Mleta mada nini kimekufanya uje na huu uzi, sio umeona malalamiko yamezidi ndio maana? Naamini utakuwa umesoma gazeti la Mwananchi la leo, wengi mno wanafeli.
Sioni sababu kwanini wanafunzi wengi wafeli kiasi hicho, ni either walimu ni incompetent, au kama ni competent, basi wanawafelisha makusudi hao wanafunzi, na kama muda wa masomo ni mfupi wauongeze, lakini sio huu utapeli wanaoufanya wa kula bure ada za wanafunzi.
Sijawahi kuona shule inayosifiwa kwa kufelisha wanafunzi wengi hapa duniani zaidi ya hiyo Law School, sifa yao kuu imekuwa ni kufelisha, na ajabu wajinga mnawapongeza.