Hongereni sana NEMC kwa kuanza udhibiti kelele kwenye bar lakini fanyeni haya kuboresha zoezi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Nawapa pongezi sana kwa mwanzo huu!

NEMC Mkiamua mnaweza!
Mmefanikiwa kufungia bar chache zinazopiga miziki mikubwa! Ni jambo jema sana!

Naomba kushauri jambo moja ndugu zetu NEMC!
Kuna msemo Wataalam wanasema "Good approach, Bring best Result"

Hakika mmethubutu kuwaonya hawa watu wanakela sana na kelele zao!
Lakini kuna jambo mnatakiwa muwe nalo makini sana ili zoezi lenu lifanikiwe!
HAKIKISHENI Ugomvi wenu na wamiliki wa bar hauathili mlevi akose sehemu ya kwenda kulewa!

Msiongeze maadui katika operesheni yenu ili wasije geuka kuwatetea wenye bar kwa hoja za ajira na mapato ya serikali (kodi)

Punguzeni maadui kwa kuondoa kero pasipo kuunda kero nyingine!

Siyo kila bar lazima iwe na mziki mkubwa ili wateja wanywe bia! Hapana!

Hivyo nashauri fanyeni hivi!
1. Mara ya kwanza onyeni wamiliki wenyewe wa bar kwa barua na nakala ya barua hiyo waachieni hapo serikali ya mtaa wao kwa ajili ya kumbukumbu ya onyo hilo.

2. Siku ya pili Pokonyeni na mtaifishe hiyo miziki (spika&mixer).

3. Wekeni namba ya simu ya miito (call center) kwa taaarifa! Ili watu wanaporipoti taarifa ziwe recorded kwa ufuatiliaji ili hata kama kuna mazingira ya rushwa kwa baadhi ya watumishi! Muwe mnapitia report ambazo zijazwe online ofisini (yaani report ijazwe kwenye system ili iwe rahisi kuipitia) kwa kuwapigia simu wateja kama bado wanaendelea kusikia mziki baada katika eneo walilolitolea taarifa!

Maoni yangu mengine pitia uzii huu
- Ushauri: NEMC fanyeni haya ili kupunguza kelele za muziki mtaani
 
Mimi wakianza kuwadhibiti hawa walokole walioko kila mtaa na spika zao za SUNDAR ndio ntawaelewa zaidi

wanafungulia miziki SAUTI KUUBWA

yani kelele nyingi kila siku utafikiri kesho mwisho wa dunia, tena katikati ya makazi ya watu
Ni mwanzo mwema wameanza watafika tu huko tuwatie moyo
 
Mimi wakianza kuwadhibiti hawa walokole walioko kila mtaa na spika zao za SUNDAR ndio ntawaelewa zaidi

wanafungulia miziki SAUTI KUUBWA

yani kelele nyingi kila siku utafikiri kesho mwisho wa dunia, tena katikati ya makazi ya watu
Na ujiandae kuwaka moto maana kesho ndo mwisho wa dunia
 
Mbona kuna msikiti hapa naona bado.
 
Huo tayari ni mradi wa watu kupiga hela
 
Naona majirani wa kidimbwi na Juliana pale sahv meno nje

Ova
 
Japo wamefingia kiwanja changu hapo gentleman ila sawa tu najua ni wanawapa onyo kali, muziki inabidi uwe wa sauti ya chini, hizi bar tukumbuke nyingi zimejengwa karibu na makazi ya watu.

Waangalie pia bar za hapo kimara Korogwe zinapiga kelele sana hasa TTG na Bar ya pembeni yake hapo wanapocheza pool table ni kero sana, mtu uko kilo mita kadhaa ndani ndani ila ikifika saa 6 usiku makelele utandani umelala kaunta.
 
Tatizo bar nyingi sahvi wanalazimisha
Ziwe pia sehemu za kupiga mziki

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…