Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Mtatiro, u have political maturity. But please don't say u will not contents in any constituency, we need you mjengoni. Consult with UKAWA leadership ili wakupe jimbo. This is the feedback kwa wapenda maendeleo wote.

Contest, not contents mkuu.
 
HONGERENI TENA SEGEREA: NINA FURAHA TELE NA SIJATETEREKA!

Na. Julius Mtatiro,

Ndugu zangu, nimejulishwa na mtu muhimu sana kwamba jimbo la Segerea limeachwa chini ya CHADEMA lakini ndani ya UKAWA, nimeshazithibitisha taarifa hizi kwa viongozi wangu.

Kwanza niwapongeze viongozi wote wa UKAWA kwa kufikia makubaliano hayo muhimu, mimi ni muasisi wa UKAWA na nimekuwa Katibu wa UKAWA katika Bunge Maalum la Katiba, naipenda UKAWA na naamini katika UKAWA; Kama viongozi wameweza kukubaliana jambo hili mimi bila KINYONGO chochote kile naunga mkono mapendekezo na maamuzi yao.

Pili nawataka wananchi wa Segerea, wanachama wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD na vyama vingine vyote waende kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 25 Oktoba na kuchagua Diwani, Mbunge na Rais aliyesimamishwa na chama chochote cha UKAWA bila kujali mambo mengine, huu ni mwaka wa mabadiliko na lazima tuyasimamie.

Tusikubali kupumbazwa na janja za CCM kuwa angekuja Mtatiro huku Segerea tungewaunga mkono! CCM ni ileile na mtu yeyote anayegombea kupitia CCM anakwenda kuimarisha mfumo uleule uliochoka, unaonuka na kukumbatia rushwa na ufisadi, wagombea wa CCM ni walewale wanaotetea mfumo uleule ambao umelifikisha taifa letu hapa tulipo. CHAGUA vyama vya UKAWA hapa Segerea na nchi nzima bila kujali kuwa MTATIRO siyo mgombea tena.

Kwa sababu siasa siyo ajira mimi ntajikita katika masuala mengine ya ujenzi wa taifa langu ikiwemo kuelimisha wananchi katika uchaguzi na kusimamia kampuni yangu na kisha ntajipanga kuingia bungeni mwaka 2020. Nataka kuwaonya wale wenzangu na mimi ambao wako katika siasa kwa ajili ya KUTAFUTA MKATE WA KILA SIKU watambue kwamba SIYO MAHALI PAKE na kwamba wataumbuka! Ukifanya siasa usiitegemee kama sehemu ya kipato chako hata siku moja ili usijekuathirika sana kila unapokosa fursa kama nilivyokosa mimi pale Segerea.

Natoa wosia na wito kwa wagombea wote wa vyama vya UKAWA nchi nzima ambao hawatapitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi huu washirikiane na wagombea waliopo ili tutafute ushindi, huu ni mwaka wa mabadiliko na mwaka wa maamuzi, shiriki kuleta mabadiliko hayo.

Na wale watakaotimkia ACT, ADC, CCM na kwingineko kwa sababu hawakupata majimbo ndani ya UKAWA nawatakia kila la heri na kuwakumbusha kuwa KIMBUNGA CHA UKAWA kitawasambaratisha kokote kule waliko bila kujali walipewa nyadhifa gani.

Nawaahidi kuendelea kusimamia ukweli na kulipigania taifa langu hadi mwisho wa maisha yangu.

Julius Mtatiro – B.A, M.A, LLB,
Mtia nia atakayewaunga mkono wagombea wa UKAWA jimbo la Segerea na nchi nzima,
Mapambano yanaendelea, ‪#‎IKISHINDA_UKAWA TUMESHINDA_SOTE‬!

Hakika kaka yangu MTATIRO kwa hekima na busara iliyokuongoza katika jambo zito kama hili.
 
Kwanza mamlaka ya kupanga wagombea wa vyama vingine wanayatoa wapi hawa Chadema?
 
hongera sana umeonyesha uzalendo Mkubwa sana na pia ukomavu wa kisiasa ulio washinda ma Dr na prof,taifa linahitaji watu kama wewe,umenifunza jambo kubwa sana
 
Nahisi mtatiro atakaimu uenyekiti wa CUF atakuwa ameshauriwa asigombee tu.

Kwani akigombea na akawa Mwenyekiti kuna shida gani?He is still young anaweza kusubiri 2020.
 
Kti ya watu ambao huwa nawafuatilia ili kunipanua kuhusu siasa ni wewe Kaka yangu JM, Hakika ulialiw umekmilika nakufuatilia sahemu nyingi makala zako kwenye gazeti la mwananchi, kwenye tv na sehemu yeyote nikayoweza ili kupata uchambuzi wako, hongera sana wewe ni kizazi halisi cha akina Nyerere, Kwame, Mandela na wengine, siku zote nitaedelea kukusoma ili kupata maarifa na ufahamu.
 
Hatuweki maneno mengi bali tu tunasema, shukrani kwa kupata hekima na kubali kuitumia.
 
Duh UKAWA umekuwa ni umoja wa kugawana vyeo, haya Mtatiro wenzako wanakufariji kwa ndoto za abunuasi eti utakuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam UKAWA ukichukua nchi.

Utasubiri sana na baada ya uchaguzi mkuu UKAWA utasambaratika na kila chama kitakuwa kinajilia karuzuku kake huku chama chako kikiwa tayari kimekufa kifo cha mende kimewekwa musiums na wanaokupongeza sasa wakiwa wanakudhihaki na kukwambia kwanini hukujiunga na CHADEMA siku nyingi? huku wakiendelea kusema ona sasa sie CHADEMA bado ni chama kikuu cha upinzani na CUF ni CCM B.
 
Mtatiro mwanangu mungu akubari sana kukubali mstokeo. Tunakuomba uwe kampain meneja yeyote ambae jina lake litakae rudi kwa ajili ya kupigia kura.
 
Kaka, we ni mtu wa ajabu saana, nakuheshimu na unafaa kuwa kiongozi mkubwa saana hapa Tanzania, leo yako kaka nitaiweka mpaka kesho. Nitaja simulia watoto wajifunze kwako. Kuna vitu nimesoma within a lines nimefarajika saaana, pigania UKAWA, pigania mabadiliko ili siku moja wa Tanzania wajue nini ulikuwa unafanya.
 
Back
Top Bottom