Hospitali ya Mzena inamilikiwa na nani? Kwanini iitwe Mzena?

Hospitali ya Mzena inamilikiwa na nani? Kwanini iitwe Mzena?

Hii hospitali wanatibiwa wafanyakazi wa Usalama wa Taifa na hata familia zao, ni kama hospitali nyinginezo za majeshi, tofauti ni kuwa miaka michache iliyopoita wamejenga wodi ya VIP ambayo Mkapa na Sita walifia hapo.
Ongezea na magu
 
Hii hospitali iko pale Makumbusho kwenye makaaazi yale ya usalama wa taifa
Ukitoka Makumbusho kama unaenda Moroco mkono wa kushoto kuna njia inaingia kuna majengo kama apartment kuna ulinzi mkali sana huwezi hata kusogea hapo nd usalama wa taifa wanapoishi na ndipo hiyo hosp ilipo
Wanatibiwa viongozi wakubwa pekee
Hata JK alipoangukaga jukwaani alipelekwa hapo... By the way kuna hospitali mbili mle ndani,moja ndo wanatibiwa wakazi wa mule ndani
 
Ipo eneo la Makumbusho, imepakana na kijiji cha Makumbusho upande wa kushoto ukiwa unaelekea eneo la Victoria. Ni kwa ajili ya viongozi na maofisa usalama na familia zao, ingawa nasikia wenye bima wanatibiwa. Ni hospitali nzuri kwa maana ya huduma, vifaa na utaalamu. Inamilikiwa na serikali, na imepewa jina la Mzena ikiwa ni kumbukumbu ya aliyewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emilio Mzena
Ukiwa na bima za kawaida? Na pale getini unapitaje?
[/QUOTE]
Hii ya viongozi kutibiwa huko siamini.viongozi wote Mbona wanajua muhimbili ?
 
Back
Top Bottom