Voltaire
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 1,964
- 2,192
Ukisikia ujuha ndio huu sasa, yani watu zaidi ya 5000 umeua,alafu unataka tuamini unachokitaka wewe!"Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru imesikitishwa na kitendo cha watu wenye nia ya kuzua taharuki kwa wananchi kutengeneza video yenye picha za miili ya watu ikiwa na maelezo kuwa video hiyo imerekodiwa kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hii.
Tunapenda kukanusha kuwa video hiyo haina uhalisia bali imetengenezwa na kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii kwa nia mbaya ya kuchafua taswira ya hospitali yetu. Hivyo IPUUZWE.
Kama ilivyooelekezwa na Wizara ya Afya, tunatoa wito kwa wanaozua taharuki kwa kutengeneza video zenye kupotosha uhalisia kuacha mara moja na kuwaasa wananchi kujiepusha kusambaza video hii."
View attachment 3503155
Kwani hatujui ndugu zetu wamekufa na mmewazika kupoteza ushahidi?
Hawapo,hawakurudi baada ya maelekezo yenu ya kuwaua kutolewa, hii laana ndo inaenda kuleta Tz mpya!