Hospitali ya Taifa Muhimbili yajibu hoja za Wana JamiiForums kuhusu vifo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila

Nilianza kuisikia zaidi Mloganzila mwakajana, wakati ndugu yangu akiwa amelazwa hapo. Naye hakuishi tena.

Kwa sasa kuna ndugu yangu anatibiwa hapo. Amefanyiwa upasuaji mara 3, hakuna mabadiliko makubwa. Siamini kuwa inatokana na ukubwa wa tatizo, uwezekano mkubwa ni huduma ya kiwango cha chini.

Majengo tulijengewa na Wakorea Kusini, ni mazuri, yanapendeza. Vifaa tiba navyo ni msaada, na vimejaa sana.

Baada ya kufuatilia kwa wataalam wa pale Muhimbili, taarifa nilizopewa na maprof. watatu tofaiti, ni kuwa hatuna wataalam wenye uwezo wa kuvitumia vifaa tiba vya kisasa vilivyopo pale.

Hata huyu prof. aliyeitoa hii taarifa, kama utakutana naye kama mtu binafsi, hatakosa kukuambia ukweli wa tatizo la Hospitali ya Mloganzila.

Bahati mbaya serikali yetu inaamini tuna uwezo wa kila kitu. Hatuna mipango ya kuwapeleka watu kwenda kujifunza nje ya nchi.

Jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Kikwete mpaka kupata msaada huu mkubwa toka South Korea, zimeshindwa kufikia matarajio yake.

Ukweli ni kuwa:

HOSPITALI YA MLOGANZILA INA VIFAA TIBA VINGI VYA KISASA AMBAVYO MADAKTARI WETU HAWANA UWEZO WA KUVITUMIA.

Kama serikali itaendelea na huu utaratibu wa kuzuia watu kwenda kusoma nje, yaliyopo Mloganzila, msitarajie yatabadilika.
 
Yaani umenena.... maana 10% ya 10 ni 1 while 10% y 1000 ni 100... hutakiwi kuona sahihi kwamba wafe tu hao 100 kwa vile waliokuja walikuwa wengi.... unajua hata akifa mmoja, AKIWA NDO MTEGEMEZI WENU, KWENU NYIE, NI SAWA NA KUSEMA WAMEKUFA WOTE
 
Nafikiri bado jitihada zinahitajika kwenye kuboresha sekta ya afya, sina uhakika madai ya kipindi kile yaliyopelekea mgomo mkubwa wa madaktari yalifanyiwa kazi
 
Wanacheza na watu wenye akili ndogo. Kilicho dhahiri, kuna huduma duni sana. Mapato makubwa ya hospitali ni gharama ya utoaji miili.

Mloganzila inanikumbusha riwaya ya Houseboy niliyoisoma nikiwa sekondari. Baada ya Toundi kupigwa sana na polisi, akiwa taabani alipelekwa hospitali moja ambayo mtaani ilijulikana kwa jina la, "NON RETURN HOSPITAL". Toundi alitoroka bila ya kupata matibabu, akaenda kufia msituni. Kukataa matibabu ya NON RETURN HOSPITAL was his last protest to colonialism.

Nadhani kuna siku, mgonjwa akiambiwa rufaa yako ni kwenda Mloganzila, atasema, hapana aheri nifie zahanati.
 
Huu mtihani wa form 4 au 6? Mbona simple hivyo, maswali mengi yapo level ya chini kabisa ya cognitive domain, acha psychomotor na affective domain zipo kidogo sana, na tunaongelea competence based curriculum, hata kama ni paper one! Form six anaambiwa Mention, list, identity, Name, explain etc very low level ya kupima competence ya A level candidate, halafu eti 10 marks! ndio maana wengi siku hizi wanapata hizo PCB AAA, sio kama miaka yetu! NECTA wajitafakari kwa kweli. Samahani kama nimeongea some terminologies kwa wengine ngeni, ila walimu na wengine wanaopenda kujiongeza kielimu watakuwa wamenipata vizuri kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hospitali kama huna, connection kumwona Daktari bingwa labda ufe ndio ufanyiwe post mortem.. Watu wanatibiwa na AMO tu.
 
HALAFU WANASOMEA MITIHANI TU SIO KUELEWA YAANI KUNA ULAZIMA WA KUBADILISHA MITAALA
 
Nafikiri tatizo kubwa ni kuwaachia wanafunzi kufanya majaribio katika miili ya wagonjwa, hivi kweli inaingia akilini wagonjwa wametolewa huko kwingineko ili kupata huduma ya uhakika halafu mgonjwa huyo anakutana na mwanafunzi ambaye naye yuko katika kujifunza!!!

Kuna siku nilikuwa Muhimbili mama, kuna mgonjwa alikuwa kakabidhiwa kwa hao hao wanafunzi, uzuri kulikuwa na specialist ambaye alikuwa akiwaongoza, picha niliyoiona pale asingekuwepo huyo Dr. tiba isingekwenda kama inavyotakiwa maana yule msimamizi alikuwa akiwapatia maelekezo wao wakadai mwl. wao hakuwafundisha hivyo aliwafundisha vinginevyo..Yule Dr. akawa mkali kwa kuwaambia fuateni ninachokisema.
 
afadhali umeliona
 
Ongezeko la wagonjwa asilia mia 48 inatisha. Nini chanzo cha ongezeko hili la kutisha?
 
Hawa Muhimbili mwez wa 11 wameniulia dada angu kwa kuwekewa damu ambayo sio group lake, alafu mwez wa 12 wameniulia mdogo wangu (presha ilishuka wakashindwa kumuwekea fluid) yaan wamejaa maintern usiku hawakai wodin nna hasira nao sana....
Maintern hapo ilogazala hosital wanapomtibu mtu ikija msg kwenye simu anamuacha mgonjwa anaanza kujibu msg huku akicheka kuhusu wanavyoambizana kwenye msg.huku Mgonjwa anazidi kuwa mahututi akirudi kumhudumia anasahau mgonjwa alikuja hapo anaumwa nini akili yake kwenye msg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu acha kutudharau tuliofanya hii paper, mimi niliambulia D hapa. Ingawa kuna paper 2 na 3 hujaziweka hivo hatuwezi kulinganisha uwiano na ugumu wa mtihani mzima.

Alie weka huu mtihani Kwa kuubeza ni dhahiri hajasoma Somo la Biology A, level. Na hata Kama alisoma huko O, level, basi Hali yake ilikua mbaya Sana.
Nadhani atakua amesoma masoma ya art.
Tumsameheni.

Huu mtihani ni standard.
 
Hawa Muhimbili mwez wa 11 wameniulia dada angu kwa kuwekewa damu ambayo sio group lake, alafu mwez wa 12 wameniulia mdogo wangu (presha ilishuka wakashindwa kumuwekea fluid) yaan wamejaa maintern usiku hawakai wodin nna hasira nao sana....
...eti hao wanafunzi wanakuwa bize na smartphone zao badala ya wagonjwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…