KERO Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Madaktari wanafunzi ni Janga. Watu wanakufa kwa uzembe

KERO Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Madaktari wanafunzi ni Janga. Watu wanakufa kwa uzembe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hii hospitali kama serikali na uongozi hautachukua hatua za haraka watanzania wengi wataendelea kufa kwa uzembe wa madaktari wanafunzi ambao hawasimamiwi ipasavyo na wakuu wao kazi.

Nimeshuhudia mgonjwa wangu akiambiwa hana tatizo lolote la nyonga baada ya kumpeleka akiwa amepata ajali na daktari ambaye ni mwanafunzi kusoma vipimo akatuambia mgonjwa aendelee na dawa alizopewa ( tulianzia matibabu hospitali ya wilaya kabla ya kwenda hapo mloganzila)

Tulipata mashaka na tukarudi tena kuomba uchunguzi zaidi ndipo daktari msimamizi wa mwanafunzi huyo alipokuja nadhani alikua kikaoni na baada ya kupitia tena vipimo alibadilika ghafla na kuwa mkali sana na kumfokea yule daktari mwanafunzi kuwa kwanini hajaona tatizo la nyonga kuvunjika? Na ni eneo hatari sana kwa mgonjwa? Japo alikua akimfokea kwa kiingereza ila tuliweza kujuwa kuwa daktari mwanafunzi alizembea katika matobabu ya ndugu yetu.
Nashukuru tumepangiwa tarehe ya operesheni. Ila nimeondoka na maswali mengi kichwani je ni wagonjwa wa ngapi wanaopitia hali kama tuliyopitia sisi?

Naomba serikali na uongozi mzima wa hospitali ya taifa ya Muhimbili (mloganzila) kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha ya watanzania.
Huwa nawaambia watu MD 's fake na incompetent ni wengi mno, diagnosis capability yao ni below 50%
 
Wakubwa wao wako busy sites za dada poa wanatafuta huduma...umkute ofisini hapo kavaa miwani yake kwny computer utajua anafanya kazi ya maana kumbe upupu...kama ni wanawake wapo busy na majungu kusemana...hii nchi Magufuli ndo aliwakomesha watumishi wa uma...kwa sbb alisikiliza kero direct na kutake actions...hapa mpk kijiji kipuputike ndo bi mdashi ataongea...
Mkuu kuna watu wata kuja kusema kama una mpenda kazikwe nae chato, au,uta itwa sukuma geng.
 
Mkuu kuna watu wata kuja kusema kama una mpenda kazikwe nae chato, au,uta itwa sukuma geng.
Hapana kuna mazuri alikua nayo lazima tuseme..na mapungufu yake yalikuwepo mengi tuu..as a human being..kwani bi tozo mbona ana mazuri yake? Na mapungufu kibao...
 
Usitegemee huyo mwanafunzi kilaza atabadilika akiwa daktari.

Ni mwendo wa kutumbuliwa majipu ya makalio kwa plaizi.

Cc: DR Mambo Jambo Poor Brain
Siku hizi kuna Elimu basi watoto wetu wengi wana fata Sehemu yenye pesa ili waweze kujipatia pesa isiyo na shuruba bhasi ila uelewa wa kungamua magonjwa hawana hawana passion ya Udajtari wala ya Kitabibu..

Hilo sipingi kabisa
 
Nini maana ya neno "mloganzila?". Neno "mloga" ni kinyambulishi cha neno "kuloga" kuwangiwa. Kwahiyo ni hospital ambayo hakuna matumaini!
"loga" ni "ulozi", Mloga ni Mtu anaye fanya ulozi. "Nzila" ni njia au barabara.

Sasa ukiunganisha haya maneno mawili unampata gwiji wa kuloga hata vitu visivyo na uhai. Huyo si mwingine bali ni MLOGA NJIA, MLOGA BARABARA. Sasa tafiri ya maana hii na hali halisi watafuteni Wazaramo wa naeneo hayo watawaambia kwa nini huyo jamaa alifikia kuloga hadi njia au barabara. Je alikuwa mhalifu kiasi akaloga ili asiweze kufikiwa kirahisi na wabaya wake? Tafakari mwenyewe.
 
Back
Top Bottom