Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini

Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini

Kwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.

Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.

Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.

Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.

Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.

Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.

Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.
Kiboko yao ni chama chetu
 
Wanaofaulu pale Law school ukisoma fact sheet yao ni chini ya 10% kila mwaka, tatizo linaweza kuwa sehemu zote mbili shule na wanafunzi.

Kiuhalisia sio vizuri kumaliza digrii ya sheria na kuunganisha law school, labda kama mtu ameshakaa kwenye.firm wakati anasoma digrii yake.

Ni vizuri na inashauriwa baada ya kumaliza digrii mtu akae angalau miezi 6 hadi mwaka 1 kwenye law firm ajifunze kwa vitendo ndio aende law school, kama ilivyokuwa lazima kwa zamani ufanye intern miaka miwili ndio ukafanye mtihani wa Bar

Tatizo digrii zote za sheria ni porojo tu (theory) ambayo hautaitumia kabisa pale law school na hata ukiitumia haifiki 25% ya ulichokivuna, law schoolni kama vile unaanza kusoma upya na unasoma mambo mapya.

Usishangae mtu ana GPA ya 4+ au hata ana PhD na law school ame disco hio ipo na inawezekana kabisa.

So ukitaka kumshauri mtu mwambie akae kwenye law firm kwanza ajifunze kisha aende sasa LST kupambania kombe
If this is the case, kwamba kabla ya mtu kwenda Law School sharti apite law firm ili kujifunza kwa vitendo, basi waweke hiyo instruction kwenye form zao za kujiunga, mwanafunzi anapojiunga awe na barua inayomtambulisha alipita firm fulani.

Japo najua, hapo Law School baada ya masomo ya theory kwisha, mwanafunzi hutakiwa kwenda field, atapita law firm then mahakamani, au vice versa, sasa kama huo muda wa field ni mdogo, basi wauongeze ili kuondoa hizo failures nyingi kupita kiasi.
 
Haha nimekukamata vizuri popoma wewe.

Narudia tena kukusahihisha; Law school inatoa mawakili sio wanasheria.

Mwanasheria na wakili ni watu wawili tofauti kabisa ila layman kama wewe hawezi kuelewa kamwe.
Mi nafkiri Law school haitoi mawakili tu, but ili uwe wakili lazima upitie law school, ndio maana sasa hiv hata ili uwe jaji au hakimu lazma uwe umepitia law school

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja!. Kufuatia LL.B kufanywa ni biashara, vyuo vikuu vinawadahili hata vilaza na kuwapa LL.B za michongo, LST ndio chekecheke ya nchi kuwa regulate hawa vilaza na kuhakikisha only the smart ones ndio wanakuwa mawakili ili taifa lipate mawakili bora!.
P
"Smart ones" wapi? sio wewe unaedai huku kila siku taifa halina mawakili competent aina ya kina Murtaza Lakha?

Mbona hauna consistence Mayalla?!

Nakuona wewe "wakili msomi" ndie unatuletea siasa kwenye haya mambo, msitetee huu ujinga unaofanyika huko Law School kisa nyie mmefaulu, simply, usiwe selfish.
 
Sasa huyo ni mtu sio kile alichosema na unasema presentation ni tofauti na kuandika barua ya maombi ya kuomba kazi hapo nakupinga na mimi nimesoma na watu wa hivyo yaan wenye soni mbele ya kadamnasi ila sio kwamba hawajui kitu nmeshawaona tangu nasoma Primary School ndio maana kuna Introvert na Extrovert watu wote hawawezi kufanana

Ushaelewa?
Kuwa introvert ndio kunamfanya mtu ashindwe hata kujitambulisha mbele ya darasa ? ,Mimi ni introvert mbona na nina rafiki introvert wengi tu ila wana confidence ,

Pia Mimi ninawajua watu kama watatu pia hawajui kuandika barua yoyote ile,Mkuu hii mada ni pana sana Boss wangu, lazima ukubali kutokana na mifano halisi hiyo niliyokupa kwamba kuna watu Elimu haijawasaidia chochote, au ngoja nikuongeze mfano mwingine

Siku yangu ya kwanza kuingia darasani chuo kikuu alikuja madam fulani na akatutaka kila mtu asimame na kujitambulisha (unasimama hapo hapo ulipokaa) unatakiwa useme wewe ni nani na umetokea wapi,kuna watu wengi walishindwa

Nahitimisha kwa kumquote lecturer mmoja alisema "darasa hili hamjawahi ku present na watu wengi hawajui presentation"
 
Sawa mkuu naona km hatuelewani sababu Chuo ulisoma sicho nilichosoma utofauti unaanzia hapo Chuo chenu kinazalisha vilaza wengi ambao hawapo competent

Naweka kalamu chini...
 
Kwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.

Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.

Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.

Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.

Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.

Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.

Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.
Kufeli Kwa wanafunzi ndio mafanikio ya hiyo Taasisi?
 
Mleta mada nini kimekufanya uje na huu uzi, sio umeona malalamiko yamezidi ndio maana? Naamini utakuwa umesoma gazeti la Mwananchi la leo, wengi mno wanafeli.

Sioni sababu kwanini wanafunzi wengi wafeli kiasi hicho, ni either walimu ni incompetent, au kama ni competent, basi wanawafelisha makusudi hao wanafunzi, na kama muda wa masomo ni mfupi wauongeze, lakini sio huu utapeli wanaoufanya wa kula bure ada za wanafunzi.

Sijawahi kuona shule inayosifiwa kwa kufelisha wanafunzi wengi hapa duniani zaidi ya hiyo Law School, sifa yao kuu imekuwa ni kufelisha, na ajabu wajinga mnawapongeza.
WANAFUNZI VILAZA MKUU
 
Siku hizi nayo huenda imekuwa simplified maana hata ambao hawana msingi wa Accouts wanazipata kirahisi tu tofauti na zamani!

Mtu amesoma course irrelevant sijui masomo gani ya arts n.k. Lakini utasikia amepata CPA [emoji87]

Naona kama heshima imeshuka!

Jamaa sijui kachoka yule?!

Hatusemi kuwa wabane sana kama zamani lakini pia sizani kama ni sahihi kuirwhisisha kiasi kwamba hata ambae hajasoma
Masomo ya commerce na bookkeeping and the related one tangu Shule ya msingi hadi chuo kikuu halafu aje kupata CPA itashangaza mno aisee?!

Kama mtu yeyote anaweza kupata!
Sasa kama mtu ana akili ya kufaulu hayo madude unataka afelishwe?
 
Idadi ya waliofaulu itapatikana baada ya supplementary kufanyika, so namaanisha itakuwa ni zaidi ya 26, hao 26 ni walio clear tu, binafsi sijaona kitu cha kushangaza hapo kwenye hayo matokeo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sio kwamba hao 26 ndo wamefaulu bila sap?? Yan wame score kuanzia “C”

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Watu kama nyie ndio mnaofeli halafu mnasingizia chuo.

Law school inatoa wanasheria wenye sifa ya kuwa mawakili.

Haitoi mawakili.

Anayetoa uwakili ni Jaji Mkuu.

Ukifaulu Law School, bado hauwi wakili moja kwa moja , lazima utume maombi kwa jaji mkuu ambaye atakuita kukufanyia interview baada ya muda wa mapingamizi kupita.

Unaweza ukafaulu law school na usiapishwe kuwa wakili kama jaji mkuu atakubaliana na mapingamizi yaliyetwa juu yako.

Hivyo Law School haitoi mawakili bali wanasheria wenye sifa ya kuwa mawakili.
Mkuu wape Elimu hao hawajui hata Utaratibu wa Mtu kuwa Wakili Law school inapokea Wanafunzi kutoka Vyuo Tatizo lipo kwenye Vyuo na Uwezo wa Wanafunzi kiakili kwani wengi wao wananunuliwa Ufaulu kwa kuhonga Fedha na Ngono .Wanafunzi wetu wamezoea kununua Mitihani kitu ambacho hakipo Law school
 
Tatizo ni digrii nyingi ni magumashi ndio maana law school hawatoboi.

Sasa mtu anamaliza digrii hajui hata kuandaa nyaraka za kufungua kesi mahakamani unafikiri atatoboa pale law school kweli?.

Amini nakwambia kuna watu wengi wanamaliza digrii ya sheria na hawajui hata kuandika barua ya kuomba kazi achilia mbali barua ya kujieleza

Law school panahitaji mtu awe na uwezo wa kuchambua mambo kwa haraka, awe na uwezo wakuandaa nyaraka za mahakamani, awe na uwezo wa kutafsuri sheria.na kujua atumie vipi zaidi ya yote awe na uwezo wakuelewa maelezo ya swali alilopewa
SAHIHI MKUU Degree nyingi ni MAGUMASHI
 
Back
Top Bottom