Hormuz yabana dunia, bei ya mafuta yazidi kuwa juu

Hormuz yabana dunia, bei ya mafuta yazidi kuwa juu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgogoro wa Mashariki ya Kati umeifanya dunia kuendelea kuonja joto la jiwe, baada ya bei ya mafuta ghafi aina ya Brent kuendelea kuwa juu tangu Agosti, kutoka wastani wa dola 91 kwa pipa mwezi huo hadi kuvuka dola 100 Septemba na kuendelea kuzunguka kiwango hicho mwanzoni mwa Oktoba, hali iliyopelekea bei za mafuta katika nchi mbalimbali kuendelea kuwa juu.

1791266371229.png
Petroli imefikia takribani Tsh. 8,462 kwa lita Malawi, Tsh. 7,441 Denmark, Tsh. 7,236 Netherlands, Tsh. 6,066 Uingereza, Tsh. 5,433 Zimbabwe, Tsh. 5,239 Rwanda, Tsh. 4,499 Uganda, Tsh. 4,347 Kenya na Tsh. 4,194 Afrika Kusini, huku Tanzania ikiwa Sh3,796 na Zambia Tsh. 3,377 huku nchini Marekani imefikia karibu Sh16,850 kwa Gallon, kutoka Tsh. 12,200 kabla ya mgogoro, ongezeko la takribani asilimia 38.

Soma >> EWURA yatangaza bei mpya za mafuta. Bei ya petroli imeshuka kwa Sh 102 kwa lita, dizeli ikishuka kwa Sh 101 kwa lita

Tanzania na nchi nyingine zinazoagiza mafuta sasa zinakabiliwa na mabadiliko ya bei katika mwezi huu wa Oktoba, wakati mafuta yaliyonunuliwa katika kipindi ambacho bei ya mafuta ghafi ilikuwa juu yakianza kuingia katika masoko yao.

1791266384174.png
Tanzania hadi sasa imeendelea kuwa na bei himilivu petroli Dar es Salaam ikiwa Tsh. 3,796 kwa lita, chini ya Tsh. 3,898 ya Agosti na Tsh. 3,990 ya Julai, lakini bei kubwa ya mafuta ghafi ya Agosti na Septemba inaweka shinikizo jipya katika bei za Oktoba na miezi inayofuata.

1791266418053.png
Ifahamike kuwa mgogoro wa Mashariki ya Kati na hofu ya kuvurugika kwa uzalishaji na usafirishaji kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz vimeendelea kuweka soko la mafuta duniani katika presha ambapo njia hiyo ni miongoni mwa mishipa muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani, huku hatari ya usalama ikiongeza pia gharama za meli na bima na kufanya mafuta yanayofikishwa katika nchi zinazoagiza kuwa ghali zaidi.
 
Kule nchini kwetu Msumbiji tuliambiwa huo mgogoro sisi hautatuathiri kabisa tuwe na amani😄
 
Kwani hao wagalatia nao wanategemea mafuta kutoka nchi za waarabu (magaidi). Najua leo kumbe wanategemea mafta kutoka kwa hao wanaowaita magaidi.
 
Hela ya Tanzania imesha kuwa SI unit siku hizi?
Bei ya petroli Malawi ni Mk 5,619 (UsD 3.24) kwa lita,ambayo ni sawa Tsh. 3,596 kwa lita,walio mpakani wananunua petroli Malawi.
Waswahili kwa kampeni za kijinga tu bei ya petroli inatafsiriwa kwa Tshs kwa kila nchi as if hiyo hela ina nguvu ya kuingia kila nchi kwa matumizi ya soko.
 
Ukifika mpakani toa shilingi 1 yako utapewa Mk0.64.
aisee sasa ndio umeandika nini
kwahiyo pesa ya malawi ni kubwa kuliko ya Tz lakini kwenye mafuta pesa ya tz inakuwa kubwa kubwa kuliko ya malawi.
Hesabu za wapi hizi..

unajikaanga mwenyewe unasema ni uss 3.24 lakini eti ni sawa na Tsh 3,596
 
Madafu tu ze wodi
 
Kwani hao wagalatia nao wanategemea mafuta kutoka nchi za waarabu (magaidi). Najua leo kumbe wanategemea mafta kutoka kwa hao wanaowaita magaidi.
Siasa zao ni kuwadanganya raia wa kawaida
Lakin mlango wa nyuma wanafanya biashara kama kawaida
 
aisee sasa ndio umeandika nini
kwahiyo pesa ya malawi ni kubwa kuliko ya Tz lakini kwenye mafuta pesa ya tz inakuwa kubwa kubwa kuliko ya malawi.
Hesabu za wapi hizi..

unajikaanga mwenyewe unasema ni uss 3.24 lakini eti ni sawa na Tsh 3,596
Una elimu ya matumizi ya pesa?
Mmarekani ana hela ya Tanzania mnavyo ifanananisha kwenye soko la Malawi?
Unadhani Malawi wanatumia hela ya madafu yenu kupata dola?
1Mk = 0.64Tsh
1 USD= 1,730Mk
1 USD= 2,630 Tsh
 
Una elimu ya matumizi ya pesa?
Mmarekani ana hela ya Tanzania mnavyo ifanananisha kwenye soko la Malawi?
Unadhani Malawi wanatumia hela ya madafu yenu kupata dola?
1Tsh = 0.64Mk
1 USD= 1,730Mk
1 USD= 2,630 Tsh
una shida kwenye hesabu wewe..sikulaumu.
haya hapo nitafutie usd 3.24 itakuwa sawa na kias gani cha tsh.
 
Nafikili ni muda wa kuswich kwenda matumizi ya umeme na jua.
 
Back
Top Bottom