Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Imekaa vizuri huku ndio kujitambua na huu ndio mwanzo wa enzi mpya ya upepo wa mabadiliko wakati ni ukuta na ccm wameshafika kikomo
 
Hakika una busara ya hali ya juu, umekomaa kisiasa ni kweli wewe huteteleki.
 
Tanzania inakuhitaji kuitumikia kama mbunge katika umri huu kaka Mtatiro. Kwanini usigombee kupitia jimbo lingine liliachiwa kwa CUF?
 
mkuu nimekudharau sana, nilikuwa nakuheshimu. Wewe ukiwa kiongozi wa chama huu haukuwa wakati wa kusema haya maana taarifa si rasimi na muda wake haujafika, je maamuzi yakitenguliwa kabla ya kutangazwa, kama lengo lako ni kuwapa moyo watakaokatwa kionevu umepotea. Najua wewe umekatwa lakini umeahidiwa kitu, au wamekuahidi kuwa mwenyekiti wa CUF??

Rafiki,
Acha maneno ya kejeli, dharau ya nini sasa? Amesema amepata taarifa kutoka kwa mtu muhimu na kuzithibitisha kwa viongozi wake. Kwanza unajichanganya, mara taarifa si rasmi, mara unajua amekatwa na ameahidiwa kitu..Mgombea makini akiwapa moyo watakaokatwa kuna tatizo gani? Acha hizo...
 
Njia aliyotumia Mbatia kuingia bungeni sikuipenda na wala sijaielewa mpaka leo.Kwa nini apewe ubunge na mafisadi?Hili ni swali ambalo sijalipatia jibu mpaka leo.
Huu ndio ukomavu wa kisiasa.

Kwa wale wanaosema watamkosa bungeni kwani kuna njia moja tu ya kufika bungeni? Hebu muulizeni Mbatia.
 
Hongera sana kiongozi. Sikuwahi kufikiria kama una busara nyingi kiasi hiki. Kiukweli ninasikitika kwasababu ningependa kuona watu wenye haiba yako pale bungeni. Ila sio mbaya, kwani umesema unakwenda kusimamia mambo mengine na utarejea panapo majaaliwa.Tunakutakia kila lililojema katika harakati zako na Mungu akuweke hai na afya njema mpaka utakaporudi tena kwenye siasa za kugombea na kuchaguliwa. Kuonyesha sapoti yangu kwako, nitaipigia kura UKAWA kuanzia diwani mpaka raisi.

All the best mwana harakati MTATIRO.
 
Maneno ya busara sana haya.

Kama kila mtia nia wa nafasi za udiwani, ubunge na Urais ndani ya vyama vinavyounda Ukawa angekuwa na mawazo na msimamo kama huo alioutoa Mtatiro basi kazi ya kuliangusha 'dubwasha' la CCM tarehe 25 Oktoba mwaka huu ingekuwa rahisi mno kama vile kumsukuma mlevi.
 
Nimefurahishwa na uamuzi wako pamoja na maelezo uliyoyatoa. kweli kama haya yako moyoni mwako basi huo ndo ukomavu kisiasa cha muhimu ni kumuunga mkono aliyepitishwa na ikibidi kuzunguka nchi nzima kuwaunga mkono wagombea wa UKAWA.
 
Hadi leo najiuliza nn kilikuondoa kwenye uongozi wa CUF cjajua.kama Lipumba alikuwa kiongoz cjui ww kwann hukuwepo
 
Hongera sana Bwana Mtatiro..wewe ni kijana wa kuigwa ,a role model in politics kwa vijana.....mchambuzi mzuri wa mambo,muungwana, mkweli na mtu unayeipinda nchi yako kwa dhati.Hongera na Mungu akujalie kila lililo jema katika harakati zako.
4CHANGE
 
Kwakua sahv tunajenga nyumba moja ni kweli hatuwez gombania fito. Busara zako zimetufanya watanzania kuzidi Kuwa na umoja zaidi huku tukijua focus yetu ni kuikomboa hii nchi . nimefarijika na uamuzi wako vilevile nimefarijika na Ben kukuunga mkono .Mungu azidi kukulinda ili ufikie malengo yako na pia mafanikio ni hatua moja baada ya ingine
 
Mungu akubariki mkuu, pamoja sanaaaaa.

CCM waondoke tu, ndiyo lengo letu, kama ndivyo ntatamani nikuone kwenye campaign huko segerea na maeneo yote ya nchi hii, ndiyo furaha yangu itakamilika
 
Julius Mtatiro – B.A, M.A, LLB,
Mtia nia atakayewaunga mkono wagombea wa UKAWA jimbo la Segerea na nchi nzima,
Mapambano yanaendelea, ‪#‎IKISHINDA_UKAWA_TUMESHINDA_SOTE‬!

Mdogo wangu Julius Mtatiro, kumbuka kura hazipigwi hapa JF au kule mtaa wa pili Facebook, hamishia mechi huku site; mtaa kwa mtaa, mlango kwa mlango na mtu kwa mtu. Nakumbuka 2010 ulifanya kampeni nzuri sana ingawa kura hazikutosha, safari hii katika ushirika wa ukawa jimbo hili ni lako.
 
Last edited by a moderator:
mkuu nimekudharau sana, nilikuwa nakuheshimu. Wewe ukiwa kiongozi wa chama huu haukuwa wakati wa kusema haya maana taarifa si rasimi na muda wake haujafika, je maamuzi yakitenguliwa kabla ya kutangazwa, kama lengo lako ni kuwapa moyo watakaokatwa kionevu umepotea. Najua wewe umekatwa lakini umeahidiwa kitu, au wamekuahidi kuwa mwenyekiti wa CUF??



Ushindwe na ulegezwe
 
Back
Top Bottom