Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Nakupongeza sana Mtatiro kwa msimamo wako huu uliojali maslahi ya taifa kwenye kipindi hiki kigumu na muhimu sana kuelekea kwenye Tanzania mpya.
 
Ukawa tumewaahidi kuwaongezea wabunge tu. Ila sarakasi mnazoendelea ruka mwapunguza ari ya wananchi kuwapeni hata wabunge.

Mapambano ya ukombozi siyo mepesi kama unavyofikiria mkuu,cha msingi ni uvumilivu na kukaza mkaja na buti ili kuyafanikisha
 
Mtatiro umeonyesha ukomavu wa hali ya juu katika siasa. kweli tumekaribia nchi ya ahadi
 
Mtatiro utakuwa umelambishwa pesa ya kutosha. Siyo bure, mawazo yangu tu. sisi wanasiasa atu give up kirahisi namna hiyo
Ivi umesoma io post yake ukaielewa au unalaumu pasipo kuelewa. Jaribu kurudia tena kuisoma Mtatiro ni CUF na maelezo yake yanajitosheleza yupo tayari kumsaidia mgombea atakaesimamishwa na chadema (UKAWA) mpaka tupate jimbo. Kama ujui Mtatiro alikuwa agombee kwa tiketi ya chama chake cha CUF lakini kwa vile kila jimbo linamsimamisha mgombea moja wa Ukawa, jimbo la Segerea limeenda chadema na co CUF
 
Big up sana J. Mtatiro. Ni wachache sana wapo kama wewe!
 
hongereni tena segerea: Nina furaha tele na sijatetereka!

Na. Julius mtatiro,

ndugu zangu, nimejulishwa na mtu muhimu sana kwamba jimbo la segerea limeachwa chini ya chadema lakini ndani ya ukawa, nimeshazithibitisha taarifa hizi kwa viongozi wangu.


Kwanza niwapongeze viongozi wote wa ukawa kwa kufikia makubaliano hayo muhimu, mimi ni muasisi wa ukawa na nimekuwa katibu wa ukawa katika bunge maalum la katiba, naipenda ukawa na naamini katika ukawa; kama viongozi wameweza kukubaliana jambo hili mimi bila kinyongo chochote kile naunga mkono mapendekezo na maamuzi yao.



Pili nawataka wananchi wa segerea, wanachama wa chadema, cuf, nccr na nld na vyama vingine vyote waende kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 25 oktoba na kuchagua diwani, mbunge na rais aliyesimamishwa na chama chochote cha ukawa bila kujali mambo mengine, huu ni mwaka wa mabadiliko na lazima tuyasimamie.


Tusikubali kupumbazwa na janja za ccm kuwa angekuja mtatiro huku segerea tungewaunga mkono! Ccm ni ileile na mtu yeyote anayegombea kupitia ccm anakwenda kuimarisha mfumo uleule uliochoka, unaonuka na kukumbatia rushwa na ufisadi, wagombea wa ccm ni walewale wanaotetea mfumo uleule ambao umelifikisha taifa letu hapa tulipo. chagua vyama vya ukawa hapa segerea na nchi nzima bila kujali kuwa mtatiro siyo mgombea tena.


Kwa sababu siasa siyo ajira mimi ntajikita katika masuala mengine ya ujenzi wa taifa langu ikiwemo kuelimisha wananchi katika uchaguzi na kusimamia kampuni yangu na kisha ntajipanga kuingia bungeni mwaka 2020. Nataka kuwaonya wale wenzangu na mimi ambao wako katika siasa kwa ajili ya kutafuta mkate wa kila siku watambue kwamba siyo mahali pake na kwamba wataumbuka! Ukifanya siasa usiitegemee kama sehemu ya kipato chako hata siku moja ili usijekuathirika sana kila unapokosa fursa kama nilivyokosa mimi pale segerea.


Natoa wosia na wito kwa wagombea wote wa vyama vya ukawa nchi nzima ambao hawatapitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi huu washirikiane na wagombea waliopo ili tutafute ushindi, huu ni mwaka wa mabadiliko na mwaka wa maamuzi, shiriki kuleta mabadiliko hayo.


Na wale watakaotimkia act, adc, ccm na kwingineko kwa sababu hawakupata majimbo ndani ya ukawa nawatakia kila la heri na kuwakumbusha kuwa kimbunga cha ukawa kitawasambaratisha kokote kule waliko bila kujali walipewa nyadhifa gani.


Nawaahidi kuendelea kusimamia ukweli na kulipigania taifa langu hadi mwisho wa maisha yangu.


julius mtatiro – b.a, m.a, llb,
mtia nia atakayewaunga mkono wagombea wa ukawa jimbo la segerea na nchi nzima,
mapambano yanaendelea, ‪#‎ikishinda_ukawa_tumeshinda_sote‬!
umeonyesha ukomavu mkubwa sana kaka!mungu atakubariki.nimeanza kuamini kuwa kweli sasa wote tumejua "nia yetu"
 
Naona kuna dalili ya jina la Mahanga kujitokeza tena segerea
 
Hapana shaka kwa uthabiti wa moyo wako kwa kutokuwa mbinafsi, thamani yako imepanda maradufu!! Wewe ni mtu muhimu sana kwa mageuzi ya nchi hii, na ninakutabiria makubwa sana katika ulingo wa siasa za Tanzania. Siku kizazi chako kitakuwa kinashika rasmi hatamu ya siasa za nchi hii, wewe utakuwa mtu mzito! Na sisi wapiga kura tumeliweka hilo katika kumbukumbu zetu. Nimekufananisha na mtoto wa chacha wangwe ambae siku za karibuni alitoa jina lake katika watia nia wa kugombea ubunge tarime, na akakubali kugombea udiwani kwanza. Busara hizi zipo kwa binadamu wachache sana. Nakutakia kila la kheri. Lakini, bado nasikitika kukukosa mjengoni.
 
Ngoja Lipumba arundi kutoka kutumbua bilioni 3 za bure za chama cha zamani.
 
yaani cdm wakimrudisha mahanga ntaona ni chama cha watu ambao kwa kweli. muelekeo wamepoteza..ni zaidi ya UJUHA...ila sio utabiri kwa jinsi inavyokwenda..tusikia na kuona mengi..
 
Dah,Unastahili uenyekiti wa CUF,umekomaa kiasi cha kutosha,Hima viongozi wakuu wa CUF
 
Pole kwa kukatwa mkuu,chezea mbowe ww utabaki kua nyumbu wake na bado utakoma...
 
Asante kaka mtatiro kwa ukomavu wa kisiasa, wewe ni mfano wa kuigwa na wanasiasa walio wengi.

Masilahi ya taifa kwanza
 
Back
Top Bottom