
Source : wakili tv
 
30 September 2022

Case : Prosecutor v. FΓ©licien Kabuga MICT-13-38

FΓ©licien Kabuga (MICT-13-38), Opening Statements, 30 September 2022


Source : IRMCT
 
Naunga mkono hoja!. Kufuatia LL.B kufanywa ni biashara, vyuo vikuu vinawadahili hata vilaza na kuwapa LL.B za michongo, LST ndio chekecheke ya nchi kuwa regulate hawa vilaza na kuhakikisha only the smart ones ndio wanakuwa mawakili ili taifa lipate mawakili bora!.
P
 
13 December 2021

VISHOKA WA UWAKILI, SIKU ZAO ZINAHESABIKA

Rais wa TLS Prof. Edward Hosea kupambana na vitendo haramu na visivyo ya kimaadili vya utendaji wa kazi za uwakili vilivyoshamiri mijini.

MAWAKILI WA KUJITEGEMEA WALA KIAPO CHA UADILIFU​

13-12-2021 0



Na Lydia Churi, Faustine Kapama na Magreth Kinabo, Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 10 Desemba, 2021 amewapokea na kuwakubali Mawakili wapya 313, ambao wamekula kiapo cha uadilifu kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa tasnia hiyo hapa nchini.

Sherehe za kuwapokea Mawakili hao zimefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wageni na waalikwa mbalimbali, wakiwemo Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) pamoja na watendaji wengine wa Mahakama wa ngazi mbalimbali.


Mawakili wapya na wageni mbalimbali walianza kuwasili katika viwanja hivyo majira ya asubuhi na shamrashamra za sherehe hiyo zilizokuwa zikirushwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Taifa-TBC 1, zilianza majira ya saa tatu asubuhi kwa Mhe. Prof. Juma ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kufika katika eneo hilo na baadaye kuwakubali na kuwapokea Mawakili hao.

Baada ya zoezi hilo, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Shamillah Sarwatt aliwainua Mawakili hao wapya kwa ajili ya kula kiapo cha uadilifu, zoezi ambalo limekuwa la kwanza tangu tasnia hiyo ianzishwe hapa Tanzania.

Baadaye, Jaji Mkuu wa Tanzania aliwakabidhi vyeti Mawakili hao kama ishara ya kuanzia sasa wanakuwa Mawakili wa Kujitegemea na watakuwa na wajibu sio tu wa kuwawakilisha wateja wao bali pia kuisaidia Mahakama ya Tanzania katika kufikia uamuzi wa haki kwa wananchi.


Akizungumza kwa ufupi kuhusu hatua hiyo, Mhe. Prof. Juma alibainisha kuwa hapo awali Mawakili wapya walikuwa hawali kiapo cha uadilifu kama walivyo watumishi wengine wa umma wanapoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, jambo ambalo lilipelekea uongozi mpya wa TLS kuja na pendekezo la kuwepo kwa utaratibu huo kwa Mawakili wote watakaokubaliwa na kupokelewa kuwa Mawakili wa Kujitegemea, kuanza kula kiapo cha uandilifu, pendekezo ambalo lilikubaliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania.


β€œNimefurahi kuona kuwa mmekula kiapo cha uadilifu, na hili wazo lilitoka kwa Rais wenu wa Chama cha Mawakili Tanganyika aliponitembelea ambapo alionesha nia ya kupambana na utovu wa maadili na akatuuliza kama kuna sehemu ambayo tunaweza kuwataka Mawakili kula kiapo cha uadilifu. Ninyi ni Mawakili wa kwanza kabisa kula kiapo cha uadilifu na tutapimana. Baada ya muda tutaangalia kama hicho kiapo kilikuwa ni cha siku ya leo kuturidhisha mpate vyeti au mtakuwa waadilifu wa kudumu,” alisema Jaji Mkuu.


Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa TLS Prof. Edward Hosea amebainisha kuwa Chama kinaendela na utekelezaji wa maono yake ya kupambana na vitendo haramu na visivyo ya kimaadili vya utendaji wa kazi za uwakili vilivyoshamiri mijini. Amesema kuwa vitendo hivyo vimesababisha kushuka kwa hadhi ya taaluma hiyo adhimu, hivyo kusababisha kukosa kuaminiwa na Serikali, wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla.

Amevitaja miongoni mwa vitendo hivyo kama uwepo wa Vishoka wa Uwakili, ambao ni baadhi ya watu wanaofanya kazi za uwakili wakati sio mawakili. Kwa mujibu wa Prof. Hosea, watu hao wamekuwa wakifanya kazi mbalimbali za kiuwakili kama kuandaa na kuthibitisha nyaraka, kushuhudia viapo, kuwakilisha wateja mahakamani na kazi nyinginezo za uwakili.

β€œWahalifu wa vitendo hivi viovu ni watu wanaojifanya ni Mawakili lakini sio, pamoja na Mawakili wanaofanya kazi zao kinyume na maadili ya uwakili kama kutoa huduma ya kisheria bila kuwa na leseni halali, kufanya kazi za uwakili katika mazingira yasiyofaa kama madukani, barabarani na vijiweni, kuruhusu mihuri yao kutumiwa na mtu asiye Wakili na kutoza ada za uwakili chini ya kiwango kilichowekwa kisheria,” amesema.

Amebainisha pia kuwa Chama cha Wanasheria Tanganyika kimekua kikipokea malalamiko lukuki kutoka wa wateja wakilalamika dhidi ya vitendo viovu visivyo vya kiuwakili vifanywavyo na Mawakili kama kuwatekeleza wateja wao na kutohudhuria mahakamani, matumizi mabaya ya fedha za wateja, kutokuwepo na mawasiliano mazuri na kuvunjika kwa usiri kati ya Wakili na mteja wake.


β€œNi wito wangu leo kwa Mawakili kuhudhuria mahakamani, kusimamia na kufanya kazi za wateja wenu kwa uadilifu, ili kuhakikisha haki za wateja zinapatikana kwa wakati na kwa utimilifu. Ni wito wangu pia kwa Mawakili kufungua akaunti za wateja ili kuepuka kutumia fedha bila idhini zao,” amesema.

Hivyo, amesisitiza Mawakili wanapaswa kuwa na mawasiliano mazuri na wateja wao kwa kuwapa mrejesho wa kesi au kazi zao, kupokea simu na kujibu ujumbe wa mteja, kutunza siri zao na kwa kufanya hivyo wataweza kulinda taaluma hiyo adhimu na kurudisha hadhi ya tasnia yao inayoonekana kushuka siku hadi siku.
Source : MAWAKILI WA KUJITEGEMEA WALA KIAPO CHA UADILIFU
 

UWAZI / TRANSPARENCY

Mfumo wa Maombi ya Uwakili na Kuratibu Mawakili

Mtambue Wakili wako bofya :

Mfumo wa Maombi ya Uwakili na Kuratibu Mawakili​

Mtambue wakili​

1 Amepatikana wakili.

Mr. Peter Kibatala 1421

Maombi Mapya ya Kuwa Wakili! Yanafungwa Oct 14, 2022

MAHAKAMA YA TANZANIA - e-WAKILI

MFANO :

MR. PETER KIBATALA
Anaruhusiwa

Mr. Peter Kibatala 1421​

Amehuisha Leseni ya Uwakili
Tazama Historia
 
Huyo jamaa yupo sahihi,mimi sijasoma sheria lakini nimesoma hiyo communication skills lakini mpaka tunafika third year second semester kuna watu hawawezi ku present, yani akisimama mbele anaona aibu kuongea
 

.... Prof. Kabudi alifanya mitihani ya Uwakili (Bar Examinations) mara kadhaa na kufeli. Prof. Kabudi aliomba kutofanya mitihani ya Uwakili(kuwa exempted) .... SOMA ZAIDI:
 
Usitudanganye na misifa yako ya ajabu, haiwezekani walimu wale wale tena wengine walokufundisha huko nyuma wafelishe law school kiasi hicho. Ni mwendo wa kujipatia pesa kupitia sap.
 
Huyo jamaa yupo sahihi,mimi sijasoma sheria lakini nimesoma hiyo communication skills lakini mpaka tunafika third year second semester kuna watu hawawezi ku present, yani akisimama mbele anaona aibu kuongea
Sasa huyo ni mtu sio kile alichosema na unasema presentation ni tofauti na kuandika barua ya maombi ya kuomba kazi hapo nakupinga na mimi nimesoma na watu wa hivyo yaan wenye soni mbele ya kadamnasi ila sio kwamba hawajui kitu nmeshawaona tangu nasoma Primary School ndio maana kuna Introvert na Extrovert watu wote hawawezi kufanana

Ushaelewa?
 
Kama Law School inachotaka ni mtu awe na uwezo wa kuandaa nyaraka za mahakamani, kujibu maswali ya mitihani kwa haraka, nk

Basi waongeze muda wa masomo, sio kulazimisha kuwa na mambo mengi kwa muda mchache yanayomshinda mwanafunzi kuyaweka kichwani, mwanafunzi asikomolewe.

Ufaulu wa Law School usigeuzwe uwe kama kufaulu kwenda peponi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…