Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Awali, Mwanachama wa JamiiForums.com alitoa wasilisho kuwa kuna changamoto ya kukosekana kwa vifungashio vya dawa na hivyo inakuwa kero kubwa kwa wanaoenda kupokea kwa kuwa zinakuwa hatarini kuharibika.
Kusoma hoja ya Mdau, bofya hapa ~ Hospitali ya Rufaa Kitete mkoani Tabora haina vifungashio vya kubebea dawa
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora (Kitete), Dkt Joachim Joctan Eyembe ameelezea kuhusu hoja hiyo ya Mwananchi kwa kusema:
“Kwanza nashukuru sana JamiiForums kwa kutaka kusikia upande wa pili kuhusu sisi, hilo ni suala dogo ambalo linaweza kufanyiwa kazi ndani ya muda mfupi, nikimaliza mazungumzo na wewe hapa nitaenda kutoa maelekezo ili liweze kufanyiwa kazi.
“Hii ni hospitali kubwa na inakuwa na mambo mengi, wakati mwingine mambo madogo madogo kama hayo unaweza usiyatambue au kuyagundua kwa urahisi, ndio maana tumeweka vifaa ambavyo wananchi wanaweza kutoa maoni yao na kero mbalimbali wanazokutana nazo hapa hospitali kama zipo.
“Wakati mwingine inawezekana vifungashio vimeisha kwa muda ambao huyo mtoa mada alienda hapo kuchukua dawa, hivyo, nasisitiza tu kama suala hilo litafanyiwa kazi haraka.”