Hospitali Binafsi wana Utu kuliko Hospitali za Serikali

Haingii hasara ila inaingiza hasara kwa kuongeza vifa vya watu masikini na vipi wale wanaoenda kutibiwa huko Apolo India na kwingineko kwa gharama za juu na Serikali inalipia na wanaishia kufia huko na kurudi wakiwa ndani ya friji hapo unasemaje?
 
Japo nipo serikalini pia lakini Taasisi za Serikalini nyingi utasikia wana jitamba wana Security ya kazi ivyo wana fanya mambo bila kujali .na hawa wakija mahakamani baada ya kufukuzwa kazi nikapewa case yao nahakikisha nawakanda kisawa sawa
 
Sio kweli Muhimbili mara nyingi tu watu wanatibiwa na mwishowe wanahitajika kulipa bills iwe mgonjwa amepona ama amefariki.

Shemeji yangu walimfanyia upasuaji wa kuzalisha mtoto hospital ya mwananyamala bills ilikuwa laki 3 walimzuia kuondoka mpaka pesa ilipolipwa.

Hospital Kuna kitu kinaitwa emergency hiyo ukiwa muhudumu wa afya unaangalia kwanza kuokoa uhai wa mtu Kisha mambo mengine yanafuata baadae.
 
Japo nipo serikalini pia lakini Taasisi za Serikalini nyingi utasikia wana jitamba wana Security ya kazi ivyo wana fanya mambo bila kujali .na hawa wakija mahakamani baada ya kufukuzwa kazi nikapewa case yao nahakikisha nawakanda kisawa sawa
Hahaha Muheshimiwa Jaji kwa hio wakisogezewa kwenye meza yako ya hukumu unawapiga malungu
 
Utendaji makini uliisha na Mwendazake..
Ukienda private kila kitu ni pesa na unapatiwa matibabu kutokana na pesa YAKO..
Kila mmoja wetu anatamani kupata Huduma bora sema ndio hvyo uwezo changamoto unless hizo Hospital na SHULE va Govt majengo wangefugia POPO.
 
Umefafanua vizuri.
Hapa nadhani watunga sheria na sera za haya mambo wangeiangalia hii ishu kuwe na unafuu kwa raia.
 
Tatizo ni mfumo wala si watu. Hao hao watumishi/wafanyakazi uliowakuta huko private hospital ndiyo hao hao utawakuta kesho kwenye hospitali za umma/serikali wamebadilika, kwa nini? Kwa sababu ya mfumo wa utendaji ambao wanakutana nao serikalini. Kwa hiyo wakiwa private hospital utawabariki na kuwasifu kwa sababu mfumo wa utendaji private sector ni tofauti na wa serikali.

Hivi karibuni serikali imetoa majina ya watumishi wengi wa kada ya afya ambao wengi wao watatoka huko private hospitals na kwenda serikalini. Wakiwa private hospitals utendaji wao ni tofauti sana na utakavyokuwa huko serikalini, wakifika huko serikalini wanakuta kuna namna ya utendaji au uendeshaji wa mambo ambao ushawekwa na wengi hufuata. Ukijifanya kuleta mapinduzi utaishia tu kuungana nao kwa sababu hakuna atakayekuunga mkono ukija eti kuleta utendaji wa private hospitals, utaachwa uhangaike mwenyewe hatimaye unakuwa kama wao.
 
Tulipofika hospitali ile tukaambiwa mgonjwa wenu tutamfanyia upasuaji na malipo mtayalipa baada ya huduma. Ikawa hivyo. Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwaumba hawa watu wenye Roho Nzuri na tunawatakia maisha marefu.

Kazi za watoa huduma za afya wanatakiwa kuokoa maisha ya wagonjwa kwanza
1)kuto sababishia madhara DO NO HARM

2)kumsaidia mgonjwa kumuondolea maumivu,kuokoa maisha huduma kwa faida ya mgonjwa BENEFICIENCE

3)Kutunza siri za mgonjwa CONFIDENTIALITY, na privacy
4)kwa kujali utu wa mgonjwa na matakwa maamuzi ya mgonjwa PT AUTONOMY

Yani PATIENT'S CENTERED kifupi AFYA USALAMA wa mgonjwa ndio KIPAUMBELE cha kwanza ni kuokoa maisha kwanza.

TENA KWENYE DHARURA EMERGENCY kipaumbele cha kwanza ni kuokoa maisha kumstabilize mgonjwa awe stable kwanza ,kumuondolea hatari ya maisha ,KUOKOA MAISHA KWANZA.

Halafu mambo ya malipo na utaratibu wa malipo UTAFUATA BAADAE.

Kwa uzoefu wangu mdogo hospitali za serikali ndio zinahudumia wagonjwa bila kutanguliza pesa kuliko hospitali binafsi.

Nimeshuhudia wagonjwa walio okotwa mahututi wakiwa hawana fahamu bila kutambulika utambulisho wao wametibiwa katika hospitali za serikali bila kulipa hata mia kwa muda mrefu mpaka wakapona ,tena si kutibiwa tu huduma zote mpaka chakula na kulishwa,kuhudumiwa kusafishwa mwili haja kubwa na ndgo,kuogeshwa,huduma zote n.k wqkihudumiwa na madakatari na wauguzi,wahudumu wa afya pasipo uwepo wa ndugu zake kuwepo pasipo kutambulika utambulisho wao hata wa ndugu zao.
Na pasipo kulipia hata mia mbovu.
Na hata kwenye vyombo vya habari huwa tunaona wagonjwa hao waliotibiwa wakitangazwa kutafuta ndugu zao waweze kuwatambua.
 
Umeimaliza kila kitu
 
Niiweke hivi. Baadhi ya hospitali wapo na wana ofisi zao katika hospitali. Tatizo ni mgonjwa kutokujua utaratibu pale ambapo hana pesa ya malipo au Bima.

Wao nao ustawi wa jamii wakisha jilidhisha hujiwezi kifedha kuna Boss juu yao wanampelekea taarifa ili awape GO ON..
 
Ni kweli huduma atapata.

" Huduma ya oparesheni tutakupatia ila madawa utanunua, vipimo tutakupa bure ila dawa utanunua. Tata kutibu ila anza kupiga simu ndugu watafte angalau chochote" kwa mtu ambaye hajiwez kabisa ( kama walioko TASaF) hukosa huduma zote

# Ingia mikoani ndanindani uone wa Tanzania wanayopitia
 
Haingii hasara ila inaingiza hasara kwa kuongeza vifa vya watu masikini na vipi wale wanaoenda kutibiwa huko Apolo India na kwingineko kwa gharama za juu na Serikali inalipia na wanaishia kufia huko na kurudi wakiwa ndani ya friji hapo unasemaje?
Achana na hao wa kuchangiwa kutibiwa nje ya nchi.

Humu tu mikoani. Ni ngumu sana mtu ambae hayupo vizuri kiuchumi kutibiwa kuanzia kumuona Daktari, vipimo, dawa , opareshini at kulazwa bure.

Msaada tena wa kibinadamu kwa mtoa huduma , huwa utakua sio vyote ivyo aidha oparesheni dawa uta nunua au vipimo dawa utanunua..

Ndo tumtafute waziri wa Afya atoe utaratibu kam hujiwezi kifedha na unataka huduma zote utaratibu ni upi?

Jiulize kwanini , Elimu bure katika shule za serikali wamefanikiwa angalaukuna michango inajitokeza kidogo ila kwa upande wa Afya Tiba bure imeshindikana?
 
Kwa hiyo bora mtu afe, utawala wa Sa100 ni hovyo sana watumishi wa umma ni wavivu kupita maelezo
 
Huduma zote za umma wana nyodo sana Kama mali za baba zao
Ni kila mahali maana hata ukimkuta boss wao ndio hovyo kuliko hata mfagiaji hapo
Huduma mbaya na majibu yasiokuwa na stara
Hiyo ni kwa sababu ubaya unaanza juu
 
Kwa hiyo bora mtu afe, utawala wa Sa100 ni hovyo sana watumishi wa umma ni wavivu kupita maelezo
NI tatizo la mifumo. Serikali itoe muongozo kwa watu wasio jiweza namna ya kupata matibabu pasipo malipo.

Mbona wanatambua kuna watu hawajiwezi kiuchumi na wanatoa pesa za TASAF ila ku gharamikia matibabu yao inakua shida.

Elimu bure wame fanikisha ila Tiba bure inakua ngumu
 
Siyo hosipitali tu, taasisi nyingi za umma zinatoa huduma mbovu sana hasa kwenye hii awamu ya sita.
Unajua kwanini? Kuna mazingira serikali imeyatengeneza yana influence mtu afanye kazi kama analazimishwa, yaani bora liende. In private sector ukifanya huo ujinga unakuwa fired asap, quality of service ni kipao mbele cha kwanza
But in gov si kipao mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…