Hospitali inapomwambia Mwanachama wa NHIF Dawa fulani haipatikani kwenye Bima, Mgonjwa anathibitishaje kwamba ni kweli?

Hospitali inapomwambia Mwanachama wa NHIF Dawa fulani haipatikani kwenye Bima, Mgonjwa anathibitishaje kwamba ni kweli?

Baada ya misukosuko ya Serikali na Hospitali binafsi kwenye Huduma za Afya kwa Wanachama wa Bima ya Taifa ya NHIF kuna kama utaratibu umeibuka wa kunyimwa baadhi ya Dawa kwa kigezo kwamba hazipatikani kwenye Bima

Sasa Me natamani kufahamu Hospitali wanaponiambia Dawa fulani siwezi kuipata kwa Bima, Je, Mimi mwanachama kuna Mfumo wowote unaonisaidia kuthibitisha kile ninachoambiwa au ndio inabidi tu nikubali nikaisake shilingi ninunue hiyo Dawa?
NHIFTZ
Tunaomba mjibu hili swali kwa ajili ya wanaotaka kufahamu
 
Hospitali Binafsi Nyingi ziko Level C na D ambayo ni sawa na District Hospital So Angalia hapa Dawa zilizopo kwenye Level C..

Japo Kairuki na Hospitali Kubwa kama Regency Na zingine ziko Level ya D na S ambayo Ni sawa na Regional refferal au Zonal..
Mkuu nisaidie Package ya Kitita cha Referral na Zonal/National Hospital...
 
Acheni ujuaji, kama dawa ipo kwenye kitita utapewa..... shida ni kitita na sio uwepo wa dawa hiyo kwenye rafu.
 
Mtuelekeze sasa namna ya kuitumia iyo catalogue iyo miandiko ya madaktari tutajua Tu kuisoma 🥱
 
Tuone Fikra za Kipumbavu zilivyo:

Mtoa huduma unanunua dawa kwa 500/=

Hiyo Dawa ukimhudumia mgonjwa then Bima wanakulipa 400/=.

Ni kweli mtoa huduma hatakunyima hii Dawa..
Huyo kaamua kufikiria kama kuku.
 
Tuone Fikra za Kipumbavu zilivyo:

Mtoa huduma unanunua dawa kwa 500/=

Hiyo Dawa ukimhudumia mgonjwa then Bima wanakulipa 400/=.

Ni kweli mtoa huduma hatakunyima hii Dawa..
Kama hilo lingekuwepo kweli isingekuwa kwa dawa moja au mbili tu naamini ingekuwa ni kwa dawa na huduma nyingine zote na kama ni hivyo ni dhahiri watoa huduma pamoja na nia yao njema ya kusaidia wananchi lakini wangeshindwa kumudu gharama za uendeshaji hivyo wangeacha kabisa kutoa huduma kwa walengwa, tuache kutungatunga mambo ili kulazimisha fikra za ovyo.
 
Hizi Bima za Afya ni wizi mkubwa kwa Wananchi na inaoneka Serikali haijali kabisa afya za Watanzania yaani Watumishi wako halafu unawasumbua kwenye matibabu kama chakula vile yaani Nchi inajali watu wakiwa wazima na sio wakiwa wagonjwa.

Kama pana kitu wamefanya cha hivyo ni kuhusu hiyo Bima na ile Bima ya watoto ni upuuzi mtupu wanafanya halafu utawaona wanazunguka Nchi nzima kutangaza Sera zao kwa gharama kubwa huku vitu muhimu wakiwa wameharibu...
 
Kama hilo lingekuwepo kweli isingekuwa kwa dawa moja au mbili tu naamini ingekuwa ni kwa dawa na huduma nyingine zote na kama ni hivyo ni dhahiri watoa huduma pamoja na nia yao njema ya kusaidia wananchi lakini wangeshindwa kumudu gharama za uendeshaji hivyo wangeacha kabisa kutoa huduma kwa walengwa, tuache kutungatunga mambo ili kulazimisha fikra za ovyo.
Ili waendelee kutoa huduma lazima wafanye udanganyifu kama huu tunaouona.

Kama ungekuwa mtoa huduma ungeelewa hii kitu.
 
Hii nchi hata njia inazotumia kutatua kero nazo ni kero tu kwa wananchi mfano mkandarasi wa mchongo aliepewa zabuni ya kujenga mabanda toka mwaka jana hajamaliza hii inaashiria hakuwa na uwezo wafanyabiashara wanazidi kuteseka na Hali ya mvua zinazoendelea
 
Kama taifa bado tunasafari ndefu kupata usawa kwenye kila jambo la kitaifa.....tunaitaji maombi
 
Nilichoka nilipoenda hospital fulani ya private kubwa tuu hapa Dar ipo Posta waliponiambia dawa ya kifua ZECUF imeondolewa kwenye Bima na hakuna mbadala wake,sasa sijajua hill swala lipoje kama lina ukweli wowote.
 
We nae acha kukaza fuvu,hizo dawa ambazo hupewi kwa bima ujue ndio za gharama kubwa,manake kama zingekuwa zinaruhusiwa mahospitali yangepata pesa nyingi sana. Hakuna mtoa huduma ambaye atakunyima dawa ya gharama kwa makusudi,pia Catalogue ipo inayoonesha dawa zinazoruhusiwa na bei zake na dawa zisizoruhusiwa. Ni kitabu kabisa kina kurasa zaidi ya mia.
Kwa uelewa wangu, mtoa mada alitaka msaada wa ufafanuzi kuhusu swala lake, kwa maana nyingine anataka kujua coz hajui ni kwanini.
Tujaribu kuwa wastaarabu kdg tunapotoa majibu maana ninachokielewa mimi, yawezekana wewe hukielewi. Anyway, vipi kuhusu vipimo navyo, mtu anaenda hospitali anaambiwa vipimo anavyotakiwa kufanyiwa haviko kwenye bima, akishafanyiwa kwa cash gharama za matibabu inaweza kuwa ni hundreds if not thousands of dollars wakati vipimo vili cost labda elf30 tu. Swala la gharama linakaaje apa embu tusaidie clinician
 
Hii nchi hata njia inazotumia kutatua kero nazo ni kero tu kwa wananchi mfano mkandarasi wa mchongo aliepewa zabuni ya kujenga mabanda toka mwaka jana hajamaliza hii inaashiria hakuwa na uwezo wafanyabiashara wanazidi kuteseka na Hali ya mvua zinazoendelea
Anzisha Uzi wa Kero umuanike huyo Mkandarasi.
 
Hii sio approach sahihi.
Sio kila mtu ana knowledge ya haya mambo, so tuwe tuna compare mwandiko wa dokta na catalogue ya NHIF kwel mkuu??

NHIFTZ wake na utaratibu rahis wa kutuwezesha sis kuthibitisha haya
Kama haujui kusoma si unamuomba hata jirani yako akusomee ili ujue hiyo dawa ipo au haipo. Muhimu hiyo orodha iwepo kwenye mahospitali notes board mgonjwa ataona mwenyewe.
 
Back
Top Bottom