Hospitali ya Taifa Muhimbili kutoisimamia tena Mloganzila, sasa Mloganzila kujiendesha yenyewe kuanzia Julai 2022

Hospitali ya Taifa Muhimbili kutoisimamia tena Mloganzila, sasa Mloganzila kujiendesha yenyewe kuanzia Julai 2022

Nililazwa Mloganzila for 8 days. Kwa kweli ni one of the best hospitals in the country if not the best.
Ukitibiwa Mloganzila hesabu uko kwenye mikono salama.
Pale alilazwa aunt yangu kipenzi japo alifariki tokana na complications za ugonjwa uliompeleka pale ila kwa standards na mazingira nadhani ni zaidi hata ya Aga Khan Upanga.
 
juzi tarehe 16/3 /2002 msikitini imamu katangaza mchango wa ndugu yake ya matibabu kapelekwa hospital iloganzila ilikuwa adhuhuri nilikuwa nimekaa na jamaa mmoja karibu yangu nikamwambia huyu ndugu wa imamu hawezi kupona tutamzika subiri uone ilipofika laasiri tukaendelea na mchango kukamilisha pesa laki 6 zinazotakiwa hospitali ilonganzila ilipofika magharibi tukatangaziwa mgonjwa kafariki
Noma
 
Wanasema"maneno ya watu sumu"
 
Hizo ni imani tu ndugu,wale watu wako vizuri na kwa kiasi kikubwa wanajitahidi mno.sisi tulikua na mgonjwa wetu Tulimpeleka pale alikua na hali mbaya sana kiasi kwamba tulikua tunajua hamalizi week tunazika.mgonjwa amekaa ICU week 3 anapumulia machine,lakini tuliziona juhudi za madaktari wa pale walivyokua wanamhangaikia pasipokuwapa hata chochote.mgonjwa wetu alipona na mpaka sasa yuko mtaani anadunda.
Sawa,tunashukuru Kama tunaweza pata angalau habari njema Kama hizi.
 
Hahaha..mimi binafsi najisikia poa tu, Ni kweli kumekuwa na changamoto za hapa na pale kwenye uendeshaji wa Hospitali hii, lakini karibia changmoto zote zinahusiana na ukosefu wa fedha tu!
Wakati huo huo, majority ya watu wanaotusema vibaya, hawajawahi kutibiwa, wamesikia tu kwa watu! Ambao nao walisikia kwa watu....and the chain goes on...
Kwa watu ambao wametibiwa hospitalini hapa, wengi wana ushuhuda mzuri tu na hospitali hii!
Lakin comments ni nyingi chief zinazoisema vibaya hospital sio wa kupuuzwa hawa.
 
Nililazwa Mloganzila for 8 days. Kwa kweli ni one of the best hospitals in the country if not the best.
Ukitibiwa Mloganzila hesabu uko kwenye mikono salama.
Mmmmh hii hatareeee, mloganzira ipi? Au ya Uingereza?
 
Wewe nadhani umesikia tu kwa watu, na hao watu walisikia kwa watu! Tuna wagonjwa wengi tu, wanakuja bila fahamu, wanahudumiwa na kupona kabisa, baadhi pia hufariki sio kwa kukosa huduma, bali hatua ugonjwa wao ilikuwa juu sana kiasi kwamba isingewezekana kuzuia vifo vyao!
Uongo nyie wafanyakazi ni wazembe khaaaah
 
Hospitali ya MLOGANZILA itasimama yenyewe na kutoka chini ya usimamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia Julai 2022. Hayo yamesemwa leo 18/3/2022 na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu alipoitembelea Hospitali hiyo na kusema kuwa serikali imejiridhisha na jinsi hospitali hiyo inavyojiendesha na ni wakati umefika sasa hospitali hiyo ijitegemee.

Aidha katika hatua nyingine, waziri huyo wa Afya amezindua mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni (Oxygen Plant) hospitalini hapo, mradi huo umefadhiliwa na Ubalozi wa Korea nchini kupitia taasisi ya ''Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH)''

Soma pia: Hospitali ya MUHAS Mloganzila (MAMC) yawekwa chini ya uangalizi maalum wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

My take: Kwa maana hiyo uongozi uliokuwepo utavunjwa na wafanyakazi walioazimwa kutoka Muhimbili watarejea Upanga na taasisi itakuwa separate chini ya wizara, je mabadiliko haya yataleta tija kwa changamoto zilizoikumba tangu ianzishwe mnamo 2016-2017? Anyways tunatarajia mema na kila la heri wana Mloganzila katika kuisimamisha taasisi yenu bila kutegemea usimamizi wa Muhimbili Taifa au MUHAS..

Hilo jina lake lilivyo limekaa kichawichawi
Kwa nini wasibadiri jina tu ?
 
Back
Top Bottom