Thread Starter
JF-Expert Member
- Mar 16, 2017
- 1,378
- 1,045
Hospitali ya MLOGANZILA itasimama yenyewe na kutoka chini ya usimamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia Julai 2022. Hayo yamesemwa leo 18/3/2022 na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu alipoitembelea Hospitali hiyo na kusema kuwa serikali imejiridhisha na jinsi hospitali hiyo inavyojiendesha na ni wakati umefika sasa hospitali hiyo ijitegemee.
Aidha katika hatua nyingine, waziri huyo wa Afya amezindua mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni (Oxygen Plant) hospitalini hapo, mradi huo umefadhiliwa na Ubalozi wa Korea nchini kupitia taasisi ya ''Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH)''
Soma pia: Hospitali ya MUHAS Mloganzila (MAMC) yawekwa chini ya uangalizi maalum wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
My take: Kwa maana hiyo uongozi uliokuwepo utavunjwa na wafanyakazi walioazimwa kutoka Muhimbili watarejea Upanga na taasisi itakuwa separate chini ya wizara, je mabadiliko haya yataleta tija kwa changamoto zilizoikumba tangu ianzishwe mnamo 2016-2017? Anyways tunatarajia mema na kila la heri wana Mloganzila katika kuisimamisha taasisi yenu bila kutegemea usimamizi wa Muhimbili Taifa au MUHAS..