Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Na huku ndiko tunakosema kupevuka kama si kukua au kukomaa kisiasa. Big up Mtatiro.
 
HONGERENI TENA SEGEREA: NINA FURAHA TELE NA SIJATETEREKA!

Na. Julius Mtatiro,

Ndugu zangu, nimejulishwa na mtu muhimu sana kwamba jimbo la Segerea limeachwa chini ya CHADEMA lakini ndani ya UKAWA, nimeshazithibitisha taarifa hizi kwa viongozi wangu.

Kwanza niwapongeze viongozi wote wa UKAWA kwa kufikia makubaliano hayo muhimu, mimi ni muasisi wa UKAWA na nimekuwa Katibu wa UKAWA katika Bunge Maalum la Katiba, naipenda UKAWA na naamini katika UKAWA; Kama viongozi wameweza kukubaliana jambo hili mimi bila KINYONGO chochote kile naunga mkono mapendekezo na maamuzi yao.

Pili nawataka wananchi wa Segerea, wanachama wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD na vyama vingine vyote waende kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 25 Oktoba na kuchagua Diwani, Mbunge na Rais aliyesimamishwa na chama chochote cha UKAWA bila kujali mambo mengine, huu ni mwaka wa mabadiliko na lazima tuyasimamie.

Tusikubali kupumbazwa na janja za CCM kuwa angekuja Mtatiro huku Segerea tungewaunga mkono! CCM ni ileile na mtu yeyote anayegombea kupitia CCM anakwenda kuimarisha mfumo uleule uliochoka, unaonuka na kukumbatia rushwa na ufisadi, wagombea wa CCM ni walewale wanaotetea mfumo uleule ambao umelifikisha taifa letu hapa tulipo. CHAGUA vyama vya UKAWA hapa Segerea na nchi nzima bila kujali kuwa MTATIRO siyo mgombea tena.

Kwa sababu siasa siyo ajira mimi ntajikita katika masuala mengine ya ujenzi wa taifa langu ikiwemo kuelimisha wananchi katika uchaguzi na kusimamia kampuni yangu na kisha ntajipanga kuingia bungeni mwaka 2020. Nataka kuwaonya wale wenzangu na mimi ambao wako katika siasa kwa ajili ya KUTAFUTA MKATE WA KILA SIKU watambue kwamba SIYO MAHALI PAKE na kwamba wataumbuka! Ukifanya siasa usiitegemee kama sehemu ya kipato chako hata siku moja ili usijekuathirika sana kila unapokosa fursa kama nilivyokosa mimi pale Segerea.

Natoa wosia na wito kwa wagombea wote wa vyama vya UKAWA nchi nzima ambao hawatapitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi huu washirikiane na wagombea waliopo ili tutafute ushindi, huu ni mwaka wa mabadiliko na mwaka wa maamuzi, shiriki kuleta mabadiliko hayo.

Na wale watakaotimkia ACT, ADC, CCM na kwingineko kwa sababu hawakupata majimbo ndani ya UKAWA nawatakia kila la heri na kuwakumbusha kuwa KIMBUNGA CHA UKAWA kitawasambaratisha kokote kule waliko bila kujali walipewa nyadhifa gani.

Nawaahidi kuendelea kusimamia ukweli na kulipigania taifa langu hadi mwisho wa maisha yangu.

Julius Mtatiro – B.A, M.A, LLB,
Mtia nia atakayewaunga mkono wagombea wa UKAWA jimbo la Segerea na nchi nzima,
Mapambano yanaendelea, ‪#‎IKISHINDA_UKAWA TUMESHINDA_SOTE‬!

Julius....hongera sana! Unastahili kabisa kuuchukua uongozi wa CUF wa nafasi ya MKiti...na soon utaibadili CUF kusimama katika nafasi ya juu just after CDM ktk siasa za Tz bara!
 
nimeanza kuamini kuwa SLAA ndiye amepewa kugombea SEGEREA ahsante kwa maamuzi mazuri mtatiro
 
Last edited by a moderator:
Kama haya uliyoyaandika ndiyo msimamo wako na kwamba uko tayari kuunga mkono maamuzi yoyote yatakayofanywa na chama chako nakupongeza sana.

Ulikuwa umeshaanza kujiwekea mikakati ya kuogombea katika jimbo hilo na sasa yawezekana umoja wenu UKAWA umeamua vinginevyo nawe unakubaliana nakusifu sana.

Bado ni kijana na ni hazina ya CUF kwa kesho, endelea kupigania mageuzi hapa nchini kwetu.

Nakufahamu vema ni mpiganaji mzuri na nakumbuka kipindi cha 2005 ukiwa na Mwikwabe mlivyopigania wanafunzi kipewa mikopo.

Nikupe matumaini kuwa utafika mbali kama utaendeleza hurka uliyoonesha na si lazima uwe umependa bali unaamini kitu kwa maslahi ya umma japo moyoni una maumivu na haya ndiyo "Maamuzi magumu"
 
Mkuu Mtatiro,
Nakupongeza kwa maamuzi yako.
Natumai huko mbeleni Ukawa watajua jinsi ya kukufix sehemu.
Natamani nikuone bungeni unaendeleza mapambano kama wakina Mnyika na wengineo.
 
uchaguzi umegeuka kuwa movement for change , haijalishi nani ni nani , asante mtatiro .
 
Mtatiro tafuta jimbo lingine hata kama polini huko kiu yangu nikuone mjengoni. Nina Imani unaweza kumtoa yeyote hats ukienda kwenye jimbo LA lusinde
 
Mtatiro,
Honera sana kwa uzalendo uliouonyesha.Natumai kuna njia nyingine inaweza fanyika kukupatia nafasi eneo jingine manake kiukweli uwepo wako unahitajika sana bungeni.Safu ya wapiganaji itakua imekamilika uwepo wako.

God bless you brother
 
Hivi Julius Mtatiro anagombea jimbo gani??
werason inaelekea huu uzi hujausoma. Ni kwamba huyu jamaa alitia nia kugombea jimbo la segerea kupitia CUF. Lakini kwa makubaliano ya UKAWA, jimbo hilo litasimamisha mgombea wa CHADEMA. Kwahiyo yeyr hatagombea tena.
 
Last edited by a moderator:
Ukawa mbelekwambele mtatiro kweli wewe umedhirisha watu wa musoma tunavyotaka mabadiliko,safi sana kaka
 
kashakatwa huyu hana lolote, au nae anaenda kufanya utafiti??

HONGERENI TENA SEGEREA: NINA FURAHA TELE NA SIJATETEREKA!

Na. Julius Mtatiro,

Ndugu zangu, nimejulishwa na mtu muhimu sana kwamba jimbo la Segerea limeachwa chini ya CHADEMA lakini ndani ya UKAWA, nimeshazithibitisha taarifa hizi kwa viongozi wangu.

Kwanza niwapongeze viongozi wote wa UKAWA kwa kufikia makubaliano hayo muhimu, mimi ni muasisi wa UKAWA na nimekuwa Katibu wa UKAWA katika Bunge Maalum la Katiba, naipenda UKAWA na naamini katika UKAWA; Kama viongozi wameweza kukubaliana jambo hili mimi bila KINYONGO chochote kile naunga mkono mapendekezo na maamuzi yao.

Pili nawataka wananchi wa Segerea, wanachama wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD na vyama vingine vyote waende kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 25 Oktoba na kuchagua Diwani, Mbunge na Rais aliyesimamishwa na chama chochote cha UKAWA bila kujali mambo mengine, huu ni mwaka wa mabadiliko na lazima tuyasimamie.

Tusikubali kupumbazwa na janja za CCM kuwa angekuja Mtatiro huku Segerea tungewaunga mkono! CCM ni ileile na mtu yeyote anayegombea kupitia CCM anakwenda kuimarisha mfumo uleule uliochoka, unaonuka na kukumbatia rushwa na ufisadi, wagombea wa CCM ni walewale wanaotetea mfumo uleule ambao umelifikisha taifa letu hapa tulipo. CHAGUA vyama vya UKAWA hapa Segerea na nchi nzima bila kujali kuwa MTATIRO siyo mgombea tena.

Kwa sababu siasa siyo ajira mimi ntajikita katika masuala mengine ya ujenzi wa taifa langu ikiwemo kuelimisha wananchi katika uchaguzi na kusimamia kampuni yangu na kisha ntajipanga kuingia bungeni mwaka 2020. Nataka kuwaonya wale wenzangu na mimi ambao wako katika siasa kwa ajili ya KUTAFUTA MKATE WA KILA SIKU watambue kwamba SIYO MAHALI PAKE na kwamba wataumbuka! Ukifanya siasa usiitegemee kama sehemu ya kipato chako hata siku moja ili usijekuathirika sana kila unapokosa fursa kama nilivyokosa mimi pale Segerea.

Natoa wosia na wito kwa wagombea wote wa vyama vya UKAWA nchi nzima ambao hawatapitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi huu washirikiane na wagombea waliopo ili tutafute ushindi, huu ni mwaka wa mabadiliko na mwaka wa maamuzi, shiriki kuleta mabadiliko hayo.

Na wale watakaotimkia ACT, ADC, CCM na kwingineko kwa sababu hawakupata majimbo ndani ya UKAWA nawatakia kila la heri na kuwakumbusha kuwa KIMBUNGA CHA UKAWA kitawasambaratisha kokote kule waliko bila kujali walipewa nyadhifa gani.

Nawaahidi kuendelea kusimamia ukweli na kulipigania taifa langu hadi mwisho wa maisha yangu.

Julius Mtatiro – B.A, M.A, LLB,
Mtia nia atakayewaunga mkono wagombea wa UKAWA jimbo la Segerea na nchi nzima,
Mapambano yanaendelea, ‪#‎IKISHINDA_UKAWA TUMESHINDA_SOTE‬!
 
Hawa ndio aina ya watu tunao wahitaj, ila ningetamani sana Mtatiro awepo bungeni
 
Pamoja sana kamanda mtatiro. Akishinda kamanda mpendazoe tumeshinda sote. Ukawa oyeee!
 
Back
Top Bottom