DOKEZO Hospitali ya Kairuki wahuni wachunguzwe. Kila mgonjwa wa Bima anaumwa Helicobacter pylori (H. Pylori)

DOKEZO Hospitali ya Kairuki wahuni wachunguzwe. Kila mgonjwa wa Bima anaumwa Helicobacter pylori (H. Pylori)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wa Zamani sisi tulikuwa tunafikiria zaidi kufanya Kazi !

Wa sasa wengi wanafikiria Kutajirika wawe na magari mazuri majumba mazuri na wake wazuri na Bata kwa kwenda mbele na kuwatambia wenzao !
Nyerere alituonya kwamba mnauacha Ujamaa ??
Huko mbele mtaujutia 😳🙄 !
 
Helicobacter pylori (H. pylori) huu ugonjwa dawa zake bei zake ni kuanzia elfu 80. Hospital ya Kairuki hasa polyclinic Kairuki ya Mbezi Magufuli kila mgonjwa atakayepima choo wote wanaambiwa wana H. pylori. Ukiwa na Bima ya afya lazma uambiwe una H. pylori.

Nilipeleka mtoto wangu akaanbiwa hivyo mtoto wa miaka 3, wakampa madawa mengi aina km 5 afu zote za kumeza siky 14 hadi 30.

Shem wangu naye ambaye hatuishi nyumba 1 na yeye aliambiwa na H. Pylori, rafiki yangu hivyo hivyo.

Mimi mwenyewe jana nilipima nilikuwa siumwi chochote nikasema ngoja niwapime wakasema nina H. pylori.

Nikamchukua mtoto na mimi tukaenda kupima bochi na Kairuki kote tulikutwa hatuna hiyo H. pylori mtoto wangu amekutwa na matosi yanayompa homa basi.

Je, nyie hospitali ya Kairuki mmeamua kufanya biashara na miili yetu au?? Je, pesa ya bima ndiyo chanzo chenu cha mapato.

Serikali fatilieni hili swala. Wagonjwa wa bima kupewa madawa mengi na kuambiwa wanaumwa magonjwa mengi ili hospital wauuze dawa siyo fair.
Kama hili ni kweli, basi hao wahuni wachunguzwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Nadhani kama tungeweza wote kwa umoja wetu kubadilisha neno ujanja kulitumia na badala yake tukasema kuna Uwizi mwingi sana !
Neno Ujanja ni sifa ya mtu kuwa mwerevu sana ! Ambayo ni sifa nzuri !
Upo sahihi unaofanyika ni wiizi sio ujamja, ujanja ni credit
 
Back
Top Bottom