Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini


Ongea ukiwa na vithibitisho.

Pascal mayalla huwa ananiudhi na kunikera kuwa chawa wa kijani lakini kwenye hili la ushoga umeenda mbali zaidi, otherwise uwe na ushahidi sio ule wa gossip.
 
Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.


Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
 
Kazieni hapo hapo.

Mnafanya vyema sana Management ya Law School.
 
Vijana wengi hatuna adabu, unamtuhumu Mzee kwamba ni shoga !!!!
 
Yuko sawa jamaa..nipo nao wengi tu huku dsm mahakama X yani duu wanazingua sanaa baadhi
 
Kuna dogo mmoja huku mtaani alisoma PCB ila sasa hivi anasomea Accountancy IAA
 
Wewe walimu wako walipata shida sana, kuwa mwanasheria siyo lazima uwe Wakili, ila kuwa Wakili ni lazima uwe mwanasheria, ni nini huelewi hapo?
Ni kweli walimu wangu walikipata cha moto. Hakuna Mwalimu alikuja darasani kunifundisha bila kujiandaa. Maana, akijichanganya akafundisha vitu ambavyo havijui sawa sawa maswali yangu yangemuumbua.

Kuna baadhi walianza ujanja ukifika muda wa kipindi wananituma ili wafundishe wakati sipo darasani. Nikawasitukia!! Unajua nilichokifanya! "Nikajijerui mguu" ili nisitumwe. Eehe Ndiyo, unashangaa nini sasa, nilifanya hivyo!!!

Kwa ufupi nilikuwa napenda kuelewa ninachofundishwa kwa gharama yoyote Ile niliyomudu kupitia udadisi na njia nyingine.

Upo Mkuu? Ha ha haaaa!
 
Unapewa Open Book but closed to your neighbours ha ha haaaa!


7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.
Hao wanafunzi wanaofaulu wanatumia mbinu gani kufaulu?
 
Ngoja tukupumzishe lupango kwanza ukajifunze ustaarabu ban yako itakapoisha.
 

Umeandika pumba ndugu.

Pana tuhuma za wazi kuwahusu LST.

Dokezo - Tuhuma za Siasa chafu "Law School of Tanzania" wahusika wajitokeze kuzijibu

Yameombwa majibu.

Yako wapi majibu?

Nikuase tu, suala hili si dogo kama unavyodhani ati au kuwa linaweza funikwa funikwa tu na watu wenye interests na status quo au mamburura wenye husuda, chuki binafsi au wasiokuwa na ufahamu wowote.

Ni wazi kuwa wewe unaangukia kwenye kundi mojawapo hapo. Si unazijua zile roho za chuki za uswahilini?

Ndivyo hizi za kwako sasa.
 
Hiyo shule haipo hapo kwa ajili ya kufurahishana.

Wazingatie weledi and nothing else.
 
Kama umesoma Elimu ya juu,utaelewa hapa hakuna Cha kulinda Elimu,ni mbinu ya kuwakamua vijana pesa,waalimu wanaowafundisha huko vyuoni wakafauru,ndio hao hao wanaowafundisha wakiwa shule ya sheria,hapa waalimu wanakula kwa urefu wa kamba,
Ukiwaferisha kwa kiwango kile,kwenye shule ya sheria,je walipitaje kwenye shahada zao?Elimu yetu kukomolewa na waalimu ni kitu Cha kawaida,zipo degree za chupi,ambapo wanafunzi wa kike,wanatoa mambo Ili wapite,wakiume wanatoa pesa,lakini kwenye shule ya sheria,na bodi ya uasibu,huko ni mwendo wa kukomoana tu
 
wale mawakili wa kina kingai na wenzie si nao walisoma hapo ama? na kingai mwenyewe naye mwanasheria eti sijui wakili, nchi ngumu sana hii, sasa walikuwa wapi siku zote kupika wanasheria weenye akili, badala yake wakaamua kugawa uwakili kama karanga , huenda amekuja mkuu mpya hapo sasa anawaprove wrong watangulizi wake
 
Wameshaona wanapeleka vilaza, hivyo kwa sasa wanabana vilaza wasiwepo
 
Wapo sahihi Vyuoni Wanafunzi wananunua Mitihani wanapasishwa kwa kutoa Rushwa ba Ngono kitu ambacho hakipo Law school ndio maana Wanafeli Wanafunzi ni VILAZA SANA
Ingekuwepo na body ya walimu, walimu wengi sana Vilaza, wamekariri, hawajiongezi mbinu za ufundishaji...
Wajuacho wao ni kile kile walichotungia mitihani.
Kuna walimu ukiwapa maswali wanachemka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…