Kipindi nimeingia dar nikiwa bado mwananchi mtiifu ,nilimpeleka mamangu ,na alikuwa Hana bima,nikatinga getini nikapokelewa na makamanda,nikaingia mpaka ndani tukiwa tunatembea na mama.kufika reception nikaulizwa nikasema nimemleta mama kutibiwa, wakaniuliza alishawahi kutibiwa hapa nikasema hapana,anatumia bima hapana,Kuna ndugu yako hapa nikasema hapana.wakanipeleleza kama nusu saa hivi nikasema basi ngoja nimpeleke kwingine,na kulikuwa na hali ya mvua hivi nikaondoka na mama na hatukuwa na usafiri ,tukiwa Bado tuko maeneo ya hospitali alikuwa kaka Moja hivi na gari akaniuliza mbona unamtembeza mama kwenye mvua akatupakia kwenye gari,akaniuliza mnaenda wapi nikamwambia nampeleka mama hospitali kairuki.alitupeleka na gari mpaka kairuki na kutufukisha akageuza gari na kuondoka.
Wale watu wako makini sana na Mimi nilienda pale kwa ajili ya kujaribu na kuona mazingira ya mle na kwa kwakuwa nilikuwa na mama na mama alikuwa umri umeenda nikasema ngoja nipaone hapa kwa makamanda