Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nawapongeza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za mwanzo ni mwanzo mzuri kwa timu zote mbili itawajengea hali ya kujiamini na kujipanga vizuri kwa michezo ijayo,.
Pamoja na kushinda timu zote 2 zimekutana na timu ambazo zina viwango vya chini, ukianzia Nyassa big bullet ya malawi ni timu inayofanya vizuri kwenye ligi yao lakini ni ligi isiyokuwa na ushindani ukilinganisha na ligi ya Tanzania na icho ndicho kilichowahukumu leo.
Unaweza kuwa bora miongoni mwa wabovu na ukatawala eneo lako, kwaiyo ushindi wa simba usiwafanye wakavimba vichwa kwamba wameishinda timu bora na wakajisahau kurekebisha mapungufu yao kuelekea kukutana na Red arrows au Ile timu ya angola, vivyo hivyo kwa yanga wanatakiwa kujipanga kisawasawa kuelekea kukutana na Al hilal au St george ya ethiopia, apo ndipo kuna kipimo sahihi awa zahlan wamewafumbua macho kwamba utakiwi kudharau timu yoyote kwenye michuano hii maana mpaka inafika hapo aikufika kwa bahati mbaya, papara yao na presha ya kutaka kufunga bila mipango ndiyo iliyowakosesha mabao kipindi cha kwanza.
Nafikiri Nabi aliliona hilo akawatuliza kipindi cha pili, Timu zote mbili zinatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kufanikiwa kutinga hatua ya makundi sio lelemama, Timu itakayojisahau kwa kujiona imekamilika baada ya kuwaondoa vibonde basi itakula kwao hatua inayofuata