Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Juni 8 wiki iliyopita TDPC na UDSM walifunga mkataba wa kujenga kituo kikubwa cha kuchataka gesi asilia eneo la UDSM karibu na Hosteli za Magufuli. Kito hicho Kitatazama barabara ya Sam Nujoma.
Lengo la kujenga kituo cha CNG (Compressed Natural Gas) ni kurahisha upatikanaji wa gesi katika maeneo ambayo hayana huduma ya gesi kwa njia ya mabomba. Kituo kikubwa UDSM kitakuwa kimekamilika hadi kufikia 2023.
Kituo hicho mama cha UDSM kitahudumia vituo vidogo vitatu ambapo vituo viwili viko katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kituo kimoja kitakuwa katika soko la samaki feri Kigamboni Dar es Salaam.
Vituo vya muhimbili vitaanza kuzalisha mvuke kwa ajili ya kupikia pia baadae wataanza kuuza kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Gesi hiyo itaweza pia kusafirishwa kuelekea mikoani kwa ajili ya kuwasogezea wateja gesi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo kupikia.